SIRI YA KIFO INAFICHUKA

SIRI YA KIFO INAFICHUKA


SIRI YA KIFO YAFICHUKA



Kijana akaanza kueleza kuwa huyu binti ni mkewangukabisa na ni mtoto wa mjpomba wangu, na huyo mjomba ni huyu mzee. Mimi na mkewangu tuliiishi vyema sana. Mkewangu alinipenda sana na miaka yote tulioishi sikuweza kumuona na tabia mbaya hata siku moja. Niliweza kuzaa nay watoto watatu. Siku moja alikuwa anaumwa, maradhi haya yali dumu kwa muda uliokaribia mwezi mmoja kisha akapata nafuu kidogo. Haikuchukuwa muda mrfu akaumwa tena baada ya siku kadhaa akapata nafuu tena.


Siku moja alinipa matumaini kuwa kuwa amepata nafuu sana. Sasa akaniambia kuwa ana hamu na tunda epo na hatokwnda kuoga mpaka ale tunda hilo. Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana mke wangu. Nilikwenda kumtafutia tunda epo popote pale. Nilihangaika sana kwenye mabostani mengi ya mjini. Lakini bila mafanikio. Siku hiyo nilirudi mtupu kwa mke wangu. Loo siku hiyo mke wangu hakwenda kuoga. Basi siku ilofata nikatoka tena kwenda kutafuta tunda epo. Wakati nilipokuwa nimekata tamaa kabisa ya tunda ndipo nikakutana na mze mmoja akanileza kuwa kuna mji matunda hayo yanapatikana. Basi nikafunga safari kulekea huko.


Safari ilinichukuwa siku tatu hata kufika na kurudi na nilinunua matunda matatu kwa gharama ya vipande 15 vya dhahabi. Cha ajabu niliporudi mke wangu hakuwa tena na hamu ya tunda epo. Lakini alichukuwa matunda yale na kuyaweka kwenye kabati. Siku tatu zikapita bil mke wangu kugusa yale matunda. Basi siku ya nne nilipokuwa mtaani nilikutana na kijana mmoja mtanashati sana akiwa na tunda la epo. Kijana yule nikamuuliza wapi amepata ili nikanunue mengine. Kijana akanieleza kuwa “nimepewa na mpenzi wangu kama zawadi, mumewe alikwenda mbali safari ya siku tatu kununua maepo matatu kwa thamani ya vipande 15 vya dhahabu. Na mkewe ambaye nimpenzi wangu wa siri akanipatia kama zawadi.


Niliposikia maneno haya nilistaajabu sana na kuvurugwa moyo wangu. Nilitoka mbio hadi kwa mke wangu. Nilipoangalia kabatini nilikuta tunda moja halipo na yamebakia mawili. Nilistaajabu na kuyasadikisha maneno ya yule kijana. Nilimkamata mkewangu na kmchoma kisu cha tumbo kisha nikamchinja na kumkatakata vipande na kuvifunga kama ulivyoona kwenye boksi. Baadaye nilianza kujuta sana na kulia sana.


Kitu cha ajabu siku ya tatu niimkuta mwanagu analia sana. Nilikuwa na uhakika kuwa hatambui kuwa kama mama yake nimemchinja. Basi nikamuuliza mwanangu kipi kinakuliza?. akanieleza kuwa “naogopa mama akirudi atanipiga, matunda yake matatu nimechukuwa mmoja, nikaenda nalo kucheza. Mkaka mmoja akaninyang’anya na kunipiga, nikamwambia kuwa ni la mama ameletewa na baba kutoka mbali safari ya siku tatu na amenunua kwa thamani ya vipande vitatu vya dhahabu. Yule mkaka akakimbia nalo” basi hapo hapo nikamwambia mwanangu anyamaze.


Dah nikagundua kuwa yule kijana alikuwa ni muongona ndiye chanzo cha kifo cha mke wangu. Niliia sana sanaaaa. Baba mkwe wangu ambaye ni mjomba wangu huyu hapa akaja. Nikamueleza kila kitu naye alilia sana. Hivyo khalifa mimi ndiye niliyemuuwa huyu binti, tafadhal niadhibu mimi niweze kulipa deni la nafsi ya mke wangu. Baada ya kusikia habari hii khalifa akamueleza waziri Mansur. “Nenda ukanitafutie huyu kijana, ninakupa siku tatu tu, na endapo hutamleta nitakuchinja kama alivyochinjwa huyu binti”.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Download App yetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela2 Main: Burudani File: Download PDF Views 713

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

ALIF LELA U LELA KITABU CHA PILI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KITABU CHA PILI HADITHI ZA ALIF LELA U LELA UFUPISHO WA ALIF LELA U LELA KITABU CHA KWANZA.

Soma Zaidi...
ALADINI NA BINTI WA MFALME.

ALADINI NA BINTI WA MFALME.

Soma Zaidi...
Hadithi ya Kaka wa tatu wa kinyozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...
Kukatwa mkono na kuurithi utajiri

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...
Hadithi ya Kaka wa pili wa kinyozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...
Nje ya jumba la kifahari la aladini

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

Soma Zaidi...
Alif lela ulela

Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Ujumbe wa Siri kwenye kitabu cha ajabu

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

Soma Zaidi...