Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA SABA YA SINBAD Walipokusanyika siku ilofata Sinbad akawaambia kuwa kilichofanya nikavunja ahadi yangu ya kutosafiri tena ni kauli ya Sultani Nilipopunzika kwa muda wa miezi miwili nilipata habari kuwa Sultani
Download kitabu Hiki Bofya hapa
SAFARI YA SABA YA SINBAD
Walipokusanyika siku ilofata Sinbad akawaambia kuwa kilichofanya nikavunja ahadi yangu ya kutosafiri tena ni kauli ya Sultani Nilipopunzika kwa muda wa miezi miwili nilipata habari kuwa Sultani ananiita. Nilipokwenda alinieleza kuwa anataka nipeleke barua yake kwa mfalme wa Serendib ya kumjibu kuwa ameridhika na urafiki. Nikamueleza kuwa nimeweka ahadi ya kutousafiri tena kutokana na yalonikuta. Sultani alisisitiza sana mimikwenda na akaniambia kuwa mimi ndie mtu nafaa zaidi kwani mfalme wa Serendib ananijua.
Basi nilikubaliana na amri ya Sultani na ikaandaliwa safari ya kifalme na jahazi lililo madhubuti zaidi na la kisasa liliandaliwa na Sultani mwenyewe. Baada ya maandalizi kukamilika mali nyingi kama zawadi ziliandaliwa kwa ajili ya mfalme. Safari ilianza salama na tuliwasili Serendib kwa amani muda wa jioni. Mfalme wa Serendib alinipokea mwenyewe na kunikumbatia na kunivika joho lenye ukosi ulochovywa kwenye dhahabu nyekundu.
Mfalme alilidhika na zawadi zile na alifurahi sana kwa kuniona. Mfalme alifurahi zaidi kuona barua ile imejibiwa kama atakavyo. Mafalme wa Serendib akaniozesha mtoto wake kama takrima ya udugu wetu. Ndoa ilifanyika salama na baada ya kukaa pale kwa muda wa mwezi mmoja nilipewa ruhusa ya kuondoka mimi na mkewangu na zawadi nyingi kwa ajili yangu na kwa ajili ya Sultani wa Baghadad.
Mfalme mwenyewe aliandaa jahazi na kulimadhiubutisha na safari iliandaliwa kifalme kwani ndani mlikuwa na mkwe na mtoto wa mfalme. Tuliwasili Baghadadi baada ya mwe ndo wa siku kumi na tano. Na Sultani alitupokea kwa heshima zote na kukutana na binti wa Mfalme wa Serendib. Sultani alitufanyia sherehekubwa kama ile ilofanyika wakati wa harusi kule Sererndib. Kwa hakika ilikuwa ni furaha kubwa zaidi. Na huu ndio mwisho wa safari zangu saba za majini.
Mpaka sasa nina wake watatu mmoja nilishamuoa nilipokuwa kijana na mwingine ni yule nilookoka nae kwenye makaburi na wa tati ni huyu. Na nimebahatika kuoa mabinti wawili wa wafalme. Kisha Sinbad akawaomba wakezake wote waje ili Sinbad wa nchikavu awaone, kisha akamkutaninisha na yule mzee wa bostani alokuja nae Sinbad. Kisha Sinbad wa baharini akamuuliza Sinbad wa nchikavu “je! Unafikiri sistahiki kupata maisha haya kwa sasa?, je! Kuna yeyote unayemfahamu amepata taabu kama mimi?” majibu ya maswali haya alibakia nayo Sinbad moyoni kwa mshangao.
Baada ya pale Sinbad wa majini akamwambia Sinbad mbeba mizigo kuwa sasa tumeshakkuwa marafiki. Kwa siku saba hizi umekuwa kama ni ndugu yangu sasa. Naomba uje na familia yako tukae hapa kama ndugu. Sindab mbeba mizigo akakubaliana na ombi lile na waliishi na Sinbad kwa muda mrefu sana. Waliishi kama kaka na ndogoake. Hata alipofariki Ndugu wa Sinbad wakamchagua kijana Sinbad mbeba mizigo awe ndiye msimamizi mkuu wa mali za mzee Sinbad. Kwa hakika maisha yao yalikuwa mazuri sana na mahusiano yao na ya Sultani wa Baghadad na mfalme wa Serendib hayakukoma.
Mpaka kufikia hapa Schehrazade akamaliza hadithi hii ya Sinbad, na tayari miezi mingi ilishapita bila ya kuuliwa na Sultani Shahariyar. Baada ya hapa Sultani Shahariyar akauliza “hatujajua kilichomkuta mtoto wa Sinbad aliyemzaa kutoka kwa ‘Aisha mtoto wa mfalme” Dinarzade akamwambia “ni hadithi ya kusisimua sana” na kama utaniongeza muda zaidi wa kuishi nitakusimulia hadithi nzuri zaidi ya yalomkuta mtoto wa Sinbad.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowDownload kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME.
Soma Zaidi...Download kitabu Hiki Bofya hapa NDOTO YA MGONJWA BINTI WA MFALME.
Soma Zaidi...Download kitabu Hiki Bofya hapa KISIWA CHA UOKOZI Nikajisogeza vyema hata nikafika kwenye kivuli.
Soma Zaidi...Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA KWANZA YA SINBAD Tambua kuwa baba yangu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana katika nchi ya baghdad wakati wa utawala wa sultan harun Rashid.
Soma Zaidi...Download kitabu Hiki Bofya hapa NDOA YA SINBAD NA BINT MFALME.
Soma Zaidi...Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA.
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari saba za Sinbad
Soma Zaidi...