Kusimamisha Swala na kuamrisha mema
Swala iliyosimamishwa vilivyo ndiyo nyenzo kuu ya kumtakasa Muislamu na kumpa sifa zinazomuwezesha kustahiki kufanya kazi takatifu ya kusimamisha Uislamu katika jamii.
(f)Kusimamisha Swala
Swala iliyosimamishwa vilivyo ndiyo nyenzo kuu ya kumtakasa Muislamu na kumpa sifa zinazomuwezesha kustahiki kufanya kazi takatifu ya kusimamisha Uislamu katika jamii. Swala ikisimamishwa vilivyo humuwezesha mja kumcha Allah (s.w) ipasavyo katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na pia ni msingi wa kumpelekea mja kusimamisha Uislamu katika jamii.
(g)Kuamrisha mema na kukataza mabaya na kusubiri juu yale yatakayokusibu
Kuamrisha mema na kukataza maovu ni masuala yanayohitaji mamlaka na nguvu (authority and power). Hata hivyo kuwa na mamlaka na nguvu sio lazima ianzie kileleni katika ngazi ya Dola, bali mamlaka na nguvu ya kuamrisha mema na kukataza mabaya huanzia kwa mtu binafsi, kisha kwa familia yake kisha kwa ndugu na jamaa zake wa karibu. Kuamrisha mema na kukataza maovu ni wajibu kwa waumini wote (Qur'an 3:104, 3:110, 8:25, n.k).
Kuamrisha mema na kukataza maovu ni suala la mapambano hata katika ngazi ya mtu binafsi na katika ngazi ya familia. Ni shughuli inayohitajia kuwa na subira ya hali ya juu. Subira ina maana pana ikiwa ni pamoja na:
1.Wewe mwenye kubakia na msimamo wa kufanya mema na kujiepusha na maovu
2.Kuwahimiza na kuendelea kuwashupalia kufanya mema
na kuacha maovu wale ambao unamamlaka juu yao.
3.Kuwa tayari kulaumiwa na yeyote atakayelaumu.
4.Kuwa tayari kukabiliana na magumu yoyote
yata kayo kufika.
5.Kutotarajia kupata matunda ya haraka haraka kutokana na kazi ya kuamrisha mema na kukataza mabaya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 web hosting 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Mifumo ya benki ya kiislamu.
Hapa utajifunza njia ambazo nenk ya kiislamu hutumia ili kujiendesha
Soma Zaidi...Ni kwa nini riba imeharamishwa kwenye Uislamu
Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake.
Soma Zaidi...Je ni kwa nini lengo la finga halifikiwi kwa wafungaji
Lengo la funga ni kuwa mchamungu sasa ni kwa nini wafungaji hawalifikii lengo hili na kuwa wachamungu.
Soma Zaidi...Jinsi ya kuswali swala vitani
Post hii itakufundisha taratibu zinazofanyika ilibkuswalibukiwa vitani.
Soma Zaidi...