image

Aina za vyakula somo la 2: Vyakula vya protini

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu vyakula vya protini, faida zake na vyanzo vyake.

VYAKULA VYA PROTINI NA FAIDA ZA PROTINI MWILINI

Katika viinilishe muhimu mwili unavyohitaji amabavyo ni fati, protini, vitamini na wanga na mafuta mwili unahitaji protini kwa kiasi kikubwa kila siku. mwili unaweza kuibadili protini kuwa fati lakini si fati kuwa protini. hivyo protini ni kiinilishe muhimu zaidi ndani ya miili yetu. Katika makala hii nimekuandalia mambo muhimu unayopaswa kuyajuwa kuhusu protini na vyakula vya protini, faida zake na hasara zake. Madhara ya kiafya yanayohusiana na protini pamoja na kuyaepuka madhara hayo. Makala hii imeandaliwa wa kufuata nukuu na makala kutoka kwa wataalamu wa Afya na lishe.

 

MUKTASARI KUHUSU PROTINI.

Protini ni chembechembe zinazotokea kwa njia ya asili (bila ya kutengenezwa) na zimetokana na asidi za amono (amino acid) zilizounganishwa kwa kutupia bondi za peptide. Neno protini asili yake ni lugha ya Kigiriki ”proteios” likiwa na maana ya kuwa ni kitu kinachopewa nafasi ya kwanza. Yaani protini ni viinilishe “nutrients” ambazo ni muhimu sana mwilini kuliko viinilishe vingine. Neno hili limeanzaka kutumiwa karne ya 19 mwaka 1838 na Mkemia kutoka Swedih Jöns Jacob Berzelius.



Protini huweza kutofautiana namna zilivyo kutoka kiumbe kimoja na chingine, pia protini huweza kutofautiana kutoka kiungo kimoja kwenda kingine. Kwa mfano protini za kwenye macho ni tofauti na zile za kwenye moyo, ini na figo. Kila kiumbe hai kina protini, na pia protini huhusika katika michakato tata kwenye miili ya viumbe hai, kwa mfano protini huhusika katika kutengeneza antibodies ambazo hutengeneza kinga na kupambana na maradhi na wadudu shambulizi kama bakteria na virusi. Protini hutengeneza enxymes ambazo ndizo hutumika katika kumeng’enya chakula. Pia protini hutengeneza homoni (hormones)



Baada ya kukila chakula chenye protini chakula kinaanza kumengenywa kinapofika kwenye tumbo na utumbo, kisha hufyonzwa kwenye utumbo mdogo na kuingia kwenye mirija ya damu. Pindi chembechembe za protini zinapoingia kwenye damu, damu huanza kusafirisha protini kwenda maeneo mbalimbali ya mwili yanayohitajia protini. Huko protini zitaingia kwenye seli za mwili. Ndani ya seli mchakato kwa kuvunjwa vunjwa protini ili kutumiwa zaidi hufanyika. Ndani ya seli mchakato huu jhufanyka kwenye sehemu inayotambulika kitaalamu kama ribosomes



Miili ya wanyama haina uwezo wa kuhifadhi protini kwa matumizi ya baadaye. Hivyo kama mtu atakula protini nyingi, mwili utaibadili protini kuwa fati na baadaye kutumika kutengeneza nishati ndani ya mwili. Na endapo mtu hataweza kupata protini za kutosha mwili utaanda kuangalia maeneo yenye protini ndingi kama misuli, kisha mwili utaanza kuvunja protini iliyomo mule na kuipeleka maeneo mengine na hapa mtua ataanza kukonda na kupoteza nyama na hatimaye kufariki kama hatapata chakula chenye protini.




VYAKULA VYENYE PROTINI

Tunaweza kupata protini kwenye mimea jamii ya mikunde kama kunde na maharagwe. Pia kiasi kikubwa cha protini tunaweza kukipata kwa kula mayai, nyama, samaki, dagaa na maziwa. Pia tunaweza kupata protini kwa kula nafaka kama mchele na nafaka zingine. Ulaji wa mboga za majani unaweza pia kutupatia protini kwa kiasi kidogo. Wadudu kama kukbikukbi, senene na wengineo pia wanaweza kutupatia protini.



Kwa kifupi vyakula vinavyotupatia protini ni pamoja na :-

  1. Samaki; samaki ni chanzo kizuri cha protini. Samaki wenye mafuta kama salmon ni vyanzo vyema zaidi vya protini. Ulaji wa samaki umekuwa ni chanzo kizuri cha protini hasa kwa wakazi wa maeneo ya baharini na maeneo ya pwani ama mitoni, mabwawa na maziwa. Tunaposema samaki hapa wanaingia mpaka dagaa, kaa, kaji, kamongo, perege, mikunga, papa na samaki wengine. Pia ulaji wa samaki ni muhimu kwa afya ya ubongo, kukinga mwili dhidi ya maradhi mbalimbali, chanzo cha madini ya chumvi na fati


  1. Mayai; mayai ni katika vyanzo vikubwa vya protini. Karibia watu wengi hujipatia protini kwa kula mayai. Unaweza kula yai likiwa limekaangwa, chemshwa ana la kuchoma. Pia unaweza kula yai bichi kama wafanyavyo baadhi ya watu. Ulaji wowote kati ya niliotaja unaweza kukupatia protini. Ila hakikisha kama umelikaanga ama kulichoma halikauki sana likawa kama chapati iliyokauka, upishi huu unaweza kuathiri virutubisho.


  1. Maziwa; maziwa ni katika vyanzo vikuu vya protini kwa binadamu na wanyama. Maziwa ya mama ni chanzo kipekee kilicho salama zaidi kwa mtoto mchanga kuliko hata ya ng’ombe. Tofauti na kutupatia protini maziwa pia ni chanzo cha vitamini na fati. Maziwa ni katika vyakula vilivyokusanya viinilishe vyote muhimu. Ni vyema kuyachemshha maziwa kabla ya kuyanywa ili kuepuka baaadhi ya matatizo ya kiafya.


  1. 4.Nyama; tunaweza kupata protini kwa kiasi kikubwa kwa kula nyama. Nyama ni katika vyanzo vizuri vya protini. Inaweza kuwa nyama nyekundu ama nyama nyeupe. Nyama nyeupe tunaweza kuzipata kwa kula kuku, baadhi ya samaki, kaa. Nyama nyekundu tunaweza kupata kwa kula mbuzi, kondoo na karibia wanyama wengi. Nyama pia ni chanzo kizuri cha fati mwilini. Ulaji wa nyama unaweza kuleta athari za protini kwa muda mchache sana.


  1. Mimea aina ya kunde na nafaka; mimea jamii ya kunde hii ni mimea ambayo inatambaa kama kunnde na maharagwe na mimea jamii hii. Mimea hii inatambulika kuwa na kiasi kikubwa cha protini. Watu wenye kipato cha chini mimea hii ni chanzo chao cha msingi cha kupata protini. Maharagwe yapo katika aina nyingi yapo ya soya na aina mbalimbali. Ulaji wa aina zote hizi unaweza kutupatia protini.


  1. Mboga za majani. Kwa kiwango kilicho kidogo tunaweza kupata protini kwa kula mboga za majani. Mboga za majani oekee hazitoshelezi kutupatia kiwango cha protini kinachohitajika. Kwa wale ambao hawali chama (vegetarian) wapo ambao hawali nyama lakini wanakula mayai na maziwa hawa wanaweza kujipati protini kwenye mayai na maziwa. Lakini kwa wale ambao hawali nyama, maziwa wala mayai watahitajika kupata vyamzo vingine mbadala vya protini yaani watumie protini za kutengeneza japo miongoni mwazo zipia mbazo zinatengenezwa kwa wanyama.


  1. Vyanzo vingune: tofauti na vyanzo vya protini nilivyotaja hapo juu lakini pia kuna vyanzo vingine kama ulaji wa senene na kumbikumbi na wanaofanana. Kuna baadhi ya jamii zinakula senene hasa jamii zinazopatikana maeneo ya kagera. Kwao senen ni chanzo kizuri sana cha protini. Kumbikumbi nao hupatikana maeneo mengi na jamii nyingi zinatumia chakula hiki.


KAZI ZAPROTINI NA VYAKULA VYA PROTINI MWILINI

Kwa kuwa sasa tunajua vyanzo vya protini sana ni vyemna tukaziona kazi za protini ndani ya miili yetu. Waandishi wengi wamekuwa wakiandika kazi za protini, na kuziorodhesha katika kazinyingi. Lakini katika makala hii itakuletea kazi zilizo kuu za protini.

Kazi za protini mwilini:-

  1. Kujenga mwili;
  2. Kupona kwa vidonda na majeraha
  3. Kutengeneza antibody (kinga za mwili)
  4. Kutengeneza hemoglobin (chembechembe zaseli nyekundu za damu)
  5. Kutengeneza enzymes zinatumika katika kumeng;enya chakula
  6. Kutengeneza homoni
  7. Kuthibiti kichakati na shughuli za ndani ya seli
  8. Huhusika katika kutengeneza tishu (nyama na misuli) ndani ya mwili
  9. Nywele, kope, nyusi, vinyweleo na kucha hutokana na rotini


  1. Kujenga mwili; protini huhusika katika kujenga mwili, na uponaji wa vidonda na majeraha. Mwili kukua vyema na kujengenka vyema protini inahitajika katika kuhakikisha hili linafanyika. Ulaji wa protini ya kutosheleza uanaweza kuufanya mwili uwe katika umbo jema na lililojengeka vyema. Endapo mwili utapata majeraha protini itahusika katika kuziba majeraha na vidonda katika eneo husika. Kama wanavyosema mwili haujengwi kwa matofali, lakini unaweza kusema kuwa protini ndio tofali la kuujenga mwili.


  1. Hutumika katika kutengeneza antibodies; hizi ni chembechembe za protini zinazopatikana kwenye damu. Chembechembe hini ni muhiu sana katika mfumo wa kinga. Hizi huweza kuulinda mwili dhidi ya mashambulizi ya maradhi na watutu waletao maradhi. Protini inahitajika ili kutengenezwa kwa chembechembe hizi kufanyike. Hivyo unaweza kusema kuwa protini ni muhumu katika mfumo wa kinga mwilini.


  1. Utengenezwaji wa hemoglobin; hemoglobin ni aina za protini, na hii huhusika katika usafirishaji wa hewa ya oksijen na kabondioxide ndani ya miili yetu. Hemoglobin ni chembechembe ambazo ninakazi ya kuchukuwa hewa ya okijeni baada ya mtu kuivuta na kuipeleka kwenye moyp ambapo husambazwa, kwenda maeneo mengine. Kisha hemoglobinhukusanya hewa chafu nyenye kabondaiyokasaidi na kuipeleka kwenye mapafu. Ijapokuwa hemoglobin ni chembehembe za protini lakini pia imetokana na madini ya chuma. Upungufu wa madini ya chuma unaweza kuathiri mfumo wa damu.


  1. Utangenezwaji wa enzymes. Hizi ni chembechembe zinazotambulika kama biological catalyst, yaani ni vichochezi vya kuchochoea michakato ya kikemikali iendelee kufanyika ndani ya miili etu. Enzymes huchukuwa nafasi kubwa katika kumenge’enya chakula katika hutau zote na katika maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Enzmes zinaweza kupatikana mdomoni, tumboni na katika utumbo mdogo. Umeng’enywaji wa chakula ili tupate vurutubisho enzymes hutumika.


  1. Utengenezwaji wa homoni; ili mwili uweze kutengeneza homoni unahitaji protini. Homoni ni chembechembe za kikemikali ambazo husaidia katika kufanya kazi nyingi na tata mwilini. Utengenezwaji wa mayai kwa wanawake na mbegu za uzazi kwa wanaume unahitaji homon. Urekebishwaji wa sukari pia unahitaji homoni. Ilijasho liweze kutoka homoni huhusika katika kurekebisha joto mwilini. Homoni zinakazi nyingi sana mwilini. Lakini jambo la msingi kufahamu hapa ni kuwa homoni hutengenezwa kwa protini.


  1. Utengenezwaji wa nywele na vinyweleo na kope pia hutokana na protini. Kama nilivyotangulia kukueleza kuwa protini ni matofali ya kuijenga miili yetu na hii ndio maana yake. Hata nywele zetu kama hatutapata protini ya kutosha katu huwezi kuna na nywele nzuru, na zenye afya ya kutosheleza. Nywele zinaweza kuwa katika hali isiyo ya kawiada ka hutapata protini ya kutosha.


UPUNGUFU WA VYAKULA VYA PROTINI

Kama tulizoona faida za protini ndani ya miili yetu basi pia itambulike kuwa kuna hasara kubwa za kiafya endapo mtu atashindwa kupata protini za kutosheleza ndani ya miili yetu. Hapo chini nitakuorodheshea tu baadhi ya madhara ya kukosa protini ya kutosha:

  1. Kudumaa na ukuaji hafifu wa mtoto
  2. Kypata kiriba tumbo
  3. Kupata kwashiakoo
  4. Misuli na nyama kustokijazia vya kutosha
  5. Kukosa nguvu ya kutoka kufanya kazi
  6. Kukonda na kudhoofu


ULAJI WA PROTINI KUPITILIZA

Kwa upande wa pili ulaji wa protini nje ya kiwango unaweza kuleta athari hasi katika afya ya mlaji. Zifuatazo ni madhara ya kula vyakula vya protini kupitiliza

  1. Kuongezeka kwa uzito mwilini
  2. Kupata tatizo la kukosa chookuharisha
  3. Kupungua kwa maji mwilini
  4. Kupata matatizo ya moyo
  5. Kuathirika kwa fogo
  6. Hatari ya kutengengezwa kwa seli za saratani mwilini





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-07-21 13:31:35 Topic: Aina za vyakula Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 142


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Aina za vyakula somo la 4: Vyakla vya wanga yaani carbohydrates
Katika post hii utakwenda kujifunza kuhusu vyakula vya wanga, kazi zake, faida zake na upungufu wake. Soma Zaidi...

Aina za vyakula somo la 61: Faida za kula tikiti
Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula tikiti Soma Zaidi...

Aina za vyakula somo la 35: Faida za kula mbaazi
Katika somo hili utakwend akujifunza faida za kiafya za kula mbaazi Soma Zaidi...

Maina za vyakula somo la 39: Faida za kula maini
Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula mainai Soma Zaidi...

Aina za vyakula somo la 15: Faida za kunywa chai yenyemajani ya chai
Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kunywa chai. Hapa tunazungumzia chai yenye majani ya chai Soma Zaidi...

Aina za vyakula somo la 51: Faida za kula papai
Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula papai Soma Zaidi...

Aina za vyakula somo la 30: Faida za kula kungumanga
Katika somo hili utakwenda kijifunza kuhusu faida za kiafya za lula kungumanga Soma Zaidi...

Aina za vyakula somo 21: Faida za kula kabichi
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu faida za kiafya za kula kabichi Soma Zaidi...

Aina za vyakula somo la 26: Faida za kula kitunguu saumu - garlic
Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula kitunguu ssaumu - garlic Soma Zaidi...

Aina za vyakula somo la 34: Faida za kula kunde
Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula kunde Soma Zaidi...

Aina za vyakula somo la 41: Faida za kunywa maziwa
Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kutumia maziwa kama kunywa ama kula bidhaa zake. Soma Zaidi...

Aina za vyakula somo la 60: Faida za kula tende
Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula tende Soma Zaidi...