Shufaa

Shufaa

Shufaa




Ni muhimu baada ya mada hii ya 'maana ya kuamini siku ya mwisho', tuiangalie shufaa kwa mtazamo wa Kiislamu. Ni muhimu kwa sababu imetokea kwa baadhi ya watu wanaoitakidi kuwa ni waumini, kwa kupenda kwao njia ya mkato, wanaacha kutekeleza wajibu wao wa kuishi kama anavyotakiwa kuishi muumini wa kweli na badala yake wanaendesha maisha yao ya kila siku kama wafanyavyo makafiri na wakati huo huo wanamatumaini makubwa ya kupata neema za peponi kwa njia ya shufaa.


Maana ya Shufaa:
Kwa mujibu wa Qur-an na Sunnah shufaa ni uombezi wa watu wema kuwaombea msamaha watu watakaokuwa katika hali ya udhalili katika maisha ya akhera ili Allah (s.w) awatoe katika hali hiyo ya udhalili na kuwapeleka katika hali bora. Patakuwa na shufaa ya:



(i)Kuwaombea watu hisabu nyepesi na wachukue muda mfupi katika hisabu.



(ii)Kuwaombea waja wema waingie peponi moja kwa moja bila ya hisabu ili kuepukana na mazito ya sikuya Hisabu.
Kuwaombea waingizwe peponi wale ambao mizani ya mema na mabaya yao imekuwa sawa sawa. Kuwaombea watu watolewe kutoka motoni na waingizwe peponi.
Kuwaombea watu wema wapandishwe daraja katika Pepo; watolewe katika pepo ya daraja ya chini na kupandishwa katika pepo ya dara ya juu.


Masharti ya Shufaa:



Pamoja na shufaa kuwepo katika siku hiyo ya malipo, Uislamu hauichukulii shufaa kwa mtazamo wa kikristo au mtazamo wa dini nyingine, ambapo hao watakaoshufaia wameitakidiwa kuwa watakuwa na uwezo wa kuwaokoa watu na adhabu ya Allah (s.w) na kuwaingiza Peponi. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Shufaa haitafanyika ila kwa idhini ya Allah (s.w). Ni lazima kwanza Allah (s.w) aridhike kuwa mkosaji anastahiki ndio atoe ruhusa ya shufaa kwa yule aliyemridhia na kisha baada ya msamaha huo kuombwa ni khiari yake Allah (s.w) kusamehe au kutosamehe. Msimamo huu juu ya shufaa umewekwa bayana katika Qur-an:' Nani huyo awezaye kushufaia mbele yake (Allah) bila ya idhini yake? ' (2:255)'Na wako Malaika wangapi mbingu ni, ambao uombezi w ao hautafaa chochote isipokuw a baada ya Mw enyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia.'
(53:26).
Pia rejea Qur-an (6:51, 10:3, 19:87, 39:44, 43:86na 74:48).


Kwa ujumla shufaa ni rehema ya Allah (s.w) atakayo ikunjua kwa wale watakaostahiki kuipata kutokana na jitihada zao za kutenda mema hapa duniani kwa ajili ya Allah (s.w) japo wakati mwingine wanaweza kutekeleza na kumuasi. Muumini wa kweli wa siku ya malipo atajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kutenda mema kwa ajili ya Allah (s.w), kujiepusha na maovu kwa kuchelea ghadhabu za Allah (s.w) na kuomba maghfira kwa haraka haraka kila atakapomkosea Allah (s.w) au kumkosea mwanaadamu mwenziwe. Udhaifu utakaompitia muumini huyu, Allah (s.w) atamsamehe kwa njia mbali mbali na hii ya kuombewa shufaa ikiwa ni mojawapo.
Nani watakao shufaia?
Watakaoombea waumini shufaa kama tulivyoona katika aya zilizotangulia ni pamoja na Malaika, Mitume, watu wema ikiwa ni pamoja na watoto wachanga na amali njema kama Swala, Swaumu, Qur-an, n.k. Wa kwanza kushufai katika siku ya kutisha, siku ya Kiyama atakuwa ni Mtume (s.a.w) kama tunavyofahamishwa katika hadith nyingi.
Baada ya Hukumu kupita, Mitume watawaombea shufaa miongoni mwa wafuasi wao ambao watakuwa wamehukumiwa kuingia motoni. Pia waumini watakoingia Peponi watapewa fursa ya kuwaombea shufaa waumini wenzao ambao kwa njia moja au nyingine walifeli mtihani na ikabidi waingie motoni. Hebu tuzingatie hadith zifuatazo:
Uthman bin Affan amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) kasema: 'Watatu watashufaia katika siku ya Kiyama: Mitume, kisha wanachuoni, kisha waliokufa mashahidi'. (Ibn Majah).
Abu Sayyid amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Kati ya Umma wangu patakuwa na watakaoshufaia makundi mengi ya watu kati yao kuna watakaoomba shufaa kwa kabila (moja) na kati yao kuna wakaoomba shufaa ya mtu mmoja, mpaka wangie Peponi. '. (Tirmidh).


Anas kasema: Wakazi wa motoni watapangwa katika mistari, kisha mmoja wa wakazi wa Peponi atawapitia. Mmoja katika wao atasema: Ewe Fulani, hunitambui? Nilikuwa yule niliyekupa maji. Na wengine watasema: Tulikuwa ni wale tuliyekupa maji ya kutawadhia. Hivyo atamuombea (kila mmoja) kwa Allah (s.w) na kumwingiza peponi. (Ibn Majah).
Abu Sayyed al-Khudry amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: 'Kila mwenye imani uzito wa hardali (atom weight) atatolewa motoni'. (Tirmidh).
Jambo la kuzingatia na kusisitiza sana hapa ni kwamba shufaa haitaombwa kwa misingi ya udugu, ukoo, utaifa au kwa misingi ya upendeleo wa aina yeyote, bali itajuzu tu kwa wale Allah (s.w) atakaoridhia waombewe na akatoa idhini juu ya kuombewa kwao. Kwa maana nyingine shufaa itategemeana na matendo mema ya mtu aliyoyatanguliza.


Mitume watashufaia wafuasi wao waliowafuata kwa uadilifu, watu wema watawashufaia jamaa zao, jirani zao, rafiki zao, wananchi wenzao, waliowatendea wema kwa ajili ya wema wao, watoto wadogo wawashufaia wazazi wao waliokuwa wema kwao, n.k. Shufaa hizi zitapata ruhusa na kukubaliwa tu iwapo wale wanaoombewa walikuwa waumini ambao kwa njia moja au nyingine waliteleza na kumuasi Allah na wakastahiki kuwa katika hali hiyo ya dhiki. Kwa kafiri au mushriki shufaa ya aina yeyote haitakubaliwa hata kama shufaa hiyo itaombwa na Mitume au vipenzi vya Allah (s.w).


katika Qu-an tumeona kukataliwa kwa maombi ya Nabii Muhu juu ya mwanawe aliyestahiki kuangamizwa pamoja na walioangamizwa kwa ukafiri wao:
'Ikiwa hiyo (jahazi) inakwenda nao katika mawimbi kama milima. Na Nuhu akamwita mwanawe aliyekuwa mbali (kakataa kuingia jahazini): 'Ewe mwanangu! Panda pamoja nasi wala usiwe pamoja na makafiri'. Akasema (huyo mtoto): 'Nitaukimbilia mlima utakaonilinda na maji'. Akasema (Nuhu): 'Hakuna leo kulindwa na amri ya Mwenyezi Mungu isipokuwa yule atakayemrehemu (Mwenyezi Mungu)'. Mara mawimbi yakaingia baina yao na akawa miongoni mwa w aliogharikishw a. Na (baada ya kuangamizw a w ote na vyote alivyotaka Mw enyezi Mungu viangam ie) ikas em w a:P 'Ewe ardhi: Meza maji yako.


Na ewe Mingu jizuie (na kuteremsha mvua)'. Basi maji yakadidimia chini na amri ikapitishwa (ya kuangamizwa makafiri), na (jahazi) likasimama juu ya (jabali linaloitwa) Judi. Na ikasemwa likasimama juu ya (jabali linaloitwa) Judi. Na ikasemwa 'Wameangamiliziwa mbali madhalimu'. Na Nuhu alimwomba Mola wake (alipomwona


mwanawe anaangamia) akasema: 'Ewe Mola wangu! Mwanangu ni katika watu wa nyumbani kwangu (mbona anaangamia)? Na hakika ahadi yako ni haki; nawe ni Mwenye haki kuliko mahakimu (wote): Akasema (Mw enyezi Mungu): 'Ewe Nuhu! Huyu si miongoni mwa watu wako. Yeye ni (mwenye) mwendo usiokuwa mzuri. Basi usiniombe ambayo huyajui Mimi nakunasihi usiwe miongoni mwa wajinga.'
(11:42-47)
Pia tunafahamishwa katika Hadith jinsi Nabii Ibrahim (a.s) atakavyokataliwa maombi yake kwa Allah (s.w) kumuombea baba yake Azar aepushwe na adhabu kali waliyoandaliwa washirikina:
Abu Hurairah amesimulia kutoka kwa Mtume (s.a.w) aliyesema: Ibrahim atakutana na baba yake. Azar katika siku ya Kiyama. Uso wa Azar utakuwa umefunikwa na lami na mavumbi. Ibrahimu atamsemesha: 'Sikukuambia kuwa usiache kunitii (usinikadhibishe)?' Baba yake atamjibu: 'Leo sitaaacha kukutii'. Ibrahim ataomba: Ewe Mola! Hakika umeniahidi kuwa hutanifedhehesha siku watakapofufuliwa watu. Sasa ni fedheha gani zaidi kuliko kuwekwa mbali na baba yangu?' Allah (s.w) atasema: Hakika Nimeiharamisha Pepo kwa Washirikina. Kisha itasemwa kwa Ibrahimu: Angalia ni kitu gani kilichoko miguuni mwako. Ataangalia, hamaki: shingo kubwa itatokeza. Ataburuzwa (Azar) kwa miguu yake na kutupiwa motoni.'. (Bukhari)
Vile vile tukirejea tena Qur-an tunaona jinsi Mtume (s.a.w) alivyokataliwa maombi yake alipowaombea wanafiki:



(Ewe Mtume: Waombee msamaha (hao wanafiki) au usiwaom bee, (yote sawa sawa). Hata ukiwaombea msamaha mara sabini, Mwenyezi Mungu hatawasamehe. Hayo ni kwa sababu ya kuwa wao wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu wavunjao amri (zake). (9:80)
Hivyo kutokana na maelezo haya, tumeona kuwa shufaa itakuwepo, lakini itawanufaisha tu walioamini na sio makafiri, washirikina na wanafiki. Jambo muhimu kwa Muislamu ni kujitakasa kwa kutenda mema na kuacha maovu na kuwa mwepesi na kurejea kwa Allah (s.w) kwa toba baada ya Kumkosea au kuhisi Kumkosea. Si vyema kwa Muislamu kuzembea katika kufanya mema na kuendelea kufanya maovu kwa matarajio ya kupata shufaa ya Mtume (s.a.w) au ya yeyote yule amtegemeaye kuwa atamshufaia. Kuna mambo mawili muhimu ya kuzingatia kwa wale wanaoacha kujitahidi kutekeleza wajibu wao kama anavyoridhia Allah (s.w) na badala yake wakaishi watakavyo kwa tegemeo la kupata uokovu kutokana na shufaa:
Kwanza kutegemea shufaa ni jambo la kubahatisha mno, kwani si jambo lililoko kwenye mamlaka ya yeyote isipokuwa Allah (s.w) pekee.
Pili, shufaa nyingine itakuja baada ya mja kuadhibiwa kwanza, adhabu ambayo ni kali mno, inayodhalilisha au kuhilikisha hata kama mja atakaa humo muda mfupi sana. Ni vyema tuzingatie sana aya ifuatayo:


Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu Kwake (Allah). (89:25)
Hivyo, jambo la busara ni Muislamu kujitahidi kuepukana na adhabu kali ya Allah (s.w) aliyowaandalia watu maasi na badala yake ayaendee kwa juhudi kubwa iliyoambatana na subira na yale yatakayompelekea kustahiki kuingizwa peponi moja kwa moja.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 646


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga. Soma Zaidi...

Hadithi inayotaja nguzo tano za uislamu
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ': ' ' ' '?... Soma Zaidi...

Adabu ya kuingia katika nyumba za watu
Enyi mlioamini! Soma Zaidi...

yaliyomo: HUKUMU YA MIM SAKINA, NUN SAKINA, MADA, WAQFU, QALAQALA, TAFKHIM NA TARQIQ, USOMAJI WA QURAN
DARSA ZA TAJWID YALIYOMOSURA YA 01 . Soma Zaidi...

MTAZAMO NA HUKUMU YA KUPANGA UZAZI WA MPANGO KWENYE UISLAMU
Atika uislamu swala la kupanga uzazi linaruhusiwa endapo kutakuwa na sababu maalumu za kisheria. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII HUD(A.S) NA WATU WA 'AD
Baada ya Nuhu(a. Soma Zaidi...

Mapambano ya waislamu dhidi ya maadui wa kiyahudi madina
Mayahud Mwanzoni Mayahud walipoona kuwa Waislamu wanafunga siku ya Ashura pamoja nao na wanaelekea Qibla cha Baitul- Muqaddas pamoja nao hawakuonyesha chuki ya dhahiri dhidi ya Mtume(s. Soma Zaidi...

Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake
Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu. Soma Zaidi...

Sifa za Allah Mwenyezi Mungu
Soma Zaidi...

familia
Soma Zaidi...

Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira ya jamii zao
Takriban Mitume wote walitokea katika jamii zilizozama katika ujahili, lakini kamwe ujumbe wao haukuathiriwa na mitazamo ya ujahili kwa ujumla, walahawakuingizautamaduni wa kijahili katika dini ya Allah (s. Soma Zaidi...

AMRI YA KUMFUATA MTUME (s.a.w9)
Amri ya Kumfuata Mtume (s. Soma Zaidi...