image

Hadithi ya Kinyozi kaka wa kwanza

Hadithi ya Kinyozi kaka wa kwanza

HADITHI YA KAKA WA KWANZA WA KINYOZIKaka yangu alikuwa ni mshona charakani maarufu sana. Alipokuwa amekaa ofisii kwake siku moja akiwa anaangalia dirishani kwa bahati nzuri alimuona mwanamke mzuri sana. Mwanamke yule alikuwa akizugumza na mwenziwe. Kwa muda kadhaa kaka yangu alikuwa akimwangalia yule mwanamke. Kumbe na yule mwanamke alikuwa akimwangalia kaka kwa kujiiba. Basi yule mwanamke alipomaliza mazungumzo yake akamwangalia kaka kisha akamkonyeza na kupotelea mtaani. Muda wote ule kaka yangu hakweza kufanya kazi kwa ufanisi kwakumuwaza.


Bila ya kutambua mambo yalivo, kaka yangu alianza kumpenda yule mwanamke bilia kujuwa kumbe yule mwanamke alikuwa ni mke wa mtu. Siku ilofata kaka alipokuwa akishona alikuwa nmambo na akili yake yote ipo dirishani kuangalia kama atamwona yule mwanamke. Mara yule mwanamke akaja akiwa ameongozana na kijakazi chake. Kijakazi wake alikuwa ni binti wa makamo mwenye sura nzuri. Uzuri wake kamwe haukumfikia mwanmke yule.


Yule mwanamke alizogea jirani na kwa kaka anaposhona, kisha akawa anazungumza na baadhi ya wanawake wenzie. Wakati huo kaka aliacha kushona kabisa, kwa kumuangalia mwanamke yule. Wakati huo yule mwanamke alikuwa akimwangalia kaka kwa kujiiba huku akimkonyeza, na kumuoneshea ishara kwa vidole. Haukupita muda yule mwanamke akaondoka zake. Kaka alichanganyikiwa na kuacha kushona kabisa. Aliondoka na kweda nyumbani kulala ili apunguze mawazo.


Loo! Usingizi haukumpata hata kidogo, kwa mawazo na hisia aliendelea kuumia tu kitandani. Hatimaye usiku ukaingia na asubuhi ikang’ara tena. Kaka hakuweza kupata hata lepe la usingizi wala kugusa chakula. Mapema asubuhi kaka aliwahi kufungua ofisi na kuanza kusubiri wateja, angalau apate japo pesa ya kumuwezesha kupata chakula. Mteje wa kwanza kuja alikuwa ni yule kijakazi wa yule mwanamke. Kaka alijuwa kuwa kutakuwa na habari za furaha.


Kijakazi alikuja na vipande saba vya vitambaa kisha akamwambia kaka kuwa bosi wangu anataka umshonee magauni 7, na itakuwa vyema kama yakikamilika leo hii. Kaka alifunga ofisi ili kuzuia wateja wengine wasije. Hapo akajifungia na kuanza kushona. Nguvu ya mapenzi ilimteka vilivyo, bila kujali njaa aliyo nayo. Kwa kuwa kaka ni mtu wa maneno mengi akaanza kueleza hisia zake kwa huyu kijakazi ili azifikishe kwa mwanamke yule.


Kwa uwongo kijakazi akasema kuwa hata bosi wake yaani yule mwanamke ameshindwa kulala kwa kumuwaza yeye. Ukweli ni kuwa kulikuwa na agend ya siri kwa mwanamke huyu na kijakazi wake. Mpaka kufika jioni kaka alishamakiza kushona nguo zote na tayari akamkabidhi kijakazi. Kaka akaendelea eti ufungua ofisi na kusubiri kama kutakuwa na wateja. Loo aliambukia mtu mmoja aliyetaka kuwekewa kiraka kwenye kanzu yake. Kaka aliambukia pesa kidogo ya kununua matunda.


Ukweli ni kuwa yule mwanamke alimueleza mume wake kuwa kuna mshona nguo anamtaka. Hivyo mwanamke yule akapanga njama ili wamchune. Walipanga njama hii na mipango ilipotimia mwanmke yule akapanaga akutane na kaka mule ofisini kwake. Mbinu yao ni kuwa baada ya wawli kukutana wanataingia kundi la watu na kuja kumfumania. Matokeo yake ni kuchukuwa kila kilichopo ndani. Baada ya mipango kukamilika yote wakaagana na kundi la vijana mabarobaro na mipango ikatekelezwa.


Ilikuwa ni siku ya baada ya juwa kuzama, kaka aliagana na mwanamke yule kukutana pale ofisisni. Siku hiyo kaka alikwenda saluni kushevu nywele zake na kuchonga ndevu zake na kuzilinganisha sawasawia. Baada ya kusubiri kidogo, kaka akaanza kupata harufu ya manukato, kamwe hajapatapo kuivuta harufu hii kwa uzuri ulioje. Zura illiyo ya kuvutia ikaanza kuonekana ikichomoza kupitia mlango wa nyuma wa ofisi ya kaka kama walivyoagana. Kwa furaha kaka akaenda kumpokea kwa madaha na tayari kuazimia kufanya walilokusudia.


Haukupita muda ndipo mlango ukagongwa kwa nguvu, hata kabla ya kufungua mlango ukavunjwa. Loo ni kundi la vijana likidai kumfumania kaka na mke wa mtu. Kaka alijitetea lakini wapi, walimpiga sana maeneo mengi ya mwiili wake na wakampiga kichwani. Kaka akapoteza fahamu. Walichukuwa kila kilichop ofisini. Kisha wakamtia kaka kwenye kari la kuburuta kwa wanyama na kwenda kumtupa mbali sana. Kaka aliathiriaka kwenye kichwa na kupoteza kumbukumbu na akilli yake haiposawa kuanzia siku hiyo.


Basi nilitoka na kwenda kumtafuta kwa siri na kwenda kumchukuwa. Haya ndiyo yaliomkuta kaka yangu wa kwanza, kutokana na maneneo yake mengi na kutokuwa na weledi mwema wa dini. Sasa ngoja nikusimulie kilichomkuta kaka yangu wa pili ambaye ni kipofu na jinsi alivyoupata upofu katika mazingira ya utata.
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 326


Download our Apps
πŸ‘‰1 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰2 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰3 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Hadithi ya tunda la tufaha (epo)
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Utajiri wa baba na kifo chake
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Wagen wa Ajabu
UJIO WA WAGENI WA BARAKA. Soma Zaidi...

Nje ya jumba la kifahari la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

NJE YA JUMBA LA KIFAHARI JUMBA LA ALADINI
Soma Zaidi...

Hadithi ya Mshona nguo
Soma Zaidi...

ALADINI KATIKA PANGO LA UTAJIRI
Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi yeye mwenyew
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Mrembo mtoto wa tajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Aladini na binti wa mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu Soma Zaidi...

HADITHI YA KILEMA WA VIUNGO
HADITHI YA KILEMA, MTANASHATI ASIYE NA MKONO Basi tambu kuwa mimi ni Mtu wa Baghadad na ni mtoto wa aliyekuwa mfanyabishara mkubwa sana. Soma Zaidi...

Hadithi iliyosimuliwq na mlevi mbele ya sultani
Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi iliyosimuliwa na mlevi mbele ya sultan Soma Zaidi...