Hadithi ya chongo watatu

By Rajabu Athuman

CHONGO WATATU NA WANAWAKE WA BAGHADAD

HATITHI YA CHONGO WATATU WATOTO WA WAFALME NA WANAWAKE WA BAGHDAD


Hapo zamani katika nchi ya Baghdad kulikuwepo na mbeba mizigo maarufu sana. Alikuwa ni kijana asiyepunguwa miaka 40, na alisifika kwa nguvu na akili sana na uwezo wa kufikiri alio nao. Alipendwa sana na watu na aliheshimika pia. Siku moja laikuwa amekaa eneo lake la kila siku kusubiri wateja, ghafla akatokea binti mmoja mrefu wa kiarabu. Binti huyu alimfanya mbeba mizigo amtazame sana kwa muda mrefu kwa uzuri alonao binti huyu. Binti akamwambia yule kijana nifate. Kwa haraka zaidi kijana akanyanyuka na kuanza kufata.


Wakafika kwenye nyumba moja yule binti akagonga mlango kwa madaha, mzee mmoja akatoka, binti akatia mkono kwenye mkoba wake na kutoa pesa nyingi na akampa yule mzee. Bila ya kuzungumza mzee alijiwa kinachotakiwa aliingia ndani na akaja na chupa kubwa lililojaa pombe. Kijana akabeba mzigo ule na kuuweka kwenye kapu lake kubwa la kubebea mizigo. Wakaelekea kwenye duka la matunda, hapa wakanunua matunda ya aina nyingi sana. Kisha wakafika duka lingine wakanunua vitu vingi sana vya harufu nzuri. Kwa urembo alonao huyu binti unaweza kufikiri ni vitu gani vya harufu nzuri angechukuwa. Kijana akamwambia “binti bora ungenambia toka mapema kama una mizigo mingi ili nichukuwe punda ama ngamia”. Binti akaheka sana na akamwambia “sijamaliza bado”.


Mambo yakawa hivyo waliendelea kununua vitu vingi katika matunda na vyakula na vinywaji. Vitu vya kunukia maua, mafuta pafyumu nna vinginevyo viingi. Wakafika kwenye nyumba mija mzuri sana, yule binti akaenda kuginja kwa madaha na upole zaidi kwenye malngo wa geti la nyumba hivyo. Muda wote kijana alikuwa akifurahia uwepo wa binti huyu na kila analofanya. Basi akatoka binti mwingine wa makamo aliyeonekana mzuri zaidi kuliko huyu na akafungua mlango.


Muda wote kijana alikuwa akishangaa na macho yake yaliganda kwa hutu mfungua mlango. Baada ya muda yule binti akamwambia “tafadhali ingia ndani”. Hapa kijana fahamu zikamrejea kwa shauku akaingia ndani. Alishangaa sana uzuri ulioje wa ndani pale. Nyumba yenye kila kizuri anachokijuwa na ambavyo ndo alianza kuviona. Kuna vinyago vya dhahabu na chemchem za maji. Meza yz almasi na sakafu yenye marumaru za kuvutia zaidi.


Kila kilichopo ndani hapa kilimflaisha kijana, ila zaidi ya hapo kilichomshangaza zaidi pale ndani kuna kiti kikubwa na zizuri. Aliyekaa kwenye kiti kile alikuwa ni dada mmoja mzuri sana huenda aliwashinda wote pale ndani. Kijana alifikiri yule ndo mkubwa wao, na huu ndo ukweli. Yule aliitwa Zubeida na yule alokuja nae kutoka kwenye bidhaa ni Sadie na yule alofungua mlango aliitwa Amina. Basi amina aliingiza mizigo ndani na sadie alitowa kiasi chapesa na kumpatia kijana.


Kijana aliendelea kushangaa pale ndani kwa muda mpaka zubeida akauliza “vipi kaka mbona hauondoki? Au unataka pesa zaidi?”. Kijana akaanza kujitetea kuwa angependa kukaa kidogo na akaleta hadithi nyingi na baadae wakamruhusu aendelee kukaa kidogo. Zubeida akamwabia “basi nitakuruhusu kukaa kwa sharti uwe mpole na usitowe siri ya maisha yetu hapa”. Kiana akakubaliana na sharti na akawajibu “nitatunza siri za humu ndani kuliko alivyotunza siri kinyozi wa mfalme”. Kwa shauku Amina akauliza “alifanya nini kinyozi wa mfalme?”. Kijana akamjibu amina “ni hadithi ndefu kidogo”. Akadakia Sadie “tusimulie basi hiyo hadithi ya kinyozi”. Kijana akamuangalia Zubeida aliyekuwa akimuashiria awaridhishe ndugu yake. Basi kijana akaanza kusimulia hadithi kama ifuatavyo;-


HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME.
Hapo zamani za kale katika nchi moja kulikuwepo na mfalme aliyependa kufuga nywele. Mfalme huyu alikuwa akinyowa nywele zake mara nne kwa mwaka. Mfalme huyu alipenda kuvaa kilemba kichwani kama ilivyo kawaida katika tamaduni za kiislamu. Watu wengi walipenda uvaaji wa mfalme wao na yeye alilijuwa hili kwa muda mrefu. Kumbe mfalme alikuwa anasiri kubwa katika uvaaji ule. Mfalme alikuwa akinyolewa na kinyozi maalumu. Ilipita masiku na miaka mingi hata yule kinyozi wa mfalme akafariki. Ilibidi mfalme atangaze kumtafuta kinyozi mwingine. Uchunguzi ulifanyika kumtafuta kinyozi muadilifu na mwenye maadili. Zaidi ya sifa hizi mfalme alitaka kinyozi mwenye sifa ya kutunza siri. Sifa hii aliitaka mfalme kwa kuwa kuna siri kubwa kwenye kichwa chake. Basi alipatikana kinyozi mmoja kijana mwenye familia ya watoto wanne. Alikuwa ana maadili mazuri na ni muadilifu pia.


Ilitokea siku moja mfalme akataka kunyolewa. Akamuita kinyozi wake na kumwambia “kwa mara ya kwanza ndo unakiona kichwa changu, utakachokiona kwenye kichwa changu iwe siri yako mpaka utakapoingia kaburini”. Kinyozi akaapa mbele ya mfalme kuwa katu hataizungumza siri ile kwa yeyote. Kinyozi kufunguwa kilemba cha mfalme alishikwa na mshangao kkubwa baada kuona siri kubwa katika kichwa cha mfalme. Kinyozi akajuwa kumbe hii ndio sababu ya mfalme kuvaa kilemba na kufuga nywele.


Basi kinyozi yule alikaa na siri ile kwa siku nyingi sana. Alithubutu hata kukimbia nchi kwa kuogopa kutoa siri ya mfalme. Hali iliendelea kama hivyo anamnyoa kinyozi na anaenelea kutunza siri ya mfalme. Kama ujuavyo siri ikikaa sana kwenye moyo utadhani moyo unataka kutumbuka. Kinyozi akawaza hii siri ya mfalme siwezi kuotoa nitafanya nini sana. “ningejua kama mfalme ana pembe katu nisingekubali kukifunua kichwa cha mfalme”. Ni maneno ya kinyozi.


Basi siku moja akatoka na chepe lake na jembe kwenda porini. Kufika kule akachimba shimo kubwa mpaka kiunoni. Baada ya hapo akainama na kuanza kuimba “mfalme anapembe, mfalme anapembe”. Aliimba hivi kwa muda mpaka alipoona moyo wake umetulia na umepoa kwa kuiweka siri ya mfalme kwa muda. Basi baada ya hapo akafukia shimo lake na akaondoka kurudi nyumbani. Haukupita muda mrefu shimo like likaota majani na pakaota mti mkubwa sana.


Ni miaka 15 sasa imepita toka mti ule uote sasa mti ule ukabakia na siri ile aloiacha kinyozi miaka 15 iliyopita. Mti ule ulipofikia kutoa maua ukawa upepo ukaja unarudia ule mwimbo wa alouacha kinyozi miaka 15 ilopita. Hivyo ukaja upepo mti unaimba “mfalme ana peembe mfalme anapembe, waaa waaa waaa”. Ikatokea siku moja wawindaji wakapita karibu na mti ule wakastaajabu kusikia wimbo wa ajabu unaozungumza kuwa mfalme ana pembe.


Basi habari zikaanza kusambaa kwa kasi sana mpaka ikamfikia kinyozi. Watu wakawa wanafunga safari kwenda kuuangalia mti uanoimba kuwa mfalme ana pembe. Habari zilisambaa mpaka zikamfikia mfalme. Mafalme akatoka na msafara wake nae akashuhudie mti unaotoa siri yake ya pembe kichwani. Alishangaa sana, ilibidi siku ilofata aitishe mkutano mkubwa kwa kila atakaetaka kuhudhuria kwenye eneo lile lenye mti ule.


Basi watu walikusanyika sana eneo lile, watoto, wazee na vijana walimwaika eneo lile la tukio. Baada ya muda watu walipokusanyika akasimama na kuanza kuhutubia, kisha akavua kilembe chake watu wote wakashuhudia pembe kichwani mwake. Kisha akasema “nimeamini hakuna siri”. Na huu ndio mwisho wa hadithi ya kinyozi msiri wa mfalme. Basi Amina na Sadie walifurahi sana na wakamruhusu kijana aenelee kubakia pale.


Basi pale ndani chakula kikapikwa na watu wakawa wanakula na kunya na kufurahi. Mashairi yaliimbwa na furaha zaidi. Wakatowa pombe wakanywa na wakaendelea kufurahi pale ndani. Nyakati za swala pia ziliwapita palelpale walipokaa. Mapaka wanakuja kutambua ni jioni na kigiza kinakaribia kuingia. Zubeida akamwambia kijana “amka uende zako, muda wa kutengana na wewe umekaribia”. Kijana akaanza kujitetea tena kuwa amelewa sana hivyo hataweza kufika kwake. Kama watamruhusu alale pale mpaka kesho ataondoka na kurudi kwake.


KUINGIA KWA WAGENI
Amina na Sadie walimuonea huruma wakamuomba Zubeid amruhusu abakie. Basi Zubeida akamwambia “naongeza sharti lingine kuwa usiulize chochote kwa utakayoyaona yanafanyika hapa ndani”. Kijana kwa mara nyingine anakubaliana na sharti hili. Basi pale ndani furaha iliendelea mpaka waliposikia mlango unagongwa. Sadie akaenda kufungua akakuta kuna watu watatu kwa mavazi yao wanaonekaa ni wageni katika mji ule. Walikuwa wote wanachogo jicho la kulia, na wamenyoa nyusi zao na vichwa vyao ni kipara. Wageni hawa wa kushangaza walikuwa wanamuomba Sadie hifadhi ya kuwaruhusu walale pale kwa leo.


Sadie akarudi kwa dada zake kuwaambia kilichopo mlangoni, Zubeida alionekana kutokukubaliana na ugeni huo Sadie akadakia “dada waruhusu walale bila shaka mtawafurahia, maana wanapendeza kweli” kwa shauku Amaina alitaka kujuwa wakoje wageni hao, “wote ni vipara na hawana nyusi upande wa kulia na waote ni chongo jicho la kulia, na wanaonekana ni wageni wa huu mji, bila shaka ni wasafiri” alisema Sadie. Basi Zubeida alijubali kuwaruhusu ila akamsisitiza Sadie awape shari la kukubaliana na kilichoandikwa mlangoni.


Wageni wakaingia ndani na bila kusahau Sadie akawaashiria wasome maandishi yaliyopo malangoni “USIULIZE CHOCHOTE KATIKA MAMBO UTAKAYOYAONA HUMU NDANI” wageni walionesha ishara ya kukubaliana na sharti hili. Basi nyumba iliendelea kufurahia, mmoja ya wale wageni akaomba apewe filimbi, na akaanza kupiga na mwenzake mwengine akawa anaimba na mwenzao mwengine akawa anacheza. Wimbi uluwafurahisha sana wakina Amina na Sadie. Zubeida alionekana kupenda zaidi namna ya yule aliyekuwa akicheza.


Basi mabo yakawa kama hivyo, furaha ilienea sana ndani mule. Siku hiyo mfalme wa nchi hiyo alikuwa anafanya uchunguzi wake akiwa amefaa nguo za kiraia zinazofanana na wafanyabiashara. Basi walipofika jirani na nyumba ya wakina dada hawa walisikia vifijo na furaha iliyoenea nyumbani pale. Basi kwa shauku kubwa mfalme alitaka kujuwa ni wakinanani hao. Na kwakuwa alifaa mavazi ya wafanya biashara haikuwa rahisi kumtambua. Basi akamuamuru waziri wake akagonge mlango. Waziri akafanya kama alivyoambiwa, na akagonga mlango akatoka Sadie kuja kufungua mlango. Akakuta wafanya biashara watatu waliovaa mavazi mazuri ya kupendeza.


Sadie akaingia kwenda kutoa taarifa ndani kwa dada zake, “dada ni wageni watatu wanataka hifadhi, wamekuja nchi hii hawana wanaemfahamu hivyo wanaomba hifadhi ya kulala kwa leo tu” ni maneno ya Sadie akiwaeleza dada zake. Baada ya mashauriano Zubeida akaruhusu wapate hifadhi lakini kwa shart lilelile liloandikwa kwenye mlango wao. Basi Sadie akawakaribisha na kuwapa sharti lile waliopewa wale wageni kwa kwanza. Basi furaha ikarejea pale ndani na vinywaji na vyakula vililiwa na wachezaji na waimbaji wakaendelea. Waziri alikuwa muda wote anadukuduku la kutaka kujuwa kwa nini pale kuna chongo watatu, wote upande wa kulia wamenyoa nyusi na ni vipara. Wakati anataka kuuliza Sadie akadakia “jua mambo yako usiulize kitu usije ukajuta”.


Haliiliendelea hivyo mapa Zubeida aliposimama na kuwaambia ndugu zake “HAYA MUDA UMEFIKA TUANZA SASA”. Basi pale Sadie akaanza kusafisha pale ndani na kupangilia kila kitu kwenye sehemu yake. Kisha akawataka wageni wote wakae kwenye viti na pale ndani pabakie pakiwa safi. Kisha sadie akamuomba kijana mbeba mizigo aje amsaidie. Wakaingia ndani na kuja na mbwa wawili wakiwa wamefungwa nyororo katika shingo zao. Zubeida akiwa amekaa kwenye kiti kile kirefu akaagiza aletewe moja kati ya wale mbwa. Basi Sadie bila kuchelewa akampelekea mbwa yule. Zubeida akambusu mbwa yule kisha akasema “je tuanze?”. Hakuhitaji kujibiwa swali lile. Basi akachukuwa mjeledi akaanza kumchapa mbwa yule kwa muda mrefu mpaka akachoka. Akapunzika kidogo na kuendelea. Alipomaliza akamshika yule mbwa miguu ya mbele na kuanza kumfuta machozi. Akajifuta na yeye pia kisha akambusu kwa mara nyingine. Kisha akaagiza aletewe mbwa mwingine na yule arudishwa, Sadie akatii maagizo. Mbwa wa pili alifanyiwa kama alivyofanyiwa yule wa kwanza.


Wakati mambo yote haya yanafanyika, wageni walikuwa wakigusana gusana kwa shauku ya kutaka kujua hasa ni nini kinaendelea. Mfalme aliyejifanya mfanyabiashara akawa anampa maagizo waziri wake kuuliza lakii waziri akajifanya hakusikia. Wakati mambo yanaendelea pale ndaubaida akamuita Amina na kumwambia “njoo Amina ufanye kazi yako”. Muda uleule Amina akaja na vifaa vyake vikaletwa pale na Sadie.kukaletwa filimbi, nguo, kioo na vitu vingine.


Basi Amina akawa anaimba mashairi kwa filimbi ile mpaka akapoteza fahamu. Walati huo watu wote wakawa wanashangaa kinachoendelea pale ndani. Basi Sadie akaja na kumpepea dada yake na kumpunguzia mavazi, basi mfalme na wenzie wakaona akovu mengi ya kutisha yaliyopo kwenye mwili wa Amini. Mara hii mfalme alishindwa kujizuia kwa shauku akataka kujuwa ni vitu gani vinafanywa pale ndani, kwa nini mbwa wamepigwa vile na ni kwa nini huyu dada ana makovu makubwa na ya kutisha kwenye mwili wake?. Basi waziri kumridhisha mfalme akamuuliza moja kati ya chongo “hebu tuambieni nyinyi wenzetu mlikuwa hapa ni mambo gani haya tunayo yashuhudia?”. Chongo akawajibu “mmh hata sisi hatuna ujuzi wa kujua mabo haya, sisi pia tumekuja muda si mrefu kabla ya kuja kwenu, lamda tumuulize kijana mbeba mizigo huyu maana tumemkuta. Huenda akawa na habari ya mabo haya”. Majibu ya kijana yakawa yaleyale hatambui kinachofanyika hapa.


Basi wakiwa katika hali ya kunong’ona pale ndani ghafla Zubeida akanyanyuka na kuwaambia “mnanini hapo? au mmesahau sharti tuliowapa kabla ya kuingia ndani hapa?”. Kijana akajibu “heti wananiuliza wanataka kujuwa maana ya mabo haya mmnayoyafany ahapa.”. Watu wote pale walikuwa tayari hata kufa lakini wajue maana ya mambo yale. Zubeida akauliza tena “ni kweli anayosema mwenzenu?”. Wote wakaitikia “naam, hasa ni kweli kabisa”. Zubeida akaoka pale kwenye kiti chake akiwa maekasirika sana na kuanza kusema “tumewafadhili hapa na tukawapa sharti moja tu lakini limewashinda. Sasa mnataka kujuwa mabo msiyopasa kuyajuwa.”. Kisha akaita “njooni”


Muda uleule wakaja walinzi wa ndani pale na kuwaekea kisu shingoni kwa kila mmoja pale ndani.


“sasa wote mtakufa kwenye mikono ya walinzi wangu hawa au kula mmoja anieleze habari yake hata bila ya kudanganya” kusikia maneno haya mfalme akafurahi kwa sababu wakisikia kuwa yeye ni mfalme wasinge muua. Basi Zubeida akamwenea kijana mmemba mizigo na kumwambia “tueleze habari yako bila ya kudanganya na umefika vipi hapa?” kwa sauti ya woga kijana akaanza kuzungumza kuanzi apale asubuhi alipokutana na Sadie maka alipofika pale ndani.


Baada ya kwisha kutaja hadithi yake kijana akaruhusiwa aondoe ke muda uleule. Akapiga magoti mbele ya Zubeida na kumwambia “dada naomba ufanye haki kati yetu, wao wamesikiliza hadithi yangu na mimi nataka Kimoyoni alikuwa akiwaza kusikiliza hadithi za hawa vichongo watatu. Basi Zubeida akamwendea moja ya chongo wale na kumwambia ahadithie hadithi yake. Kichonho yule akanza kusema “kwanza jua ewe dada mkubwa wa nyumba hii kuwa sisi unaotuona ni chongo wote ni watoto wa wafalme katika tawala mbalimbali. Kila mmoja anastori yake ya kustaajabisha kuhusu chongo yake. Basi wakaanza kuhadithi stori zao kama ifuatavyo;-


HADITHI YA CHONGO WA KWANZA MTOTO WA MFALME
kwanza utambue mimi ni mtoto wa mfalme na ni wa kipekee katika uzawa. Hivyo kwa upekee wangu nilipokea mapenzzi makubwa kutoka kwa baba na mama. Mama yangu alifariki nikiwa mdogo. Hivyo kwa muda mrefu nilibaki na baba yangu. Nilikuwa napenda kuwinda ndege kwa kutumia mishale. Nilikuwa nikitembea na waziri mkuu ninapokwenda kuwinda.


Sikumoja tulipokuwa mawindoni nilikuwa nikilenga shabaha shingo ya ndege aliyejificha kwenye kitundu chake. Bila ya kujuwa hili wala lile kumbe waziri alikuwa nyuma ya kile kitundu nae akimvizia yule ndege. Nikarusha mshale wangu na kumpata waziri kwenye jicho. Waziri aligugumia sana kwa maumivu makali yaliopelekea kupata chongo. Nilimuomba msamaha lakini alionesha kutokuridhia na kuamini kuwa nilifanya kwa makusudi.


Tulivofika nyumbani nikamueleza baba stori mzima hapo baba akamuita waziri na kutaka kumfariji. Waziri hakutaka chochote na mwisho aliahidi kuwa lazima alipe kisasi kwa yaliyompata. Tulikaa kwa muda mrefu hata nikasahau tukio lile. Nilipata safari ya kwenda kumuona mjomba wangu ambae pia ni mfalme aliyekuwa ni jirani na utawala wa baba. Mjomba huyu nae alinipenda sana. Wakati mwingiune hunambia anaponiona eti namkumbusha marehemu dada yake.


Mjomba alikuwa na kijana wake mmoja ambaye ni binamu yangu. Mimi na kaka huyu tulukuwa marafiki sana tulipokuwa wadogo. Hata hivyo urafiki wetu uliendelea hata nilivyokuwa mkubwa. Nilikwenda kwake kumsalimia. Kwakweli alifurahi sana uwepo wangu. Tulizungumza mengi sana na kufurahi pia. Tulipokula chakula cha usiku akanambia “kuna kitu nataka nikuoneshe, nilikuwa ninakiandaa toka ulipoondoka wakati ule”. Basi akachukuwa taa na kuniambia nimfate.


Tulikwenda kwa muda wa usiopungua dakika 20 na tukakuta nguzo mbili zilizokaa mfano wa mlango. Tulipofika pale akanambia nifukue pale chini. Bila kuchelewa nikatafuta mijiti na kuanza kuchimba pale. Urefu wa shibri moja nikakuta zege, akanambia “fungua huo ni mlango”. Nikafungua na kukuta ngazi. Tukachuka kwenye ngazi ile na kukutana chini kuna mfano wa mlango ndani ya handaki. Akfungua mlango ule na tukaona nyumba nzauri sana. Akanambia “turudi sasa hiki ndio kitu nilichokuwa naandaa, nakuomba usimwambie mtu jambo hili”.


Basi tuliporudi siku ile sikuweza kulala usiku nilikuwa nikiwaza ni la nini jumba lile na ni kwa nini anafanya siri. Niliwaza mengi mpaka nikapitiwa na usingizi. Siku ilofata tuliendelea kufanya mabo ya kawaida mpaka. Baada ya wiki tatu binamu yangu aliniita na kunambia niende nyumbani kwake muda wa usiku. Basi nikaenda na kunambia kuwa “kuna mwanamke atakuja hapa umchukuwe wende nae pale kwa siku ile na mimi nitakuja baadae.


Mambo yakawa kama vile haikupita muda yule mwanamke akaja na nikaenda nae mpaka pale. Hatukukaa sana binamu yangu akaja akiwa amebeba mfuko wa sementi na nyumdo na chepe. Bila ya kuzungumza na mtu alipofika pale akaanza kufukuwa mpaka akaikuta ile zege. Akafungua mlangomule na kushuka yeye na yule mwanamke kisha akanambia “ahasante sana nakushukuru wewe rudi na usimueleze yeyote jambo hili”. Basi akaziba ule mlango na mimi nikarejea nyumbani.


Nilikaa siku tatu kisha nikarejea kwa baba. Nilipofika kule nilishangaa sana mambo yamebadilika sana. Nilipouliza wakaniambia kuwa baba yangu amepinduliwa na mfalme wa sasa ni waziri mkuu yule niliyemtoboaga jicho lake. Nilishangaa sana na haukupita muda nikakamatwa na kuingizwa mahabusu. Waziri akaja na kunambia sasa umefika muda wake wa kilipiza kisasi. Nilimuomba sana msamaha lakini alikataa.akaamrisha askari wake anichukuwe na akaniuwe na kunitowa jicho moja la kulia.


Basi askari yule akanichukuwa mpaka mbali na kunambia “ nikifikiria wema alotufanyia baba yako siwezi kukuuwa lakini naomba uniridhie nikutoe jicho ili kumridhisha mfalme wa sasa na nitamwambia nimesha kuuwa”. Nilikubali nikamuomba niingie porini na kutafuta dawa ya kunifanya nipoteze fahamu. Dawa hii nilifundishwaga na binamu yangu. Yeye alikuwa akiitumia dawa hii anapokuwa na mawazo mengi hivyo hujipoteza fahamu kwa muda.


Nilitafuta dawa hivyo kwa muda na nikaipata nikayafikicha majani yake na yalipotowa mai nikayanywa na nikapoteza fahamu muda ulelule na sikujuwa kinacho endelea. Nakuja kuamka nikiwa na maumivu makali sana kichwani na jichoni nikiwa chongo asiye na jicho moja la kulia. Askari akanambia niondoke aneo lile na nisirudi tena nchi ile. Nilirudi kule kwenye utawala wa mjomba wangu.


Kufika kwamjomba nae alikuwa katika hali nzito ya kumtafuta mtoto wake. Alifurahi pindi aliponiona maana aliamini nitakuwa na taarifa kuhusu mtoto wake. Aliponambia ni mwezi sasa hajaonekana nilipatwa na hofu, hivyo nikamueleza mjomba kuhusu stori nzima. Usiku ulipoingia nilitoka na mjomba kwa siri na kuelekea kule kwenye ule mjumba wa ardhini. Basi tukaingia palele baada ya kuvunja mlango. Tulipofika kwenye jumba ile tukaingia na tukakuta kuna moshi pale ndani. Tulipopita moshi ule tukamkuta binamu yangu amelala chini akiwa amekauka kama amebanikwa nyama.


Kuona hali ile mjomba alilia sana na akanambia tutoke na tumuache palelpale. Tulipofika pale nje akanambia “nilijuwa tu nilipomuaona anakaana mwanamke yule nikajua kuwa atakufa tuu, yule mwanamke ni jini”. Basi akanambia nisimwambie yeyote habari ile. Niliishi na mjomba kwa muda ila alifariki na nikachukuwa madaraka yake.


Siku moja nilishangaa kuona ufalme wangu umezungukwa na askari wa ile nchi ya mjomba. Kumbe yule waziri aliyempindua baba amekuja kupindua na utawala wa mjomba wangu. Kwakuwa nchi yangu haijajiandaa kwa vita niliamua kukimbia ilikuepusha vifo vya watu. Niliondoka pale nikawa nalanda mpaka nikafika nchi hii ya baghdad nikanyoa nyusi zangu na nikakutana na wenzangu wawili hawa maka tukafika hapa. Hii ndio stori yangu. Zubeida kusikia maneno yale alifurahi sana kwa stori ile na kumwambia umeokoka. Akamfata chongo wa pili na kumwambia tuambia na wewe stoti yako. Naye akaanza kama ifuatavyo:-


HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME.
Kwanza utambuwe kuwa mimi nimekuwa chongo si kwa sababu ya ajali ama bahatimbaya kama iliyompata mwenzangu huyu. Mimi ni kwa sababu ya ujeuri wangu wa kutaka kujuwa mambo yasiyo nihusu. Hadithi yangu ni hii:-


Kama nilivyotangulia kusema mimi ni mtoto wa mfalme na ni wa kipekee katika uzawa na baba yangu akanichagulia jina la Agib. Baba yangu alinipa taaluma nyingi sana. Ila kwa upand wangu nilipenda kuwa mfanya biashara. Hivyo nilikuwa nikisafiri kwa kufanya biashara maeneo mengi ya dinia. Tulikuwa tukiuza vitu mabalimbali. Kwa ufupi nilikuwa nimejaaliwa kwa kuwa na nuru ya biashara. Nilikuwa nikiuza sana na kupata faida nzuri.


Siku moja tulikuwa tumetoka kibiashara kwa njia ya majini. Nahodha alikuwa mjuzi sana wa safari hizi na safari yetu ilikuwa nzuri sana. Tulifanya biahsra katika visiwa kadhaa na kuelekea upande wa kusini kutoka kisiwa tulichotoka. Upepo ulikuwa mzuri kwa muda wa siku nzima. Hali ilibadilika pale ilipofika asubuhi. Upepo ulikuwa mbaya sana na chombo kilikuwa ninakwenda uelekeo usiojulikana. Nahodha na wenzie walijitahidi kutuwa nanga lakini kamba ilikuwa fupi. Basi wakakiachia chombo kiende tu.


Ilipofika asubuhi nyingine tupepo ulitulia na tukaona mbele kuna mlima uliotanda kiza kinene sana. Nahodha alipoulizwa alisema hana ujuzi na eneo hilo lakini anachoweza kusema ni kuwa mlima uliopo mbele yetu ni mlaima wa sumaku hivyo misumari yote iliyopo kwenye chombo chetu itatoka na kuvutwa kwenye mlima. Hivyo nahodha akatutaka kila mmoja ajiandae na ajali hiyo.


Mambo yalikuwa hivyo hivyo baada ya muda kadhaa misukari ikaanza kung’oka na kwenda kunata kwenye mlima. Jabir tukaanza kung’ang’ania mbao. Kwa upande wangu mbao nilioipata ilikuwa ni madhubuti hivyo niliogelea naye kwa muda wa siku kadhaa. Mapaka siku ya 5 nikaona kuna kisiwa kidogo. Nikajitahidi nai kufika pale nikaona kuna mti wa mpera nikafika hini pale na kuanza kula mapera.


Nilikaa pale kwenye mti ule kwa muda mpaka nikapitiwa na usingizi. Nilipoamka nikaona kuna msafara mkubwa sana unakuja kuelekea pale nilipo. Nikapanda juu ya mpera ule na kujificha pale. Msafara ule ukaja mpaka pembeni kidogo ya mpera ule kwa futi 50 wakachimba chini na kufungua mlango pale chini na msafara wote ukaingia pale. Baada ya muda wa masaa kama matatu walitoka wote kasoro mtu mmoja tu ndiye aliyebaki mule ndani.


Walipoondoka nilisubiri kama masaa 2 nikafungua pale na kuingia ndani. Nilipofika nikamkuta kijana wa umri wa miaka 10 ivi. Nikamsalimu na kumuuliza kilichomsibu hata wenzake wakamuacha mulendani. Akaanza kunieleza stori yake kama ifuatavyo;-


HADITI YA MWENYE KUTABIRIWA MTOTO WA TAJIRI
Kwanza tambua ewe ndugu yangu kuwa mimi ni mtoto wa tajiri mkubwa sana katika nchi yetu hii. Kwa sasa nina umri w miaka 15 na baba yangu aliponizaa alinichagulia jina la Agib. Nimewekwa hapa kwenye handaki si kama nimetelekezwa hapana. Hii ni njia pekee iliyoonekana kuwa nitakuwa salama. Bla shaka unataka kujuwa hasa nini kilinitokea, mambo yalikuwa hivi;-


Baba yangu kabla hajanizaa kwa muda wa mwaka mmoja alipata ndoto ya ajabu sana. Aliwatafuta watu maarufu na wenye elimu ya kutambuwa maana za ndoto na wakamwambia kuwa mke wake yaani mama yangu atapata ujauzito wa mtoto wa kiume. Na mtoto huyo ataishi kwa furaha na amani kwa muda wa miaka 15. na kama akifika miaka 15 bila ya kitu chochote kumpata Jabir mwana wa mfalme katika mlima wa sumaku, mtoto huy ataishi salama mpaka uzeeni. Vinginevyo kama akifika miaka 15 na mwana wa mfalme Jabir akipatwa na ajali katika mlima wa sumaku basi uhesabu siku 40 tu za umri wa mtto wako zitakazokuwa zimebaki toka utakapopata hiz habari.


Hivyo mambo yakawa kama hivyo mimi nikazaliwa na mpaka sasa nina miak 15 sijawahi kuumwa wala kupata majonzi makubwa. Lakini ni siku 5 zilizopita baba alipata habari kuwa Mlima wa sumaku umesababisha ajali ya watu na huenda huyo Jabir mwana wa malme akawemo humo. Hivyo baba akaamuwa kunificha huku ili nisiweze kukutana na jabir. Kwa sasa nina matumaini kidogo lakini huwezijua hatima ya mwanadamu. Hii ndio stori yangu ewe ndugu yangu.


Basi niliposikia stori ya kijana yule nilipatwa na majnzi kuona kumbe ni mimi nitakayemuuwa. Sikuamini mawazo haya na kikaapa kuakaa pale ili nimlinde huenda akawa ni mtu mwingine atakayekuja kumuuwa. Basi niliaua kumdanganya jina langu na kumwambia naitwa Habir ni mvuvi niliyepatwa na ajali majini. Nikampatia mapera niliyochuma kule nje na aliyependa sana. Basi nikamwambia nitaishi na wewe hapa na nitakulinda na huyo anayetarajiwa Jabir kama akija.


Kijana alikubali na alifurahi pia, kwani alitaka hata apate mtu wa kuweza kuzungumza naye pale ndani, maana wazazi wake walimuahidi kuwa watakuja siku ya 40. basi mimi nikawa ndiye mfanyaji kazi pale ndani, napika na kufanya mambo kmengine kama kutandika kitanda na kufagia. Kwakweli tuliishi kwa furaha sana wawili sisi pale ndani. Nilikuwa nikijaribu kumfurahisha kila wakati kwa namna yoyote ile.


Basi mabo yakawa kama hivyo, tuliishi kwa upendo na furaha kubwa kwa muda wa siku 39 zote pale handakini. Siku ya 40 hatimaye ikafika na kila mmoja katika sisi alifikiri mambo yale yamekwisha hivyo kijana yupo salama. Siku hii kijana alivaa nguo zake nzuri na niliandaa chakula kizuri sana. Ilifika muda wa wa kukaribia mchana kijana akaend kualala. Basi mimi nikaendelea kuandaa chakula na vinywaji. Lakini nilipotaka kumenya matunda sikukiona kisu.


Nikaenda kukitafuta kisu nimenye matunda bila ya mafanikio. Ghafla nikakumbuka kuwa kijana alikuwa akimenyea embe jana kitandani kwake. Basi nikaelekea kwenda kukichukua kisu. Nikakikuta amekitundika kwenye mjiti wa kitanda kunapochomekewa pazia la kitanda. Basi kwa utaratibu nikapanda pale kwenye kitanda bila ya kumuamsha na nikawa nakichomoa. Kwakuwa mikono yangu ilikuwa ikiteleza kisu kiliniponyoka na kufikia kwenye kifua cha kijana na kuumaliza uhai wake kupitia moyo.


Nilipatwa na woga sana, sikiamini9 kama mimi niliyetaka kumlinda ndiye nimemuua. Nililia sana, ila ghafla nikakumbuka leo wazazi wake watakuja hivyo nikatoka pale ndani kwa haraka. Nilipomaliza tu kutoka nje na kuukaribia mpera nikaona kundila watu linakuja. Basi kwa woga wangu nikaificha pale kwenye mpera.


Wale watu wakaingia ndani mule na kwa muda usiopungua masaa 3 wakatoka na mwili wa kijana huku wengine wanalia sana. Wakauzika mwili ule pale pembeni na kisha wakaondoka. Nilikaa pale kwa muda mrefu hata ilipokaribia jioni nikatoka pale na kutembea tembea katika eneo lile. Nikakuta kanhia kanakoelekea milimani nikakafuata. Huko nikakutana na watu 10 wote ni machongo wa jicho la kulia.


Watu wale nikawaelezea kuwa mimi nimepata ajali baharini na sina ninaemjua eneo hili hivyo nikawaomba wanihifadhi. Ijapokuwa kati yao baadhi walikuwa wakikataa lakini mkubwa wao akazungumza “tutakukubalia kukaa nasi ila kwa sharti moja naloni KUTOKUULIZA CHOCHOTE KATIKA MAMBO YATAKAYOFANYIKA USIKU”. kuna mwengine akaongezea kwa kusema “na sharti hili ni kwa ajili ya usalama wako tu” basi nikatoa ishara ya kukubaliana na sharti lile.


Kwahakika niliishi bila ya shaka nyumbani kwao wale machongo. Lakini jambo moja tu lilikuwa likinisumbua ni kuwa kila ifikapo usiku wanachukuwa mijeledi na kuanza kujitandika mgongoni viboko 100. nilikaa hivi bila ya kuuliza kwa muda wa siku kadhaa. Siku moja nikaamuwa kuwauliza na lolote litakalotokea na litokee ila lazima nijuwe ni kwa nini wanajitandika mikwaju ile na ni kwa nini wote ni machongo wa jicho la kulia?.


Basi mambo yakawa kama hivi, siku ile mchana nikawauliza maswali yale mawili. Basi walishangaa sana kuona ninakiuka masharti ya kuishi ndani pale. Mkubwa wao akanieleza “kijana sharti hili tuliweka kwa ajili ya usalama wako, lakini sasa inaonekana hata haujali nini kitakupata”. kaka mimi naomba kupata majibu ya maswali haya na sijali kwa lolote litakalonipata. Akanijibu “sisi hatutakueleza chochote katika hayo ila utajionea mwenyewe, kama ukotayari tutafanya maandalizi kesho” nikamjibu kuwa nipo tayari.


Basi siku ile ilofata asubuhi wakamchinja kondoo nakuniambia “tutakushonea kwenye ngozi ya kondoo huyu na tutakupa kisu. Tuatkuweka juu ya mlima na hapo atakuja roki (ndege) atakubeba akidhani ni kondoo. Pindi akikutuwa tumia kisu na uchane ngozi yeye atakimbia. Utakapotoka upande wa mashariki ya mlima kwa chini utaona njia ndogo. Ifate njia hiyo na utakuba nymba. Humo usimuulize mtu yeyote juu ya mambo haya. Ukifanikiwa kurudi hapa ndani ya sikua 100 na ukawa haukupata majibu ya maswali yako nitakujibu mwenyewe”.


SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI.
Basi mambo yaka wa hivyohivyo, siku ile wakaniweka kwenye ngozi ya kondoo na kubebwa na roki. Alikwenda kunituwa juu ya mlima na nikatumia kisu na kutoka yule ndege akakimbia. Nikafata ile njia niloambiwa mpaka nikakuta nyumba kubwa sana. Kwa hakika nyumba ilikuwa ni nzuri sana na ni kubwa. Ilikuwa ina vyumba zaidi ya 100. ilikuwa ina vitu vingi vya kuvutia na mabostani ya matunda na miti.


Nyumba hii ilikuwa imetulia sana yaani utadahani haina hata mtu mmoja japo utashangazwa kwa usafi wa nyumba hii. Nilianza kuhesabu vymba mpaka nikafika chumba cha 35, na humo nikasikia sauti za wanawake. Nilibisha hodi na kukaribishwa kwa furaha. Nilipewa chakula na malazi, vinywaji na furaha nyingine.


Nilikaa pale kwa muda wa siku 5 nikiwa ninabadilishiwa furaha mpa ya mambo mapya kila siku. Huenda hata ningeishi siku 1000 ningepata mabo mapya kila siku. Kwa hakika nyumba hii ilikuwa na kila kitu nilichokisikia na kila uzuri. Niliendelea kukaa pale hata ilipofika mwezi 3 kambla ya kumalizika kwa mwaka kwa siku 10.


Siku ile wale wanawake wakaniita na mkubwa wao akaanza kuongea “mgeni wetu, tunapenda sana kuishi na wewe hapa kuwa muda zaidi lakini hatunabudi ya kutengana kwa muda wa sili 100. sisi ni watoto wa wafalme na huwa kila mwisho wa mwaka tunarudi makwetu kwa ajili ya mabo ya kifamilia. Hivyo hatunabudi kutengana nawe ila tutakuacha hapa. Tunakuachia funguo hizi za vyumba 100 humo utafutahia vitu ambavyo hujapata kuviona kwa muda wote uloishi hapa. Ila vyumba vyote fungua isipokuwa cha 100. kama tutakutana baada ya siki hizo tutafurahi sana na tusipokutana usisahau kutuombea dua.”


Kwa majonzi niliagana nao sikuile na wakaondoka. Basi nikaanza kufurahia mambo mazuri yaliyomo pale ndani. Nikawa kwa kialsiku Snafunguwa chumba kimoja. Ikawa kila chumba nikuta mambo mazuri ambayo chumba nilichofungua jana hakina. Kwahakika nilifurahia sana harufu nzuri ya mawaidi mule ndani. Sauti nzuri za kupendeza za ndege, chemchem za maji na asali iliyohifadhiwa. Vyakula vya kila namna na vikalio vya kuvutia.


Nilifanya hivyo mapaka pale nilipomaliza vyote vyumba 99 kwa siku 99 na kubakia chumba kimoja na siki moja mpaka kurudi wale wenyeji wangu. Sikuile ya 100 ilipofika nikawa sina hamu ya kurudia vyumba vya nyuma hivyo nikataka kufungua kile cha 100. nikaenda kwenye mlango na kuanza kupiga mahesabu ya kufungua. Nilianza kuoiga ramli ya vigole kwa kufumba macho lakni matokea yakawa nisifungue, basi nikaamua niondoke pale mlangoni.


Nilizunguruka mule ndani na nikajikuta narudi tena chumba cha 100. mara hii nilikuja na jani nikawa napiga ramli ya majani lakini matokeo yaka wa nisifungue. Dukuduku lilianza kuniumiza kwa nini chumba cha 100. mna nini hasa humu mpaka nisifungue. Basi nikaichukua ile funguo na kufungua kidogo ili nichingulie. Nilipofungua ghafla ilikuja harufu nzuri ya ajabu na hapohapo nikapoteza fahamu.


Nilipokuja kuzindukka nikafungua ili nijue kuna nini na ni wapi harupu ile ya kuvutia ilipotokea. Basi nilipofungua tu nikajikuta nipo nje, kumbe kile hakikuwa ni chumbaila ni mlango wa kutokea kwenye bostani. Nilipofika mule nikaona kuna ndege wanaoimba nyinyo nzuri, matunda ambayo sijayaona na mauwa yanayotoa harufu njema ya kuvutia. Maji ya chemchem yenye rangi ya dhahabu na ni ya moto. Halikadhalika vivuli vyenye mumbo


Kwa hakika katika bostani lile kulikuwa na mabo mengi na ya kuvutia sana. Cha ajabu zaidi niliona kuna farasi mwenye mabawa na mkia mrefu wa kuvutia wenye mashapupo yanayofanana na miba ya nungunungu. Nilitamani sana kumpanda farasi yule. Nilimsogelea na kutafuta fimbo ya kumuendeshea na nikaiona. Polepoe nikampanda na kuanza kumuendesa mrembo farasi.


Farasi yule ghafla akaanza kupaa hata kabla sijakua namna ya kumpaisha, alipofika umbali kadhaa akaanza kunifiga na mashaputo ya mkia wake ulio mrefu. Mashaputo yale yakanipata kwenye jicho langu la kulia na kunitoboa. Nilianguka chini ghafla na kupoteza fahamu. Nilipokuja kushitua nikajikuta nipo karibu na mlima na lile jumba sikuliona tena na hata ile njia sikuiona tena.


Basi nikarudi kwa wale wenzangu machongo tukawa tupo chongo11. wale wakanambia siwezi tena kukaa na wao maana wamesha enea. Hivyo yule mkubwa wao akanimalizia majibua ya maswali yangu kuwa sababu ya wao kujitandika na mikwaju ni adhabu ya kuvunja amri ya kutoufungua mlango wa 100. hivyo wakaniambia niende baghadi huko nitakutana nae ali anipangie adhabu yangu.


Baada ya hapo nikanyoa nyusi zangu na nywele zangu na kuelekea baghdad na nilipofika hapa nikakutana na wenzangu hawa watatu na usiku ulipotufikia tuakaamua kuomba hifadha hapa kwenu. Hivyo hii ndio stori yangu ewe dada Zubeida.


Zubeida alipomaliza kusikiliza stori ya chongo huyu akamuelekea chongowa tatu na kumwambia aeleze stori yake bila ya kuficha kitu na vinginevyo atakufa. Chongo wa tatu akaanza kuelezea kuwa na yeye ni mtotowa mfalme na amepata chongo si kwa sababu ya ubishi wake bali ni qadar tu na hivi ndibyo mambo yalivyokuwa;-


HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME
Mimi ni mtoto wa mfalme kama nilivyotangulia kusema na ni mtoto wa kipekee kwa baba na mama. Nilipewa taaluma nyingi na wazazi wangu na nilifahamu vizuri. Nilifundishwa sayansi, maarifa ya mazingira, simulizi na biashara. Kwa upande wangu nilipenda sana uandishi na nilikuwa na muandiko mzuri sana hata niliwashinda waandishi wote nilowahi kukutana nao. Uzuri wa muandiko wangu ulifika mbali sana hata nikawa ninaa ndika barua zote za mfalme kwenye nchi za majirani.


Ilitokea sikumoja nikaandika barua iliyotakiwa kuenda nchi za hindi kwa mfalme wa wahindi. Niliandika barua ile kwa ufndi wa hali ya juu na ikatumwa kwa mfalme wa hindi. Taarifa zikatujia baada ya miezi kadhaa kuwa mfalme wa wahidi amestaajabishwa sana na uzuri wa mwandiko wa barua ile hivyo akataka amuone mwandishi huyo na alitowa zawadi nyingi kwa mfalme wa nchi yetu yaani baba yangu ili aniruhusu niende uhindini akanione.


Baba alifurahihwa sana n barua ile na mimi pia nilifurahi japo nilisita kuenda hindi. Kwa zawadi alizopokea baba aliniomba niende na kuniambia huenda nikajifunza mambo mengi ambayo pale nchini kwetu hakuna. Baba alichagua walinzi wazur kwa ajili ya kuulinda msafara wetu kwani safari ilikuwa ni ndefu na yenye ugumu pia.


Basi ilibidi nikubaliane na mawazo ya baba ya kwenda nchi ya wahindi chini ya ombila mfalme wa watu nwa hindi. Baada ya siku 10 safari ilianza kuelekea uhindini. Safari ilikuwa nchema na yenye amani. Tuliweza kupita kwenye majangwa na misitu. Tulivuka mito na mabwawa ya kuvutia na kupendeza. Nilifurahishwa na safari na kujiahidi mwenyewe kuwa kwa hakika nitajifunza mengi huku niendko.


Tulitembea bila ya dharuba kwa siku 15 na tulilala siku hiyo katika eneo la jangwa lenye mlima wa michana na vichuguu vya hap na pale. Bila ya kujua lolte kumbe kulikuwa na wavamizi wanatuchunguza. Asubuhi ya siku ilofata tuliondoka pale na tukapita kwenye ponde lililochimbika. Wale wavamizi walikaa juu ya bonde na kutuacha sisis tunapita chini yake. Ghafla wakaanza kutushambulia na wengi katika sisi wakapoteza maisha. Kila mtu akaanza kukimbia upande wake kuokoa maisha yake.


Kwa upande wangu sikuona hata askari aliyekuwa akinikinga. Basi nikavua yale mavazi ya watoto wa wafalme na kuwatupia wavamizi na nikaanza kukimbia. Hii ilikuwa ni salama yangu kwani mavazi yale yana thamani kubwa hivyo wasingethubutu kuniachia. Nilikimbia bila ya kujua ninakoelekea mpaka niliposilkia sauti ya jogoo akiwika. Kwa mbali nikasikia sauti ya pungu hapo nikajuwa kumbe ilikuwa ni saa saba sasa.


Nilielekea kule niliposikia sauti zile na kukutana na mzee mmoja na kumuelezea tukio lote. Mzee huyu akakybali kunipa msaada wa kuishi pale kkwake. Nikaishi pale kwa muda wa siku tatu kwa yule mzee nikila na kuoga bila ya tatizo lolote. Siku ya nne yule mzee akaniuliza. “mwanangu, unaishi hapa ila inabidi ujifundishe kuishi mwenyewe bila ya kunitegemea. Vip kwani mwanangu una ujuzi gani wewe?”. nikamjibu “mimi nimeishi maisha ya kifalme kama nilivyokwambia baba yangu ni mfalme hivyo maisha niloishi ni ya kisomi. Taaluma nilonayo ni masimulizi na uandishi”.


Yule mzee aliposikia maneno yangu akaguna kidogo kisha akasema “mwanangu, kwa ujuzi ulonao hapa ni vigumu kuweza kujitgemea. Hivyo nakushauri uanze biashara ya kukata kuni. Nitakuandalia zana na nitakufundisha pia. Kwa hakika ni kazi njema na ni ya rahisi katika eneo hili”. Basi siku ilofata yule mzee akanikabidhi shoka na panga pamoja na kata ya kubebea mizigo ya kuni.


Basi mzee alinichukuwa kuelekea msituni ambapo akanifundisha kazi ile na unielekeza mambo yahusuyo. Tulikata kuni siku ile na tukarudi na mizigo kila mtu na wa kwake. Mzee akanipeleka sokoni na kunelekeza matajiri wa kununua kuni zile. Siku ilofata nikaenda peke yangu, kwa kweli mwanzo kazi niliiona ngumu sana ila baada ya siku kadhaa nikaanza kuzoea.


Nilianza kuishi bila a kumtegemea mzee wangu yule, kwa hakika alinizoea sana na alinifanya kama mwanae. Alikuwa nabinti yake aliye mdogo alikuwa kila siku akiniambia pindi akikuwa ataniozesha. Ingawa sikua na matumaini hayo lakini nilikubwa kwa kuataka kumridhisha mzee yule. Hivyo nikawa ninatoka asubuhi kuelekea kazina na mida ya mchana ninarudi kwa ajili ya kutegea soko la mchana na wale anaotaka kupika usiku.


Sasa nimesha zoea kazi hata mzee aliweza kuniachia familia yake niweze kihudumia pindi alipopata safari za dharura. Ni mieze miwili na siku nane sasa toka nikutane na mzee huyu. Nilimuheshimu sana na alinipenda pia. Kwakweli heshima inapelekea kupendwa na watu. Mambo yalikuwa kama hivyo, ila siku moja kila kitu kiliharibika. Kwa hakika sikuweza kuisahau siku hii hata mara moja.


Ilitokea siku moja nilikwenda kukatakuni asubuhi sana na mapema. Siku hii nilikwenda mbali sana tofauti na sikuzote. Nilipokuwa ninachanja kuni ghafla nikasikia sauti kama vile shoka imepiga chini ambapo kuna shimo. Nikaacha kuchanja kuni na kuanza kufukua pale chini na nilishangaa kuona kuna mfunikowa zege. Pale nikaanza kuchimba ule mfunika hata nikaufungua na kukuta kuna ngazi ya kushuka chini. Kwa umakini nikaikamata ngazi ile na kuanzakushuka nayo kule chini na kukuta kuna jumba moja kubwa sana.


Nilistaajabu kuona jumba kule chini. Kwa udadisi zaidi nikataka kujua kuna nini hasa. Ikaelekea mlango mkuu wa jumba lile na kugonga mlango na kufunguliwa na wafanyakazi wa kike. Wakanipeleka mpaka kwa mkubwa wao. Kumbe jumba lile lina wananwake watupu na mkubwa wao ni mwananoke ambaye ni mtoto wa mfalme. Nilipomuona tu nilistaajabu kwa ururi ambao ameumbiwa. Kwa hakika ni mzuri na anaonekana katika mavazi ya heshima zaidi.


Nikamsalimia kwa upole na kurudisha salamu. Baada ya salamu nikajitambulisha kwa jna la Hamid mchanja kuni wa kijiji, binti alitabasamu na kuniacha mdomo wazi kwa mshangao.nilimuuliza kipi kimemsibu na yeye ni nani hasa. Akaanza kunielezea habari yake kama ifuatavyo;-


HADITHI YA BINTI MWENYEKUFICHWA, MTOTO WA MFALME.
Juwa ewe mwenye kuja kwa jina la Habili kwa cheo cha mchanja kuni kuwa mimi ni mtoto wa mfalme niliyetambulika kwa uzuri na hta mawaziri na watoto wa wafalme wakawa wanagombana kwa kutaka kunipata kuwa mke wao. Ugovi huu ulikuwa mkali hata ukaingiliwa na viumbe visivyo onekana navyo vikataka kunioa nao ni maini waliombali na rehema za Mwenyezi mungu.


Nyumbani kwetu kulikuwana kisima kilichoaminika kuwa ni cha muda mrefu kisichopungua umri wa miaka 150. katika kisima hiki kijana wa kijini alichikuwa madaraka ya kutawala majini waliopo kwenye kisima kile. Siku ile nilikwenda kuchota maji kisimani pale nikiwa kichwa changu kipo wazi kinyume na maamrisho ya dini yetu. Bila ya kutambua unywele wangu mmoja uliangukia kwenyekisima kile na kumganda kiongozi mpya a majini alipokuwa akipewa majukumu.


Nilirudi nikiwa na mabadiliko katika kichwa changu hata ndoo ya maji niliiona n nzito sana kuibeba hivyo nikatumia mikono yangu kubeba maji yale. Siku ile sikupata usingizi kwa maumivu ya kichwa na nilipopata usingizi nilshituka kwa ndoto za kutisha nilizokuwa ninazipata. Sikujuwa chanzo cha matatizo haya yote. Ilipofika asubuhi nilimueleza baba yangu ju ya maumivu ya kichwa changu. Baba alimwita daktari wetu na kuanza kunitibia. Kwa muda wa siku 5 sikupata nafuu zaidi ya maradhi yaliyokuwa yakinizidia.


Kwa muda wa miezi waganga na madaktari wote walishindwa kutibu ugonjwa wangu. Ilifikia hali kuwa mbaya hata nikawa sinafahamu juu ya niayofanya, unaweza kusema nilikuwa mkichaa ambaye akili zinaingia na kutoka. Hali hii ilimpa baba yangu wakati mgumu hata akafikiri ni maradhi yaliyosababishwa na wale wachumba wliokuwa wakinigombania. Habari za ugonjwa wangu zilienea nchi nzima na kila mtaalamu wa tiba alikuja kujaribu bahati yake kwani donge nono liliahidiwa kwa atakayenitibu.


Miezi sita ilifika na habari za ugonjwa wangu zikaenea nchi za majirani. Baba alifikia hatua akatangaza kwa yeyote aatakayenitibu ataniozesha nae. Jambo hili lilisababisha hata wataalamu wa ta kutoka nchi za jirani wa lengo la kunioa pindi wakifanikiwa kunitibu. Bila ya mafanikio yeyote juu ya ugonjwa wangu ijapokuwa wapo walofaniukiwa kunipa nafuu lakini haichukui muda kabla ya ugonjwa kunizidia.


Siku niliota ndoto ya kushangaza. Ndoto hii nilipomwambia baba alijaribu kuwauliza wataalamu wenye kujuwa tafsiri za ndoto. Basi akaja mtaalamu na akaniambia nimueleze ndoto ile bila hata ya kuacha hata sehemu ndogo. Basi nilikaa kimya kwa muda kisha nikakusanya mawazo yangu na kuanza kumuelezea ndoto yangu kama ifuatavyo;-


NDOTO YA MGONJWA BINTI WA MFALME.
Nilipokuwa nimelala nilioa kana kwamba nipo katikati ya kundi kubwa la watu na wote ni wanume. Wote walikuwa wanagombania kuushika mkono wangu. Ila walishindwa kuupata kwa sababu nilipokuwa nipo nilizungukiwa na miba hivyo walishindwa kupita. Watu hawa walionekan kuminyana na miba ile bila mafanikio hata wakaanza kugombana na kulaumiana juu ya nani ameweka miba ile.


Wakiwa katika hali hiyo ghafla upepo mkubwa ulivuma ukiambatana na vumbi kubwa. Miti iliinama kwa upepo ule na wale watu wote wakatulia kwanza. Katika hali hiyo alitokea kijana mmoja mzuri aliyevaa mavazi meupe yenye kuvyovywa kwenye dahabu nyekundwu. Kwa hakika alinivutia sana. Kisha akawaambia wale watu kuwa wasigombane yeye ndiye aliyeweka ile miba, na hivyo hakuna hata mmoja ataweza kuivuka miba ile ila mpaka aitoe.


Mmoja kati ya wale watu akamuuliza ni kwa sababu gani ameamua kuweka miba ile. Akawajibu kuwa “kwa muda mrefu pacha wangu amekuwa akiulinda mkono wa huyu binti dhidi ya wabaya na mabaya. Lakini si muda mrefu amepoteza maisha kwa sababu ya huyu binti. Wale watu wakaanza kupiga makelele na kumwambia kuwa yeye ni muongo. Vipi itawezekana huyu binti asiyejuwa hata kushika silaha akamuuwa pacha wako. Kwakweli hatujasikia jambo kama hili.


Akawajibu kuwa huyu binti siku moja alipokuwa anachota maji kisimani sehemu ya mwili wake ilidondokea kisimani na kumkuta pacha wangu akiwa katika hali ya kupewa majikumu hivyo muda ule hakuwa na nguvu yoyote ya kujikinga. Hivyo aliungua mwili wake kwa sababu hiyo akapoteza maisha baada ya siku 9 toka tukio lile. Hivyo nikaweka miba hii na kuapa kuwa hakuna yeyote atakayeipita miba hii na kukuta mkono wa binti huyu muuaji wa pacha wangu.


Mtu mwingine kati ya wale watu akauliza “vipi sasa miba hii utaitowa lini, au ni lini utaweza kuushika mkono wake na kumtoa kizuizini”. akajibu kuwa mpaka sasa huyu binti alikuwa kwenye adhabu ya kumuua pacha wangu lakini kwa sasa adhabu imekwisha hivyo nitamtowa kwenye kizuizi hiki mbele ya macho yenu. Basi pale pale akazungumza maneno fulani kisha miba yote ikaondoka. Nilipokuwa nikitoka yule kijana akanishika mkono na kunitowa pale. Ila kabla ya kuondoka eneo lile ghafla akachomwa na mkuki na kufariki palepale.


Jambo hili liliwashangaza wale watu wengine na wakaanza kujiuliza nani amemuuwa. Mtu mmoja mwenye sura mbaya akatokea akiwa amepanda punda mweusi. Akazungumza kumwambia yul kijana “nilikuwa nakusubiri tu umtoe ili nimchukue mimi, wewe ni kijana mdogo lakini ulinishinda wa miba yako hii kwa hakika nilishindwa kupita ila sasa hakina wa kunizuia” basi palepale akanichukuwa na kunipeleka chini ya ardhi iliyopo nchi nisiyoijua. Ghafla nikasikia maumivu kwenye mgongo wangu na nikashituka kuoka usingizini. Hii ndiyo ndoto niliyoiota ewe mjuzi na muelewa wa hadithi za usiku.


Katika kuitafasiri ndoto ile akasema kuwa “umekuwa ukiposwa na watu wengi lakini hakuna alokubaliwa mpaka sasa, hii ni kutokana na jini aliyekuwa amekfunga usiolewe akisubiri apewe madaraka kwenye utawala wao ili akuchukuwe na akufanye mke wake. Jini huyu alikuwekea ulinzi mkubwa dhidi ya maradhi na wachawi katu usingeweza kudhuriwa hata. Alikuwekea kinga iliyofanana na kunga yake. Bila shaka ulipokwenda kuchota maji sehemu ya mwili wako iliyomdondokea ni nywele zako. Na kwa kuwa alikuwa akipokea amri hakuweza kudhibiti usito w nywele yako iliyojaa nguvu iliyotokana na kinga zake. Hivyo alipatwa na matatizo kama ndoto inavyo elezwa.


Utawala huu wa majini upo chini ya kisima hicho ulichokwenda kuchotea maji. Majini hawa walikuwa mapacha hivyo moacha wake kama ndoto zinavyoonesha kwa hasira na majonzi akakupa haya maradhi kama adhabu. Na bila shaka atakuja mwenyewe kukutibu kama ndoto inavyosema. Halikadalika pacha huyu unamfahamu na ulishawahi kukutana nae na anakupenda pia hivyo hataweza kukuua.


Ila pindi atakapo kutibu tukio kubwa litampata litakalopelekea mauti yake na kwa upande wako pia hautakuwa salama kama ulivyoona kwenye ndoto. Alivyomaliza kusema hayo akamwambia baba kuwa hii ni tafasiri ya ndoto ya binti yako ewe mtukufu mafalme. Basi baba aliingiwa na majonzi kwa tafasiri ile ila hakuwa na jinsi. Kwa hakika nilikumbuka kuwa nilipokuwa mdogo sura ile niloiona kwenye ndoto niliiona. Niliona mtoto anazunguruka kwenye kisima na nili[omfuata akasema amepotea.


Basi siku ya ilofuata asubuhi akaja mganga mmoja na akasema anaweza kunitibu, lakini akataka mfalme aweke ahadi juu ya kumuozesha pindi atakaponitibu. Baba alikubali, basi nilipomuona tu nilimjuwa kuwa ni yule nilomuona kwenye ndoto. Kwa hakika alikuwa ni kijana mtanashati na ni mzuri pia, nilikubaliana na wazo la baba la kuniozesha kama ataitibu. Ila sikuweza kumueleza baba kuwa huyu mdiye yule nilomuona wenye ndoto kwa kuhofia kuvunja ahadi ya kuniozesha kuokana na tafsiri ya ile ndoto.


Basi ilichukua nywele kumbe ni ile nywele yangu na kuichoma na kuniambia nijifunike shuka ili mosho wote wa ile nywele unipate mimi. Basi haukupita muda nilipiga ukelele mkali sana hata baba alishangaa, kisima kiliporomoka madongo na maji yalijaa kwenye kisima, kuku walitawanyuka na punda wakawa wanapiga kelele ovyoovyo. Nilipoteza fahamu na nisijue kilichofata baada ya hapo. Nilipokuja kuzinduka mikajikuta nimepona kabisa. Basi ahadi ikaendelea na nikaolewa na yule kijana.


Tuliishi pale nyumbani kwa raha kwa muda wa siku tatu. Siku ya nne asubuhi nyoka mkubwa alitoka kisimani mchana na watu walimshuhudia a kuja ndani akamuua mume wangu na kunimeza mimi. Sikujua nini kiliendelea kuhusu mwili wa mume wangu au nini kiliendelea baada ya pale. Nilikujakushituka siku tatu baadae na kujikuta nipo humu ndani. Huyu jini ameniweka humu na amenifanya mkewe na anakuja kila baada ya siku 40. ila nikiwa na shida nae au nikipata matatizi huwa nabonyeza hii pete ya mkufu na hapohapo atakuja. Hii ndio stori yangu ewe Habil makata kuni.


Basi niliposikia habari hii nilistajabu sana na kuona kumbe kuna watu wamepta makubwa kuliko hata mimi. Basi na mimi nikamueleza stori yangu hata nikafika pale. Basi tulikunywa na kufurahia pae ndani. Nilikunywa pombe na nilipokuwa nimelewa nikaivuta ile pete ya mkufu na kuanguka chin. Yule binti alipiga kelele na kusema umeniua na maisha yako yapo hatarini pia. Toka nje na ukimbie.


Basi muda uleule pale ndani pakawa na kiza kinene nikajitahidi kutoka nje na kiakumbuka kuwa nimesahau kiatu kimoja ndani. Sikujuwa kilichoendelea huko ndani ila nilipofika nyumbani niliishia kitandani. Haikupita muda ilifika mchana na akaja mtu mmoja kutaka kuni. Nilipotka moyo wangu ulitetemeka kwani sikupata kumjua mtu yule akaniuliza “asubuhi ya leo ulikuwa wapi” nikamjibu nilikuwa hapahapa leo sijatoka. Akanionesha kiatu changu akasema “hiki sio chakwako?” nilionekana kubabaika basi akapiga guu lake chini na hapo hapo upepo mkali ukanibeba.


Alinituwa ufukweni mbele ya yule binti na kumuuliza kama ananijua. Yule binti akakana na kusema kuwa hanijui na mimi pia nikakana kusema kuwa namjua. Basi jini yule akamchinja ule mwanamke na kunuiambia “sasa ni zamu yako”. nikaanza uomba msamaha lakini hakuonekana ni mwenye kusamehe. Nika mwambi “naomba unihurumie kama khalid alivyomuhurumia Jlid”. basi jini akauliza “kwani jalid alimfanya ni ni Khalid”. nikaanza kumsimulia kisa cha Khalid na Jalid kwa upole kma ifuatavyo;-


HADITHI YA KHALIDI MWENYE KUNEEMESHWA NA JALID.
Khalid na jalidi waliishi eneo moja huko kijijii kwao. Walikuwa na chuki zao za muda mrefu na hivyo ilipelekea uadui kati yao.Khalidi hakupendezwa na ile hali ya kuwa na uadui na watu. Khalidi alifahamika kwa ucha mungu pale kijijini na ukarimu alio nao. Wat walikuwa wakimpenda sana khalidina kumchukia Jalidi kwa tabia zake mbaya. Ijapokuwa Khalid alikuwa akimtendea wema Jalidi lakini hili halikumfanya jalidi kupunguza chuku zake kwa Khalidi.


Hapo zamani khalidi na Jalidi walikuwa ni marafiki wapenzi sana wa tangu utotoni. Ijapokuwa tabia ya Jalidi haikuwa njema sana hata wazazi wa Khalidi wakawa wanamkataza kucheza na jalidi. Mambo hayakuwa hivyo urafiki wao haukuweza kuvunjika kwa maneno haya. Marafiki hawa wawili walippenda sana kuwinda kwa kutumia manati, mikuki na mishali. Walifahamika kwa uhodari wao pale kijijini walipokuwa wanaishi.


Sikumoja walipokuwa wanawinda karibu na mto ghafla nyoka aina ya chatu alimkamata Jalidi na kuanza kumbingirisha ili amuingize kwenye maji. Jalidi alipiga kelele na hiku akijikwamua kwenye mbavu za joka hili lakini juhudi zake zilikwama. Khalidi alikuja akiwa na mkuki wake na kuanza kumsaidia rafiki yake. Khalidi hakuwa na nguvu sana ukilinganisha na Jalidi lakini alikuwa akitumia akili ya ke hasa.


Khalidi alikumbuka kauli ya babu yake alipomwambiaga kuwa ukipambana na chatu lenga macho yake, ukiyakosa kamata mkia wake na ukiukosa mtie jeraha sehemu ypyote lakini bora umjetuhi kwa kuuvunja mgongo wake. Mawazo haya yakapelekea mapambano makali kati ya Khalidi na nyoka yule ili kumsaidia Khalidi. Wakati huo Jalidi alikuwa ameshaanzwa kuviringishwa na lijoka hilo tayari kuanza kuvunja mbavu laini za Jalidi.


Kwa upande wa Khalidi alikitafuta kichwa kwa hali na mali lakini hakukiona akakumbuka kauli ya baba yake alipomwambiaga “chatu mara nyingi anapokamata huficha kichwa chake ili kisijedhuriwa wakati wa mapambano”. basi akahamia kwenye mkia lakini mkia wa chatu ulikuwa ni vigumu kuumiliki alipoukamata alirushwa na mkia ule na alipata maumivu makali. Katika hali hiyo akakumbuka kuwa aliwahi kusikia kuwa chatu huulinda mkia wake kwa hali na mali.


Katika hali hiyo Khalidi akahamia kwenye mgongo na kuamza kumjerui nyoka yule, juhudi za Khalidi hazikutoka patupu alifanikiwa kumtia majeraha kadha na hapo chtu akaanza kupoteza nguvu. Wakati anataka kuvunj mgongo wa chatu mkuki ulidunda pale ngonjo ni na ukamtoka mkononi. Mkuki ule ulikwenda mchoma Jalidi kwenye jicho na kumtoboa. Kwa pigo lile chatu alipata maumivu na kukimbia mbalia sana na kumuacha Jalidi akiugumia maumivu.


Kuja kupata ahueni Jalidi alijikuta akiwa na chongo la upande wa kulia. Hali hii ilipelekea kutengeneza uadui na kuvunja urafiki. Jalidi aliamini Khalidi alifanya kususi kwani angeweza kumnusuru bila hata kumjeruhi lakini uzembe wake wa kutokukamata vizuri mkuki umepelekea maumivu kwa jalidi. Hivyo uadui huu ukajengeka kwenye nafsi ya Jalidi na kuanza kumfanyia vituki vipy kila siku. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu sana hata Khalidi akachoshwa na vituko vya Jalidi.


Hali hii haikumpendeza khalidi hivyo akaamua kuhama kwenda mjini kwa kumkimbia jalidi na kwa kuepusha shari zaidi. Kule mjini Khalidi alifahamika sana wa uchamungu hata ikafikia watu wanampenda sana kwa uchamungu wake. Watu wakawa wanakuja kwake ili awaombee dua kwa Allah Muumba wa mbingu na ardhi. Basi Khali alihamia mjini na kwa pesa alizotoka nazo kijijini alinunua nyumba na kuanza kufanya biashara ndogondogo pale mjini.


Watu walimpenda sana Khalidi pale mjini kwa ukarimu, ucheshi na uchamungu wake. Watu kutoka mjini pale walikuwa wakienda kwa Khalidi na kumuomba awaombee dua. Watu wa mjini waliamini dua ukiombewa na Khalidi itkuwa ni yenye kukubaliwa na Mwenyezi Mungu. Basi pale mjini Khalidi aliishi maisha mazuri sana akiwa na upendo kwa watu hata akasahau vttuko vya jalidi. Biashara zake zilipata nuru na kipato chake kikawa kinaongezeka siku hadi siku.


Licha ya kuwa nyumba ya khalidi ilikuwa eneo zuri la kibiashara lakini nyumba yake ilikuwa ina kisima ambachoo katu hakikuwahi kukaukwa wala kuchimbwa upya kwa muda wa miaka 50. khalidi alitumia maji haya kwa matumizi ya nyumbani na akawa anatowa sadaka ya maji kwa wapita njia na watu wanaokujwa kununua biashara zake. Khalidi sasa amefika umri wa miaka 30 bila ya kuwa na mke. Sasa khalidi alikuwa akifikiria kupata jiko.


Siku moja bila ya kutarajia aliuona uso wa Jlidi pale mjini akija kumsalimia. Khalidi alimpokea Jalidi kwa tabasamu na bashaha akidhani ugomvi wao umekwisha. Jalidi alikaa pale kwa muda wa siku mbili na akawa anachukiwa sana na mafanikio ya Khalidi pale mjini. Basi siku ya tatu walipokuwa wanazungumza huku wanatembea wakati wa jioni wakapita karibu na kisima kile. Jalidi akajifanya anataka aelezwe mengi kuhusu kile kisima ila haukuchukuwa muda akamsukumiza khalidi kwenye kisima. Bila ya kujuwa kinachoendelea kwenye kisima alirudi nyumbani kijijini akiamini ameshammaliza Khalidi.


KUTOKA KWENYE KISIMA MPAKA KUWA MFALME.
Pale kisimani khalidi aliokolewa na majini waliokuwa wakiishi pale kwa muda wa miaka mingi iliyopita. Hata kabla ya kufika chini walimzi,isha na kumbebe na kumtua kidogokidogo na hakupatwa na madhara. Majini hawa walimpenda Khalidi kwa tabia zake njema na ukarimu uliopambwa na uchamungu wake. Hivyo hawakupenda damu ya mtu mkarimu iumwagike mule kisimani walipokuwa wakiishi.


Basi alipokuwa kati ya kupoteza fahamu na kurudi fahamu yaani akiwa kwenye mang’amung’amu akawasikia majini wakizungumza. “unajuwa mtoto wa mfalme wa nchi hii anaumwa sana na inapata miezi sita sasa bila ya kupona” wengine wakawa wanajibu “mimi sijapata kusikia hilo kabisa” kukatokea mmoja akasema “mimi nafahamu dawa ya ugonjwa wake” basi pale yule aliye anzisha mada akamuuliza “ni ipi dawa yake?” akamjibu “nyumbani kwa Khalidi kuna paka mwenye rangi nne na adimu sana paka hawa. Magoya saba ya mkia wa paka huyu ukiyachoma na ubani na harufu ikimpata vilivyo huyo mtoto wa mfalme kwa hakika atapona.


Wale majini hawakujuwa kama Khalidi amewasikia. Basi baa da ya muda wakamtoa pale ndani ya kisima. Khalidi alipitiwa na usingizi na aliposhituka akajikuta kitandani kwake. Alipoamka asubuhi akachukuwa magoya saba ya mkia wa ule paka akisubii kuona kama aliuwa anaota au ilikuwani kweli. Siku ile ilienda salama sana na hakukuwa na tatizo lolote, na huku Jalidi akaamini amemuuwa Khalidi,


Siku ilofata akaona ugeni unaingia kwake ni mfalme na msafra wake wakija kwakwe ili amuombee dua binti yake aliyekuwa anaumwa kwa miezi sita hata bila ya kupoona. Hapo khalidi akajuwa kumbe haikuwa ndoto ila ni ukweli. Pale akamchukuwa mgonjwa yule na akachukuwa udi na kachanganya na mgoya yale na akaomba dua. Hata kabla ya kumaliza alisikia kishindo. Mgonjwa alianguka chini na kupoteza fahamu.


Watu wakaanza kumpepea na mflme alijuwa lamda binti yake amepatwa na jambo. Baada ya masaa kadha akazinduka na hakuhisi maumivu yeyote. Hii inamaanisha alipona kabisa ugonjwa wake. Basi mfalme kwa furaha akamwambia “kijana kwa furaha nilizo nazo sina kikubwa cha kukulipa lakini naomba umuoe binti yangu” Khalidi alikubaliana na mawazo hayo na akamuowa binti mfalme. Kwakuwa mfalme hakuwa na mtoto wa kiume basi alopofariki Khalidi akapewa ufalme na akawa anaongoza nchi.


Miaka 15 sasa imepita toka aonane na Jalidi. Siku moja aliiona tena sura ya Jalidi ikiwa getini kuja kuomba msaada kwani maisha yamemuwia magumu. Jalidi alishangazwa kumuona Khalidi kuwa ndiye mfalme wao. Bila ya kinyongo Khalidi akamaidia Halidi n kumpati a vyakula na nguo kwa wingi sana na kumpatia na usafiri wa kubebea mizigo kwenda na yayo kijiji ni.


Kijana alipomaliza kusimulia hadithi hii akmwambia jini “nii ndio ilivyokuwa kati ya wagomvi wawili hawa, hivyo nakuomba unifanyie huruma kama Khalidi alivyomuhurumia Jalidi pindi alipomtumbukiza shimoni. Lile jini likasema “kwa hakika khabari hii inasikitisha lakini haiewzi kulinganisha hasira nilizo nazo . kwa hakika binti niliyemuuwa nilitoka nae mabli sana. Basi pale pale jini likapiga mguu chini na upepo mkali ukanibeba. Niliachwa kuleleni cha mlima uliopo pembenu ya ufukwe. Jini lile likanambia “nitakuonea huruma, sitakuuwa lakini nitakigeuza nyani” basi akanimwagia maji yamoto na palepale nikaanza kutowa magoya na kuota mkia. Kucha na hatimaye nikawa nyani kamili.


KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO.
Katika hali ya unyani nikajiambia “kama nikiishi msituni kwa hakika italiwa na chui bora niende kwa binadamu huenda nikapata muokoaji”. mwazo yangu yakawahivyo nikashuka pale na kuelekea ufukweni. Nikakuta kunajahazi linakaribia kuondoka. Basi niktafuta mti na kuutumia kama mtumbwi na kielekea kwenye jahazi.


Watu walishangaa sana kuona nyani anaweza kutumia nyenzo kuweza kuvuka. Wakaanza kukusanyika ili kuona akina ya nyani walioendelea kiasi hiki. Walikuwepo wengine wananipigia makofi na wengine wakawa wananicheka na wengine wananozonea. Mimi sikujali mpaka nikakamata jahazi na kukaa pembeni. Walikuwepo watu walotaka kunirudisha majini na wengune hata wakadiriki kunipiga mawae. Kwa bahati njewa nahodha wa jahazi akawakataza ni kuahidi kunilinda kwa maajabu niloonesha.


Haukupita muda ghafla jahazi letu likavamiwa na kundi kubwa la watu walooneka na ni waheshimiwa wenye madaraka ya juu serikalini. Mkubwa wao akajitambulisha “sisi ni watu wa baraza la mtukufu muheshimiwa mfalme. Karani muandishi wa mfalme amefariki mwezi ulopita hivyo tunatafuta mtu mwenye muandiko mzuri ili achukuwe nafasi” basi wakagawa makaratasi kwa kila mtu aandike chochote kwenye karatsi.


Basi walipomaliza na mimi nikaashiria nipewe karatasi ya kuandika. Basi nahodha akanipatia karatasi na kaamu na nikakaa mkao wa 4 na kushika kalamu vizuri kisomi. Watu wote walishangaa sana kuona nyani mwenye ujuzi wa hali yajuu hii. Basi niliandika mashairi machache ya kumsifu mfalme na kumjazia sifa kemkem. Kisha nikawapatia karatasi. Kwa hakika walishangaa sana kuona nyani ana ujusi wa namna hii.


Basi walichukuwa makaratasi yao na kuondoka, huko mfalme aliziangalia karatasi na kuupenda mwandiko wangu. Palepale aliamuru uletwe usafiri uje kunibeba. Nilibebwa kiheshimiwa zaidi na kuekwa mbele ya mfalme. Nilitowa heshima kinyaninyani na mfalme akaelewa. Alimipa karatasi niandike nikaandika tena mashairi ya kumpamba zaidi ya yale ya mwanzo. Kwakweli alistaajabu na kufurahi pia. Mfalme alikuwa anapenda sana kucheza bao. Hivyo aliashiria liletwe bao.


Basi nikacheza mechi na mfalme. Kwa mara ya kwanza nilimfunga nikaona amekasirika. Hivyo nikamwachia kanifunga goli tatu na kulipisha zote. Mwisho mfalme akaamrisha kiletwe chakula asi kikaletwa na sikula kinyaninyani nilinawa mikono na kula kwa kutumia mikono yangu. Yote nilokuwa nikiyafanya yalikuwa yakimstaajabisha mfalme na watu wa baraza lake.


Ilipofika jioni mfalme akaagiza aletwe binti yake wa kipekee ili astaajabu uwepo wa nyani mbele ya macho ya mfalme. Kama zilivyo tamaduni za waislamu mtoto wa kike hujifunika mwili wake ila kwa ndugu zake wa karibu na wazazi wake. Kwakuwa aliitwa na baba yake alukuja kawaida hat bila ya kujifunika. Ila maratu alipoingia kwa baba yake alihaza na kurudi nyuma na kwenye kujifunika kisha akarudi. Mfalme alishangaa kilichomsibu hata mwamnae akarudi.


Binti akaeleza “baba unaniita mbele ya mwanaume mwingine nikiwa sijajifunika” pale mfalme alishangaa na kumwambia “nipo mimi tu hapa na huyu nyani, ametoka wapi huyo mwanaume mwingie?”. akajibu “baba huyo sionyani ni mtu na amegeuzwa kuwa nyani kiuchawi. Ni aina za uchawi wanaotumia majini” basi mimi kusikia maneno yale nilitingisha kichwa kuashiria kukubaliana na maneno ya binti. Mafalme akamwambia “umeyajuwa vipi haya mwanangu?” binti akajibu “yule bib I aliyekuwa akinilea alinifundisha aina nyingi za uchawi na kuopoa”.


Basi mfalme akamtaka binti yake aniopoe na binti akakubali. Siku ilofata asubuhi sisi watatu tulielekea kwenye jumba bovu lililohamwa zamani am,bapo binti amelelewa na huyo bibi. Binti akatuambua mimi na mfalme kukaa pale na tusiondoke kwa loote lile litalotokea. Hivyo binti akaanza kuzungumza maneno yasiyojulukana. Ghafla akatokea nge na binti akageuka kenge akawa anamkimbiza nge amle. Yule nge akageuka tandu na binti akageuka nyoka.


Basi ikawa hivyo kila mmoja akigeuka flani mwinzie anageuka kitu kingine. Hali ilikuwa hivyo mpaka yule nge akageuka kunguru basi binti akageuka kipanga wakapaa wakikimbizaa na tusiwaone walipokwenda. Tulikaa pale kwa muda mrefu na tusiwaone. Ghafla tukaona punda aliyefundia kitu anakuja na akatema punje za komamanga. Kisha akageuka kuwa kuku mtembe na uanza kula punje za komamanga. Alizila zote alizoziona akawa anaashiria kama kuna ingine.


Kumbe kulikuwa na punje moja imebaki iliyokuwa ikibingiria kulekea kwenye mfereji wa maji. Aliiwahi aikamate lakini akachelewa na ikaangukia kwenye maji, na palepale ikageuka kuwa samaki. Binti akageuka kuwa samaki mkubwa zaidi na wakakimbizana mpaka yule samamki akageuka kuwa dragon na kuanza kumwaga moto. Binti akageuka kuwa dragoni na kutukinga sisi na motoule. Kwa bahati mbaya moto uke ulumchoma binti kwenye miyo na chehe ikajanipata kwenye jicho na kulipasua na hiyo ikawa ndio sababu ya chongo yangu ya jicho la kulia.


Baada ya mapamabno makali binti alifanikiwa kulichoma jini lile na kuliuwa. Alianguka chini na kuanza kuhe,a kwa uchovu. Alipopata nguvu akachukuwa majivu ya lieldragoni la kijini na kuchanganya na maji. Akatamka maneno na kunumwagia na palepale nikageuka kuwa mtu kamili. Furaha ilitanda kwa mfalme ila ghafla binti aliikata furaha hii kwa kumwambia “baba nimefanikiwa kumuuwa jini na kumtibu kijana, ila na mimi umri wangu umebakia siku tatau tu. Ule moto uliniunguza kweye moyo”.


Siku tatu binti alifariki dunia na majonzi yalienea kwa mfalme kwani alikuwa na mtoto mmoja tu. Baa da ya situ saba mfalme aliniita na kunambia “upo huru kwa sasa maana sio nyani tena. Nimefanikiwa kukuokoa lakini nimepoteza maisha ya binti yangu. Hivyo siwezi kukuangalia. Ninakuomba uondoke nchini hapa na usirudi tena, kwani uwepo wako utaendelea kunikumbusha binti yangu.


Basi nikaamua kuondoka nchini pale na nisijuwe pa kwenda. Nikaeekea baghdadi na nikanyoa kichwa cahngu na nyusi zangu. Nilipofika hapa nikakutana na wenzangu hawa na hatukupata kujuwa hadithi ya kila mmoja kati yetu. Hivyo hii ndio hadithi yangu. Zubeidah akamfuata waziri na kumwambia ataje stori yake yeye na wenzie basi akaeleza kuwa wao ni wafanya biashara wameomba hifadha pale baada ya kuingiliwa na usiku.


Basi mpaka wanamaliza kusimulia hadithi zao ilikuwa ni majogoo hivyo Zubeydah akwaaruhusu watu wote watoke mule ndani. Bila hata kuomba waruhusiwe kukaa mule mpaka asubuhi walitoka mbiombio. Mfalme aliyejifanya mfanya biashara akamwambia waziri “wachukuwe chongo hawa watatu na ukalale nao nyubani kwako na ifikapo asubuhi niitie wale wanawake watatu wote waje kwenye baraza letu nao wataje hadithi zao. Inaonekana kuna makubwa yamewafika.


Basi mambo yakawa kama alivyotaka mfalme, kesho asubuhi wale wadada wakaletwa mbele ya mfalme na mfale akawaambia “hatukuwaita kwa kuwaadhibu kwa mlichotufanyia jana ila tunataka mtueleze na nyinyi haithi zenu hata mkayafanya yale mlikuwa mkiyafanya. Zubeydah aliposikia sauti ile akajua niwale watu wa jana kumbe ni mfalme na watu wake. Basi akapiga magoti na wenzake wakafata na akaanza kuomba msamaha “tusamehe ewe mtukufu mfalme, kwa hakika hatukujuwa kuwa ni wewe mfalme, tumekukosea sana hata tukaweza panga kwenye shingo yako” mfalme akamjibu “nimekwisha samehe tafadhali aeni bila wasi na mueleze hadithi zenu.


Mfalme akawa anawashawishi kwa maneno mazuri na kuwaambia “nioneni kama mpo na rafiki zenu hapa na kuwa huru kusema chochote kile”. basi mabinti wakaanza kuangaliana wakitafakari ni nani aanze kusimulia hadithi yake. Kabla hawajaanza na wale machongo watatu wakaletwa ili wapate kusikiliza hadithi za wadada hawa. Basi wakaanza kusimulia hadithi zao kama ifuatavyo;-


Kupata mwendelezo wa Hadithi hii soma hadithi ya Wanawake watatu wa baghadad
Pata kitabu Chetu Bofya hapa