Baada ya kukatika kwa Wahyi kwa muda wa masiku kadhaa hatimaye Jibril akaleta tena wahyi kwa mara nyingine.
GABRIELI ALETEA UFUNUO WA ALLAH TENA:
Ibn Hajar alisema: "Kusimama kwa ufunuo (wahyi) wa Allah kwa siku chache kulikuwa ni ili kumtuliza Mtume wa Allah (Rehema na amani zimshukie) kutokana na hofu aliyokuwa nayo na pia kumfanya atamani sana kuupokea ufunuo. Wakati hali ya mkanganyiko ilipoondoka, alama za ukweli zilionekana, na Mtume wa Allah (Rehema na amani zimshukie) alijua kwa hakika kwamba alikuwa amekuwa Mtume wa Mola Mkuu. Alikuwa na uhakika pia kwamba kile kilichomjia kilikuwa si kingine bali ni mjumbe n wahyi kutka kwa ALLh. Kutamani kwake kuupokea ufunuo huo kulikuwa sababu nzuri ya uimara wake na utulivu wake wakati wa kupokea ufunuo wa Allah."
Al-Bukhari ameripoti kutoka kwa Jabir bin ‘Abdullah kuwa alimsikia Mtume wa Allah (Rehema na amani zimshukie) akizungumza kuhusu kipindi cha kusimama kwa ufunuo kama ifuatavyo:
“Wakati nilipokuwa natembea, nilisikia sauti kutoka angani. Nilipoinua macho yangu, kwa hakika alikuwa ni yule malaika yuleyule aliyenitembelea katika pango la Hira’. Alikuwa ameketi kwenye kiti kati ya ardhi na mbingu. Niliogopa sana na nikapiga magoti chini. Nilirudi nyumbani nikisema: ‘Nifunikeni…, nifunikeni…’. Allah aliniteremshia aya:
‘Ewe uliyejifunika (kwa nguo)! Inuka ukahadharishe! Na Mola wako Mtukuze! Na nguo zako zitakase! Na uepukane na uchafu (sanamu)!’” [74:1-5]
Baada ya hapo, ufunuo ukaanza kuja kwa nguvu, mara kwa mara na kwa mpangilio.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza mchango mkubwa wa nyumba ya Arqam Ibn Abi AL Arqam katika historia nzima ya Uislamu
Soma Zaidi...Mwaka wa 10 toka kupata utume, Mtume Muhammad (S.A.W) anaanza kulingania dini nje ya Mji wa Makkah
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz ahistoria ya kuhamia Madina kwa waisalmau. Namna ambavyo walihama na mateso waliokuwa wakiyapata.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuusu malezi na makuzi ya Mtume Muhammad ﷺ akiwa kwa bibi Halima
Soma Zaidi...katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Mazazi ya Mtume MUhammad ﷺ na kupewa jina.
Soma Zaidi...Katikasomo hili utakwenda kujifunza stori maarufu ya Bahira kuhusu kukutana na Mtume Muhammad ﷺ na kumtambuwa utume wake.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu tukio la Kupasuliwa kwa Kifua Mtume Wakati Akiwa Mtoto
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu ndoa ya Mtume Muhammad ﷺ na Bi Khadija
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza njia zilizotumika kuwafikishia wahyi Mitume wa Allah amani ishuke juu zao
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza historia ya Adui wa Mtume Muhammad ﷺ mwanzoni mwa kuenea kwa Uislamu Makkah.
Soma Zaidi...