HISTORIA YA PANGO, ALADINI NA KITABUAladini alipofika kwake alikuwa na mawazo sana, maana ilibakia kidogo aingie majaribuni. Aladini sasa alikuwa na mawazo kuwa muda wowote asipokuwa makini anaweza kupoteza kila kitu. Kwa mawazo yote aliamua akalale. Katu usingizi hakuweza kupata hata lepe la usingizi. Aladini akiwa kwenye fikra na mawazo haya ghafla aliwaza kile kitabu. Aladini alifikiri hasa ni nini chanzo cha lile pango na ni kitu gani kimeandikwa kwenye pango lile. Aladini akapatwa na hamu kubwa ya kusoma, ijapokuwa Aladini hakukulia katika mazingira ya kupenda kusoma. Aladini alifikiri ili aweze kuelewa vyema akaoge. Pia huenda alikwenda kuoga kwa sababu Aladini aliamini kuwa kitabu kile kitakuwa ni kitabu kitukufu hivyo si vyema kukigusa bila hata kuoge.


Baada ya kumaliza usafi wa mwili Aladini akakamata kitabu akiwa yupo kitandani kwake. Hata mkewake alishangazwa sana na tabia ya mumewe leo kusoma. Kwa hakupatapo kumuona akisoma hata. Gamba a juu la kitabu lilikuwa ni la ngozi iliyokunnwa vyema. Gamba la juu lilikuwa ni chakavu na halikuweza kuonyesha chochote katika picha wala maandisi. Lakini mshangao mkubwa ni pale Aladini alipofunua ukurasa wa kwanza wa kitabu ambapo alikuta picha ya pete aliyovaa, mshumaa wa ajabu, yule ndege wa ajabu, vile vijiwe vya pangoni, vile vijiko pamoja na kit kama yai. Lakini kitu hiki kumeandiwa juu na nyuki kadhaa wa dhahabu. Picha hizi hazikuwa na majina. Hapa Aladini akaanza kupatwa na mshangao na kuanza kufikiri kuwa huwenda mambo yote aliyokutana naye yalishatabiriwa kwenye kitabu hiki.


Aladini alizidiwa na ushawishi na madukuduku. Aladini hakuridhishwa na zile picha alitaka sasa kuona nini maana ya picha zile. Ndipo akafunguwa ukurasa unaofata. Loo! Aladini alistaajabu zaidi kuona kuna mchoro wa sura yake, mkewe, baba yake na pia kulikuwa na sura mbili za watu ambazo ni ngeni sana kwa Aladini. Watu hawa alikuwa ni babau yake na mchawi wa pili. Aladini alianza sasa kuamini kuwa kitabu kile kuna familia yake, hivyo kuna uwezekana wa uhusikaji wake katika pango lile. Chini ya ukurasa huu kulikuwa na maandishi ya lugha asiyoijuwa. Lakini maandishi hayo yalifanana sana na maandishi ya majini.


Ukurasa uliofuata ulikuwa na rangi nyeusi tupu na maandishi ya rangi nyeusi yaliyoweza kuonekana kwa mbali sana, kama vile jongoo kwenye usiku wa kiza. Maandishi yaliweza kusomeka kwa mbali sana. Aladini akabaki kukodoa mimacho tuu. Baada ya kutazama kwa muda mrefu maandishi yale yakaanza kubadilika taratiibu kuwa meupe na kuanza kusomeka vyema. Mambo haya yalimshangaza sana Aladini. Muda wote Aladini alikuwa akisoma kitabu akiwa amelala kichalichali. Basi akajigeuza upande wa kulia. Wakati anajigeuza kwa bahati mbaya alikifunga kitabu. Alipokuja kukifungua kila alichokisoma na kukiona kwenye kitabu kile hakikuweza kuonekana tena. Zilibaki kurasa tupu. Dah aladini alistaajabu sana, na alitambuwa kuwa hakuna kinachobakia kwenye kitabu hiki baada ya kukisoma.


Kwa kuwa Aladini hakuweza kusoma yale maandishi yaliyokuwa yakisomeka baada ya kukodoa macho kwa muda maandishi yakaanza kurudi tena. Maandishi hayakuwa mengi sana ila yalisomeka kama ifuatavyo


“Salamu nyingi zikufikie mchaguliwa wetu ewe Aladini, bila s haka ndiwe unayesoma hiki kitabu kwa sasa. Kwani asingeweza yeyote kusoma ila wewe. Siri nzito ya familia yako na pango ili inapatikana humu. Tumekilinda kitabu hiki kwa miaka zaidi ya 85 sasa, na baada yako hakuna atayeweza kuisoma katu, kwani maandishi tutakuwa tumeshayachukuwa. Kumbuka siri za kwenye kitabu hiki hutamueleza yeyote. Tambua pia kuwa kurasa zijazo utatakiwa kufumba macho ndio uweze kusoma kitabu hiki. Hakikisha upo peke yako katika sehemu tulivu, mwisho ninakutakia mafanikio mema na binti mfalme”


Aladini sasa maswali mengi yakazidi kuzunguka kichwani mwake hasa pale alipotakiwa mafanikio mema yeye na binti Mfalme. Inamaana maisha ya Aladini yalishaandikw akuwa atamuoa binti Mfalme. Aladini alijaribu kufungua kurasa zijazo lakini hakuona maandishi. Alijaribu kukodoa macho kwa muda mrefu lakini wapi. Aladini sasa akawaza kuwa njia pekee ya kuendelea kusoma kitabu kile ni kufumba macho na kuwa katika sehemu nzuri na tulivu. Aladini akafikiri kuwa chumba cha stoo ambapo kulikuwa kukitoka mwangaza hajawahi kuingia, wala kuchunguza mwangaza ule ulitokea wapi. Aladini akawaza kule ndio sehemu pekee iliyo tulivu ambapo hatoweza kusumbuliwa katu.


Aladini akabeba kitabu chake na kuelekea kwenye chumba kile. Loo! Harufu nzuri ya marashi yaliyonukia vyema ilimkaribisha. Aladini alistaajabishwa kuona kuwa chumba kile kina vijiwe vinavyotoa mwangaza kama vya kule pangoni. Vijiwe vilikuwa kwenye kaboksi kadogo ka vioo. Chini ya kiboksi kulikuwa na karatasi iliyoandika “zawadi kwako Aladini mjukuu wangu”. Aladini alikuta kwenye chumba kile kuna kiti kikubwa kizuri sana. Kiti kilichofanana na cha mfalme. Aladini alikaa pale na kujiandaa tayari kwa kusoma ujumbe wa siri kwenye kitabu cha maajabu.