Navigation Menu



HADITHI ZA ALIF LELA U LELA (sehemu ya kwanza): KIAPO CHA SULTAN

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA (sehemu ya kwanza): KIAPO CHA SULTAN

kiapo Cha Sultani

www.bongoclass.com

KIAPO CHA SULTANI

KIAPO CHA SULTANI.
Hapo zamani sana katika nchi za Uajemi , china na hindi kulitokea sultani aliyefahamika kwa kuwa na upendo kwa watu wake na nguvu pia ya kijeshi na kuitawala. Watu wake walimpenda sana na yeye aliwapenda. Sultani huyu alikuwa na watoto wawili ambao ni Shahriyar ambaye ndiye mkubwa na mwingine ni Shahzanam ambaye ndiye mdogo.


Watoto hawa pia walitambulika kwa ushujaa walio nao na uhodari katika mambo mbalimbali, hususan katika fani ya kupanda farasi. Sultani huyu alipofariki utawala wake akamwachia mwanaye mkubwa ashike madaraka yake. Na mwanae mdogo akabakia anatawala maeneo mengine katika utawala wa baba yake. Huyu mdogo akaelekea maeneo ya Samarkand na huyu mkubwa akabaki palepale.


Sultan Shahriyar alikuwa na mke wake aliyempenda sana kwa muda mrefu. Hakuwahi kuamini kama itaweza kutokea sikumoja akamsaliti. Ilitokea sikumoja akamkuta mkewake anazini na mtumwa wake. Kitendo hiki kilimuuma sana na akamuuwa mkewe na yule mtumwa. Kutokea hapo akaapa kutokumwamini mwanamke yeyote duniani. Na kitendo hiki kilimfanya ajiwekee utataratibu mpya wa maisha nao ni kuoa kila siku mke mpya na kisha humuuwa ifikapo asubuhi.


Hivyo mambo yakawa kama hivi kila siku jioni bibi harusi mpya mwanamwari huolewa na na ikifika asubuhi huuliwa. Kitendo hiki kiliendelea kwa muda mpaka watu wakawa wanaogopa. Ikiwa nyumba moja watu wanalia kwa kufiwa na bint yoa nyumba nyingine hufanyika harusi. Sultani alikuwa na waziri wake maalum ambaye alikuwa amepewa kazi hii ya kumletea mfalme wanawari na kutekeleza amri ya kuwauwa kila ifikapo asubuhi.


Waziri huyu aliyepewa kazi hii alikuwa na watoto wawili aliyewapenda sana, mmoja aliitwa Schehra-zade ambaye ndiye mkubwa na Dinar-zade ambaye ndiye mdogo. Schehra-zade alipata upendo mkubwa kutoka kwa baba yake. Alipewa taaluma mbalimbali za matibabu, sanaa, kuandika, masimulizi , kazi za mikono na nyingine nyingi. Ukiacha mbali na taaluma hizi pia alijulikana kwa uzuri wake ulioaminika kuwashinda wanawake wote katika nchi hiyo. Mabinti wawili hawa walipendana zaidi kila mmoja.


Ilitokea siku moja katika mazungunzo waziri mkuu akiwa na mabinti zake wanaongea Schehra-zade alitowa ombi kutoka kwa baba yake ambalo lilionekana kumshangaza sana. “baba ninaombi ila niahudi kwanza kuwa utanitekelezea” alizungumza Schehra-zade kumwambia baba yake. “naahidi nitalitekeleza kama lipochini ya uwezo wangu” alisikika waziri mkuu akimjibu binti yake.


“ninataka kukomesha tabia ya kikatili ya sultani kuuwa mabint” mmmmhhh mwanangu kipenzi, vip utaweza kumaliza tabia hii ya sultani wetu? Ni maneno yaliyokuwa yakizungumzwa kati ya waziri na mwanae. “baba ninataka unipeleke mimi kwa sultani niwe mkewe” alizungumza Schehra-zade. Mwanangu unafahamu fika kuwa ukuolewa punde tu ifikapo asubuhi nitaamriwa nikuuwe” alizungunza waziri kwa masikitiko makubwa.


Schehra-zade aliendelea kusisitiza ombi lake la kutaka kuolewa na sultani ili akamalize tabia yake ya kuuwa mabinti. Waziri nae hauacha kumsihi mwanae asithubutu kijiingiza kwenye matatizo haya makubwa. Wazii akawa anamwambia mwanae “ hivi mwanangu unataka nikufanye kitugani mpaka uachane na msimamo wako huo? Au unataka yakupate yalompata mke wa mfugaji?” kwa shauku Schehra-zade akauliza “kwani baba ni kitu gani kilimpata mke wa mfugaji” mmmmhh.. Ni habari kubwa lakini nitatakusimulia hadithi yake” alizingumza waziri na kuanza kusimulia hadithi hii


KISA CHA MFUGAJI NA MKEWE.
Hapo zamani kulikuwa na mfugaji maarufu sana na alikuwa ni tajiri na mfanyabiashara aliyekuwa na mafanikio makubwa. Alikuwa anaelewa lugha za wanyama. Alipata tunu hii kwa sharti kuwa asisimulie kwa yeyote mazungumzo ya wanyama na pindi tu akisimulia alichokisikia atakufa hapohapo. Alikuwa akifurahia sana kuwaona wanyama wake na kujuwa nini wanazungumza. Alikuwa na banda lake la wanyama ambapo ndani kulikuwa na ng’ombe na punda, ambapo kazi ya kuwasimamia wanyama hawa alimpa mtumwa wake.


Sikumoja alipkuwa amekaa pembeni mwa banda hilo akasikia mazungumzo ya kustaajabisha kati ya punga na ngo’mbe. Ngombe akamwambia punda “ nakuonea wifu kwa raha unayoipata. Wakati mimi ninashinda juani kulima shamba la bwana wetu wewe mwenzangu unaogeshwa na kupambwa na kazi yako ni kummeba bwana wetu, wananipiga, wananifunga majembe yao shingoni. Nakuonea wivu natakani ningekuwa wewe” punda akamwambia ng’ombe “usijali nitakueleza jambo ukilifanya katu hautalimishwa tena.. Kesho akija mfanyakazi mpige mateke na mtishe kwa pembe zako na umfukuze. Kataa kula chakula chao. Ukifnya hivi katu hawata kulimishwa tena”


Siku iliyofuata ng’ombe akafanya kama alivyoshauriwa na punda, akamtisha mfanyakazi na akamkimbiza akataka kumchoma kwa pembe zake. Alikataa kula chakula. Siku iliyofuata mfanyakazi akakuta kile chakula alichokilet jana kipo vilevile hivyo akatoa taarifa kwa bwana wake. Mfugaji akamuamuru mfanyakazi wake amchukuwe punda kwenda kulima amfanyie mazoezi. Hivyo siku ile punda akapew mazoezi ya kulima na akalima pia kwa jembe la kubuluza (plau). Jioni akarudi akiwa amechoka sana.


Kufika hapa waziri akamwambia mtoto wake Schehra-zade “binti yangu hivi unataka kuangamia kama punda alivyomshauri mwenzie vibaya na akaumia mwenyewe?” Schehra-zade akamwambia baba yake “baba bado msimamo wangu upo pale pale nipeleke kwa sultani nikakomeshe tabia yake. Lakini baba bado sijajuwa mke wa mfugaji kilichompata?” alizungumza Schehra-zade kutaka hadithi iendelee. Waziri akaendelea kumsimulia Schehra-zade hadithi hii


Siki moja mfugaji akiwa na mkewe wameketi karibu na banda la wanyama hawa ili kujuwa nini punda atamshauri mwenzie. Akamsikia punda akimwambia ng’ombe “rafiki yangu nakupa ushauri unisikilize vizuri. Nimemsikia bwana wetu akimwambia mfanya kazi kuwa kama hali yako utaendelea nayo basi uchinjwe na upelekwe buxher ukauzwe nyama. Hivyo nakushauri kesho utii amri ya mfanya kazi hivyo atadhani kuwa ulukuwa umeumwa na sasa umepona” ngo’ombe alionekana kutii ushauri huu. Hapo mfugaji akacheka sanaa. Kicheko hiki kilistaajabisha hata mkewe. Mkewe akataka kujua kinachomchekesha akamjibu ni siri na nikikwambia nitakufa ila naweza kusema kuwa ninacheka kwa sababu ya mazungumzo kati ya punda na ng’ombe.


Mke huyu alionekana kuwa na msimamo wa kutaka kujuwa hasa nini mazungumzo hayo nini kilisemwa mpaka akacheka. Akaahidi kama asipomwambia atarudi kwao. Ugomvi ukawa mkubwa ikafikia hatuwa ya kuita ndugu waje kusuluhisha. Mfugaji akabaki na msimamo wake kuwa kama atasema atakufa paohapo na mke akafikia kusema kama asipi niambaia na mimi nitajiuwa. Hali hii iliendelea kwa muda mpaka kufikia hali mbaya zaidi. Mfugaji akiwaza nimwambie ili nife kwa kumridhisha mke wangu au nisimwambie. Na nisipo mwambia atajiuwa. Ni mawazo ya mfugaji. Ugomvi uliendelea kwa siku kadhaa bila ya maelewano pale ndani.


Siku moja alikaa nyumbani kwake ghafla akamuona mbwa wake aliyempenda sana anamkimbilia jogoo la kuku. Kisha akamuelezea mambo yote yaliyompata bwana wake yaani mfugaji na mkewe. Hapo jogoo akacheka sana kisha akamwambia “bwana wako ni mpumbavu kweli, hivi hauniono mimi nina wake zaidi ya hamsini hapa na ninafanya ninalo taka, lakini yeye ana mke mmoja tuu pia anampa wakatimgumu hivi. Akieleza siri atakufa hapa dawa ni ndogo tu. Achukuwe fimbo mzuuri kisha amtandike kisawasawa, bila shaka atarudisha akili yake.” Baada ya maneno haya jogoo likawika na kuondoka zake kwa mwendo wa madaha.


Mfugaji alifikiri atumie ule ushauri wa jogoo, asubuhi ya siku ilofata mke wa mfugaji aliendelea na vurumai lake. Mfugaji akaagiza aletewe bakora nzuri na kutekeleza ushauri wa jogoo. Mambo yakatulia nyumbani na hakuleta vurumai liole tena. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii waziri akamwambia Schehra-zade “binti yangu, je unataka na mimi nitumie uamuzi wa jogoo?” Schehra-zade akamwambia baba yake “hapana baba ila mi nadhani hadithi hii hainitoshelezi kubadili uamuzi wangu”. Basi waziri baada ya mazungumzo marefu akakubaliana na maamuzi ya mwanae na kukubali kumpeleka kuwa bibi harusi kwa sultan kwa usiku uliofuata.


Siku ile waziri akaenda kwa sultan kwa masikitiko na majonzi akamweleza sultan kiola ambacho kilitokea kati ya yeye na binti yake. “sultan Schehra-zade anataka kwa heshima yako awe mkeo japo kwa usiku mmoja tu. Nimejaribu kumnasihi na kumkataza kwa hali zote nilizoziweza lakini imeshindikana” ni mameno ya waziri alo,mwabia sultan. “Unajuwa fika kuwa asubhi baada ya harusi itabidi ushukuwe amri ya kumuuwa na ukishindwa na wewe pia utauliwa na kichwa chako kutundikwa.” ni mameno ya mfalme akisikika anamwambia waziri. Baaada ya mazungumzo marefu Waziri akarudi nyumbani kwa majinzi na kumueleza binti yake ajiandae kwa harusi jiono ilofata.


Schehra-zade akamueleza mdogo wake Dinar-zade “mdogo wangu ninaombi unifanyie huenda likawa ndio la mwisho kabla sijauliwa au likanusuru maisha yangu na maisha ya mabinti wengine wa nchi hii”. Nilipi hilodada? Dinar-zade alimuuliza dada yake. Schehra-zade akaendelea kumweleza “nitakapokuwa nimeingia kwa mfalme nitamwomba ruhusa ya kuwa na wewe katika chumba kile ili nipate kukuaga kabla sijauliwa. Hivyo nikipewa ruhusa hivyo itakapofika saa 11 alfajiri niamshe kisha uliombe nikusimulie hadithi nzuri iwe kama furaha ya kuagana”. Mdogo wake akakubaliana na wazo hilo la dada yake.


Hal ilikuwa kama hivyo na harusi ikafanyika kati ya sultan na bint wa waziri mkuu. Bibi harusi akaingia kwenye jumba la kifalme huko akakutana na sura ya sultani. Kwa madaha na manjinjo akamuomba ombi lake la kuruhisiwa kuwa na mdogo wake usiki ule katika chumba kimoja ili aweze kumuaga kesho asubhi kabla ya kuuliwa. Sultan akakubali ombi lile na kuamuru Dinar-zade aletwe na chemba maalumu ikaandaliwa ndani pale.


Mambo yakawa kama hivyo usiku haukuwa mrefu kati ya mabint wawili hawa. Ilipofika lisaa limoja kabla ya kupambazuka Dinar-zade akamwambia dada yake “dada yangu kipenzi, naomba unifurahishe kwa kunisimulia hadithi nzuuri iwe kama furaha ya mwisho ya kuagana kabla ya kuuliwa” Schehra-zade kabla ya kumjibu mdogo wake akaomba ruhusa kwa sultan ili amruhusu aweze kutimiza matakwa ya mdogo wake kipenzi. “hakuna shida msimulie tuu ….”’ ni maneno ya mfalme. Hapo Schehra-zade akaanza kusikumulia hadithi kama ifuatavyo.



Pata kitabu Chetu Bofya hapa
  1. 1
  2. 2

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 1191


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

UFUPISHO WA ALIFU LELA ULELA KITABU CHA KWANZA
Posti hii inakwenda kukisimulia kuhusu hadithi za alifu lela ulela KITABU CHA KWANZA Soma Zaidi...

Ndoa ya Sinbad na binti mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Hadithi ya binti wa kwanza na mbwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

HADITHI YA KHALID MWENYE KUNEEMESHWA NA JALID
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA KHALIDI MWENYE KUNEEMESHWA NA JALID. Soma Zaidi...

Safari ya sita ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari za Sinbad Soma Zaidi...

Hadithi ya chongo wa tatu mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

HADITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE. Soma Zaidi...

alif lela u lela
Download kitabu Hiki Bofya hapa Kupata mwendelezo wa hadithi hii Download App yetu. Soma Zaidi...

Kisa Cha mfugaji na mkewe
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya mzee wa pili na mbwa wawili weusi
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...