ALADINI KATIKA PANGO LA UTAJIRIMzee akampatia pete Aladini na akamueleza Aladini kuwa utaingia kwenye pango hili, usiguse chochote na elekea mbele zaidi. Utakutana na baraza kubwa sana, mbele yake kuna bostani la mauwa mazuri ya thamani. Katikati utakuta mshumaa. Uchukuwe kwa polepole uje nao.” kisha mzee akaendelea kuzungumza maneno na huku anazidi kukoleza moto kwa maneno yake, ardhi ikaadha utetemeka na Aladini akaanza kuingia. Mwanzoni Aladini alikuwa anaogopa lakini kadiri alivyozidi kuingia ndivyo uoga ulivyo mtoka. Kauli ya kutogusa chochote iliendelea kujirudia masikioni mwa Aladini.


Aladini aliendelea kungia katika pango lenyekiza. Baada ya kufika mbele alishangazwa sana kukuta kuna mwangaza asioujuwa nini chanzo chake. Baraza kubwa sana lililosakafiwa kwa madini ya kupendeza sana. Mchanganyika wa madini ulioonyesha sura nzuri sana. Barasa lilikuwa likiwaka kwa ubora wa mpangilio wa rangi zake. Aladini kijana mpumbavu wa mtaani leo yupo sehemu ya ajabu. Baraza liliwa zuri kwa sakafu na dari, ila hali hiyo haikumfanya Aladini asite kuendelea na safari yake.


Mbele kidogo Aladini akakuta bostani zuri sana. Bostani lwenye matnda na mauwa ya kupendeza. Aladini alishangwazwa sana kuona kuwa yale mauwa na matunda yalikuwa ni madini yanayong’aa na kuning’inia kwa mpangilio wa kupendeza. Madini ya Almasi kwenye mti wa mdizi, yamejipanga kwenye mkungu kama ni ndivi. Hali hii ilitengeneza sura ya ajabu sana na ya kupendeza. Midizi hii ya Almasi ilikuwa na rangi za kupishana zilizo nzuri. Haikuwacha kuwaka, na kuongeza mwangaza kwenye bustani hili.


Hali haikuwa kwenye midizi tu bali machungwa yalikuwa ni mawe ya dhahabu yenye kupangiliwa katika miduara yenye kumemeta na kutoa nuru ya kupendeza. Hakika Aladini alipatwa na jambo kubwa sana. Alitamani kuchuma tunda moja lamda aonje aone kama ni dhahabu kweli ana ni matunda tu. Ila kwa muonekano iliweza kuthibitisha kuwa ni dhahabu, kila tunda lilikuwa na rangi zke za kupendeza. Aladini alitamani siku moja aweze kuishi katika sehemu hii. Michungwa iliyojipanga vyema kwenue mistari ilifuatiwa na mauwa mazuri.


Mauwa haya nayo yalikuwa ni madini yenye rang tofauti tifauti za kupendeza. Aladini alishangazwa na kuona kuwa hata nyuki waliokuwa wakipepea kwenye ,auwa walikuwa ni dhahabu tupu. Aladini ilibidi aangalie vyema hapo akagunduwa kuwa mzinga wa nyuki uliopo jirani nao ni dhahabu tubu. Mwangaza mzuri ulikuwa ukiwaka katikati ya mzinga ule. Vitone vyenye rangi za kupendeza vilikuwa vikishuka kutoka kweye mzinga. Aladini masikini na njaa aliyo nayo alitamani kwenda kukinga ulimi. Ila sauti ya mzee ilijirisia “usiguse chochote”.


Hali haikuwa kwenye mauwa na nyuki pia Aladini alishuhudia kabati kubwa lililopo katikati ya bustani. Kabati ilo lilikuwa na bilauri nzuri na za kupendeza. Bilauri zenye maji yenye rangi ya fedha (silva). visahani vyenye rangi ya hudhurungi na mauwa ya kupendeza. Birika tati kubwa zenye rangi nzuri, maandishi ya kiarabu yaliyopangiliwa vyema yaliandikwa kwenye mabirika hayo. Aladini alishikwa na butwaa ana asijuwe nini afanye.


Aladini aliendelea mbele kidogo akakuta kuna meza lingine kubwa. Meza hilo lilikuwa na taa ya mchumaa. Taa hiyo ilikuwa ikiwaka bila kutoa moshi. Moto wake ulikuwa na rangi zenye kupishana na za kupendeza. Aladini aligunduwa kuwa mwanga wote unaopatikana humu ndani ulitokana na kamshumaa hako. Aladini akauendea mshumaa na kuunyakuwa kwa upole sana. Alipoushika mshumaa mwangaza wote pale ndani ukazima. Na rangi nzuri na ya kupendeza aliyokuwa akiiona ikageua kuwa kiza la kutisha.


Mwangaza mdogo uliotokana na pete yake ndio uliokuwa ukimsaidia. Aldini akaanza kutoka kwa araka na kwa umakini zaidi. Alipokaribia kutoka tu yule mzee akataka Aladini ampatie ule mshumaa kwa kuurusha. Aladini alikataa kwa sababu ya kuwa mpaka atoke salama ndipo ampatie. Jambo hili lilikuwa ni kinyume na alivyotarajia huyu mzee. Ukweli ni kuwa mzee alitaka amtumie Aladini kupata mshumaa kisha amuuwe humohumo. Mzee alivyoona hapa atakosa yote akaamuwa afunge pango ili aladini afio humohumo. Mzee bila ya kuchukuwa pete yake kwa Aladini alifunga pango kwa uchawi na kutimua zake. Na kumuacha Aladini kwenye pango lenye giza, akiwa na njaa kali. Aladini aliendelea kulia, kujuta na asiwe na njia ya kutoka nje.