Katika somo hili utakwend akujifunza faidaza kiafya za kula njegere
Njegere ni mboga jamii ya kunde. Njegere ni mboga tamu, kama hujawahi kuila, tafuta siku ujaribu. Mboga hii, mbali na utamu wake, imekuwa ikitajwa sana katika nyanja za afya. Hivi unazijua faida za kula njegere? Hakika, faida zake ni nyingi sana kiafya, kimwili, na hata kwa utamu. Makala hii inakuletea faida za kiafya za kula njegere.
Virutubisho Vingi Njegere zina virutubisho vingi sana ukilinganisha na mboga nyingi. Njegere zina vitamini A, K, B, na C. Pia, njegere zina madini ya chuma, manganese, phosphorus, na folate. Njegere pia zina protini na nyuzinyuzi. Katika mboga, njegere ni mojawapo ya mboga zinazokusanya protini kwa wingi sana.
Kudhibiti Kiwango cha Sukari Mwilini Njegere husaidia kudhibiti matumizi ya sukari mwilini. Hii husaidia kuwapa nafuu watu wenye kisukari aina ya pili (type 2 diabetes). Hali hii pia husaidia kuboresha afya ya moyo.
Kuboresha Afya ya Mfumo wa Mmeng'enyo wa Chakula Kama unasumbuliwa na kukosa haja kubwa, njegere ndio mtatuzi wako. Njegere husaidia kuondoa vimbe zilizopo kwenye njia ya chakula na kufanya choo kiwe kizito na kupita kwa urahisi. Pia, njegere husaidia kuzuia saratani ya utumbo mpana na kusaidia kuondoa chakula chote kupitia haja.
Kulinda Mwili Dhidi ya Maradhi Hatari Njegere husaidia kulinda mwili dhidi ya maradhi hatari kama saratani, maradhi ya moyo, na kisukari. Kwa sifa hii, njegere ni mboga pekee ambayo unatakiwa uile mara nyingi kwa lengo la kujikinga na maradhi haya. Hata hivyo, kwa ambaye ni mgonjwa tayari, mboga hii itamsaidia kupunguza uzito wa tatizo.
A. Kuzuia Maradhi ya Moyo: Njegere zina madini ya magnesium, potassium, na calcium. Ulaji wa chakula chenye madini haya kwa wingi husaidia kuzuia shinikizo la juu la damu (presha ya kupanda) ambalo ndio chanzo kikuu cha maradhi ya moyo. Pia, ndani ya njegere kuna flavonols, carotenoids, na vitamini C. Pamoja, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya moyo kwa sababu huzuia uharibifu wa seli.
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula ukwaju
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula maharagwe
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu vitamini D, kazi zake, vyanzo vyake na upungufu wake mwilini.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula kitunguu ssaumu - garlic
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kjifunza faida za kiafya za kula njugumawe
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu vyakula vya protini, faida zake na vyanzo vyake.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula nazi
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula nanasi
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula tunda embe
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula nazi
Soma Zaidi...