picha

ENYI WAJA WANGU NIMEIKATAZA NAFSI YANGU DHULMA

ENYI WAJA WANGU NIMEIKATAZA NAFSI YANGU DHULMA

الحديث الرابع والعشرون

"يا عبادي إني حرمت الظلم على نفسي"

عن أبي ذَرٍّ الْغِفاريِّ رضي الله عنه، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم فيما يَرْويهِ عن رَبِّهِ عَزَّ وجَلَّ أَنَّهُ قال: 

(( يا عِبادي إنِّي حَرَّمْتُ الظُلْمَ على نَفْسِي وَ جعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّماً فلا تَظَالَمُوا.

يا عِبادي كُلُّكُمْ ضالٌّ إلا مَنْ هَدَيْتُهُ، فاسْتَهدُوني أهْدِكُمْ.

يا عِبادِي كُلُّكُمْ جائعٌ إلا مَنْ أطْعَمْتُهُ، فاسْتَطْعِمُوني أُطْعِمْكُم.

يا عِبادِي كُلُّكُمْ عَارٍ إلا مَنْ كَسَوْتُهُ، فاسْتكْسوني أَكسُكُم.

يا عِبادِي إِنَّكُمْ تُخْطِئُونَ بالليْلِ والنَّهارِ، وأنا أَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَميعاً، فاسْتَغْفِرُوني أُغْفِر لكُمْ.

يا عِبادِي إِنَّكُمْ لنْ تبْلغُوا ضُرِّي فتَضُرُّوني، ولن تبْلُغُوا نفْعي فَتَنْفعُوني.

يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجِنَّكُمْ كانُوا عَلَى أَتْقَى قَلْبِ رَجُلٍ واحدٍ مِنْكُمْ ما زادَ ذلك في مُلْكي شَيئاً.

يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجِنَّكُمْ كانُوا عَلَى أَفْجَرِ قَلْبِ رَجُلٍ وَاحدٍ مِنْكُمْ ما نَقَصَ ذَلِكَ مِنْ مُلْكي شَيئاً.

يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجنَّكُمْ قاموا في صَعِيدٍ وَاحِدٍ، فَسَأَلُوني، فأَعْطَيْتُ كلَّ واحدٍ مَسْأَلَتَهُ ما نَقَصَ ذلك مِمَّا عِنْدِي إلا كما يَنْقُصُ الْمِخْيَطُ إذا أُدْخِلَ الْبَحْرَ.

يا عِبادِي إنَّما هي أعمَالُكُمْ أُحْصِيها لَكُمْ ثُمَّ أُوَفِّيكُمْ إيَّاها، فَمَنْ وَجَدَ خيْراً فَلْيَحْمَدِ اللهَ، ومَنْ وَجَدَ غَيْرَ ذلك فَلا يَلومَنَّ إلا نَفْسَه))

 رَوَاهُ مُسْلِمٌ   


 ENYI WAJA WANGU NIMEIKATAZA NAFSI YANGU DHULMA

 

Kutoka kwa Abu Dharr Al-Ghifariy رضي الله عنه   naye kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم  akisimulia yale aliyopokea kutoka kwa  Bwana wake   عَزَّ وَجَلَّ   ni:

Enyi waja Wangu, Nimeikataza nafsi Yangu dhulma na Nimeiharamisha kwenu (hiyo dhulma), kwa hivyo msidhulumiane.

Enyi waja Wangu, nyote mumepotea isipokuwa wale Niliowaongoza, kwa hivyo tafuteni muongozo kutoka Kwangu Nitakuongozeni. 

Enyi waja Wangu nyote mna njaa isipokuwa wale Niliowalisha, kwa hivyo tafuteni chakula kutoka Kwangu na Nitakulisheni.

Enyi waja Wangu, nyote muko uchi isipokuwa wale niliowavika nguo, kwa hivyo tafuteni vazi kutoka Kwangu nitakuvisheni.

Enyi waja Wangu, mnafanya  makosa usiku na mchana, na ninasamehe dhambi zote, kwa hivyo tafuteni msamaha kutoka Kwangu nitakusameheni.

Enyi waja Wangu hamuwezi kunidhuru Mimi wala kuninufaisha.  

Enyi waja Wangu, ingekuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mcha Mungu kama moyo wa mcha Mungu yeyote katika nyinyi, haitaongeza  chochote katika ufalme Wangu.

Enyi waja Wangu, angelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mbaya kama moyo mbaya wa mtu miongoni mwenu (mtu mbaya kupita kiasi) haitonipunguzia chochote katika ufalme Wangu.

Enyi  waja Wangu ingelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi mukasimama pahala pamoja na mkaniomba, na nikawapa kila mmoja alichoomba, haitonipunguzia katika nilicho nacho zaidi kuliko sindano inavyopunguza bahari inapochovya.

Enyi waja Wangu, ni vitendo vyenu ninavyovihesabu, kwa ajili yenu nikakulipeni.  Kwa hivyo anayekuta wema amshukuru Allaah na yule anayekuta yasiokuwa mema (basi) ajilaumu mwenyewe.

Imesimuliwa na Muslim



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views 1515

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 ai web app     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Makundi ya dini za wanaadamu

Kwenye kipengele hichi tutajifunza makundi ya dini za watu. Na makundi hayo ni matatu.

Soma Zaidi...
Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika Surat ahzab

Na waliposema wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, "Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu.

Soma Zaidi...
Ni Ipi Elimu yenye manufaa

Elimu inaweza kugawanyika katika makundibmrngine mawili ambayo ni elimu yenye manufaa na elimubisiyi na manufaa

Soma Zaidi...
Kwa namna gani nabii Musa na Bi Mariam waliweza kuzungumza na Allah nyuma ya pazia

Nabii Musa na Mama yake nabii Isa bi Mariam waliweza kuwasiliana na Allah nyuma ya pazia.

Soma Zaidi...