msimamo wa uislamu juu ya kupanga uzazi na uzazi wa mpango

Msimamo wa Uislamu juu ya kudhibiti uzaziKama tulivyoona, msukumo wa kampeni ya kudhibiti kizazi, umetokana na mfumo mbaya wa kijamii na kiuchumi ulioundwa na wanadamu kutokana na matashi yao ya ubinafsi.

msimamo wa uislamu juu ya kupanga uzazi na uzazi wa mpango

Msimamo wa Uislamu juu ya kudhibiti uzazi
Kama tulivyoona, msukumo wa kampeni ya kudhibiti kizazi, umetokana na mfumo mbaya wa kijamii na kiuchumi ulioundwa na wanadamu kutokana na matashi yao ya ubinafsi. Je, katika Uislamu ambapo kila kipengele cha maisha katika jamii kinaendeshwa kwa kufuata sheria za muumba, kuna haja ya kampeni ya kudhibiti kizazi? Hebu tujibu swali kwa kuuangalia kwa muhtasari mfumo wa jami ya Kiislamu.



Mfumo wa uchumi wa Kiislamu unapingana na mfumo wa kibepari na uchumi wa ulimbikizaji mali pasi na kutoa jasho. Uislamu umeharamisha nba, kamari, kuhodhi bidhaa, udanganyifu na ujanja katika biashara, n.k. Badala yake Uislamu umeweka mfumo wa uchumi ambao unamlazimu kila mtu kutekeleza wajibu wake katika kuchuma na kujipatia chumo halali linalotokana na jasho lake. Pia Uislamu umeweka mfumo wa mgawanyo wa uchumi kwa njia ya Zakat, Sadaqa, urithi, mshahara unaolingana na kazi na kuhakikisha kuwa kila mtu anapata mahitaji muhimu ya maisha yake, ambapo humpelekea kuinua hali za watu mbali mbali za kiuchumi ili kuondoa matatizo yanayosababishwa na mgawanyo mbaya wa uchumi kama ule wa nchi za Ulaya na Marekani uliosababisha kuinukia kwa watu wachache kumiliki uchumi wote wa jamii na kuwanyonya sana watu wengine waliobakia katika jamii.



Jamii ya Kiislamu pia imempa mwanamke haki zake zote za kisheria, kijamii na kiuchumi sawa na ilivyompa mwanaume. Mke ana haki ya kisheria katika kipato cha mumewe, ana haki zote za kumiliki kile alichokichuma mwenyewe, ana haki ya kuwa na hisa kwa jina lake katika taasisi yoyote ya kiuchumi. Bali Uislamu umeweka mipaka ya ufanyaji kazi baina ya wanaume na wanawake. Umeweka mgawanyo wa kazi za wanaume na kazi za wanawake kulingana na maumbile yao. Mchanganyiko holela kati ya wanaume na wanawake umeharamishwa na wanawake wameamrishwa kuvaa "hijabu" (vazi Ia Kiislamui lenye kumstiri mwanamke vizuri kama anavyoridhia Allah (s.w)) wakati wanapokuwa nje ya majumba yao au wakati wakiwa katika hadhara ya wanaume waasio maharimu zao.



Hivi ndivyo Uislamu ulivyotatua matatizo mengi ya kiuchumi na kijamii ambayo huwapelekea wanaume na wanawake kuchupa mipaka ya maumbile katika utendaji wao. Hifadhi na maendeleo ya maisha ya mwanaadamu havikuachwa vibuniwe na mwanaadamu, bali mfumo mzima wa maisha ya jamii umewekwa na Muumba kwa kiasi kwamba kwa upande mmoja mahitajio yote muhimu ya maisha ya mwanaadamu (kama vile chakula, mavazi, makazi) yanakidhiwa na kwa upande mwingine jukumu Ia kuzaa na kulea kizazi kipya linaendelea kwa namna bora kabisa.



Kwa upande wa maadili, Uislamu unamtaka mwanadamu aishi maisha ya heshima na sitara yaliyoepukana na mambo ya aibu. Uislamu unaharamisha mambo yote yanayomvunjia mwanaadamu hadhi yake na utu wake ikiwa ni pamoja na ulevi, uzinifu, uzururaji, uvivu na upotezaji muda katika mambo ya upuuzi. Uislamu unaalani uzembe na kutowajibika, ubadhilifu, anasa na mambo yote yanayompelekea mwanadamu kujisahau. Uislamu unamtaka mwanaadamu aishi maisha ya kati na kati- afanye kazi kwa bidii na kupumzika, awe na vitu na utu, ayajali maisha yake ya binafsi na maisha ya jamii. Kwa mfano katika Qur-an tunahimizwa:


"Enyi wanaadamu chukueni mapambo yenu wakati wa kila sala na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizuri) lakini msipite kiasi (msfanye israfu). Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wapitao kiasi (wapindukiao mipaka). (7:31).



Mtizamo wa Uislamu juu ya matumizi, ni kwamba utajiri wote na kila alicho nacho mwanadamu ni amana ya Allah (s.w) ambayo hana budi kuitumia kwa kuzingatia maagizo Yake (s.w). Hana budi kuitumia katika mambo ya halali kwa kiasi kile kile kinachohijika. Kwa hiyo, Uislamu haukubaliani kabisa na anasa na ubadhilifu wa mali, vitu ambavyo ndio vichochezi vikubwa vya kampeni hii ya kudhibiti uzazi.


Pia Uislamu unawahimiza watu kupendana, kusaidiana na kuhurumiana. Unasisitiza kila mtu kupewa haki yake katika jamii na unaweka utaratibu wa kushirikiana na kusaidiana. Uislamu umeweka mfumo unaoifanya jamii iwajibike katika kuwasaidia na kuwahifadhi mafukara, maskini na wale wote walioathirika kiuchumi kutokanana tatizo moja au jingine bila ya ubaguzi wa dini, rangi, kabila wala taifa. Pia Uislamu umeweka utaratibu wenye kuzuia uchoyo, ubinafsi na unyonyaji, maovu ambayo yamekuwa ndio vichochezi vikubwa sana katika kuleta dhana ya kuwa na sera ya kudhibiti uzazi.



Pamoja na mfumo huu wa Kiislamu, Uislamu unamkumbusha mwanadamu mara kwa mara kuwa hapa ulimwenguni hayuko mwenyewe katika kuendesha maisha yake, bali yuko karibu sana na Mwenyezi Mungu ambaye ni Muumba wake, Mlezi wake na Bwana wake pekee. Mwanadamu hana budi kujitahidi katika kuchuma lakini hana budi kukumbuka kuwa matunda yajitihada zake yatapatikana kutoka kwa Allah (s.w).Jitihada za mja hazishindi kudra ya Muumba. Kwa hiyo mwanaadamu pamoja na kujitahidi katika kuchuma hana budi kumtegemea Muumba wake na awe na yakini kuwa Yeye pekee ndiye Mlishaji na Mlezi wake kama anavyovilisha na kuvilea viumbe vyote vilivyomzunguka. Utambuzi huu utamwondolea mwanadamu dhana na kiburi kuwa yeye mwenyewe ndiye anayejilisha na kujitosheleza kwa kila kitu. Dhana hii ya kuwa mwanaadamu anajilisha na kujitegemea mwenyewe ni sababu nyingine iliyochochea sera hii ya kudhiibiti uzazi. Allah (s.w) anatuasa katika aya zifuatazo:


Wala msiwaue watoto wenu kwa kuogopa umaskini. Sisi ndio tunaowaruzuku wao na nyinyi (pia). Kwa yakini kuua ni hatia kubwa. (17:31).


Na wanyama wangapi hawawezi kujimilikia rikizi zao;


Mwenyezi Mungu huwaruzuku wao na nyinyipia, naye ndiye asiki aye, ajuaye. (29:60)
Aya hizi na nyingine kama hizi (Rejea Qur-an 2:29, 67:15, 51:58, 15:20-21) zinamkumbusha mwanadamu kuwa pamoja na jitihada zake za kujitafutia maslahi ya maisha yake na ya wale walio chini ya uangalizi wake, hana budi kufahamu kuwa riziki inatoka kwa Allah (s.w). Kwa mtazamo huu wa kumuelekea Allah (s.w) kuwa ndiye Rabbi (Bwana, Muumbaji, Mlishaji na Mlezi) wa viumbe vyote, jamii ya Kiislamu kamwe haiwezi hata kukaribisha mawazo ya kuwa na sera ya kudhibiti uzazi, eti kwa kuhofia njaa au upungufu wa mahitajio muhimu ya maisha.



Kwa muhtasari, tumeona kuwa mfumo wa Uislamu ukiwa ni pamoja na mfumo wake wa uchumi, utamaduni, maadili na mtazamo wake juu ya uendeshaji wa maisha na kufikia lengo lake, hauna nafasi ya kuruhusu msukumo uliopelekea kutokea kwa kampeni hii ya kudhibiti uzazi na kuifanya sera ya jamii. Kwa hiyo usitazamie kamwe kwa jamii ya Kiislamu kufikiria kuwa na sera ya kudhibiti uzazi.



Kwa maelezo yote haya, ni dhahiri kuwa sera ya kudhibiti uzazi haina nafasi katika Uislamu - wala si jambo Ia kulikaribisha katika fikra za Muislamu kwa sababu:
(a)Dhana kuwa wanaadamu wakiwa wengi watakosa riziki ni potofu. Ni kukana uwezo wa Allah, na huo ni utwaghuuti (uchupaji mipaka).



(b)Matatizo ya uchumi (mbali na mengine pia) yashawekewa ufumbuzi wake na mfumo wa maisha ya Kiislamu.



(c)Sababu nyingine inayofanya sera ya kudhibiti uzazi kijamii isikubalike katika Uislamu ni kuwa huchochea uzinifu. Sera hii imejengwa juu ya dhana kuwa hakuna makosa mume na mke kuingiliana iwe ni nje ya ndoa, wawe ni watoto wa shule n.k. bali lililokosa ni kuzaa mtoto. Kwa hiyo ili mafasiki wautumie "uhuru wao kikamilifu" hapana budi uwepo utaratibu wa kuwahifadhi wasifanye kosa Ia kuzaa - au tuseme kuzaa kiholela. Huku ni kueneza uzinifu na ufuska katika jamii. Hapana haja ya kuyakariri tena madhara yake hapa, lakini jambo Ia kutilia mkazo hapa ni kuwa sera ya kudhibiti uzazi inachochea zinaa na zinaaa ma madhara makubwa katika jamii. Ndio maana Uislamu umeiharamisha zinaa na kuikemea vikali:


Wala msikaribie zinaa. Hakika hiyo ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa). (17:32)


Mzinfu mwanamke na mzinfu mwanamume, mpigeni kila mmoja katika wao m/eledi (bakora) mia. Wala isiwashike kwa ajili yao huruma katika (kupitisha) hukumu hii ya Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu (liii) kundi ?a waislamu. (24:2)
Zaidi ya kuweka makemeo na adhabu kali kwa mzinifu, Uislamu umeweka kanuni za kudhibiti vishawishi vya zinaa kwa kuhimiza "Hijab"



(d)Tusisahau pia kuwa kuweka sera ya kudhibiti uzazi ni kuingilia mfumo na utaratibu wa Allah (s.w). Allah (s.w) ameweka utaratibu wa mahusiano ya mume na mke yawe kwa njia ya ndoa. Kuhusu malengo ya ndoa tunafahamishwa katika Qur-an:


"... Wao (wanawake) ni kama nguo kwenu na nyinyi (wanaume) ni kama nguo kwao..." (2:187)


"Wanawake ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Na tangulizeni (wema) nafsi zenu; na mcheni Allah najueni kwamba mtakutana naye." (2:223)


Na katika Ishara Zake nikuwa amekuumbieni wake zenu kama jinsi yenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya ziko ishara kwa watu wanaofikiri. (30:21)



Kama aya zinazobainisha, malengo ya ndoa ni
(i) Kupata watoto na kuendeleza kizazi.
(ii)Kujenga maisha ya jamii. Mume na mke wanapoamua kuishi pamoja katika misingi ya ndoa, makutano yao kimwili hupalilia mapenzi na huruma kati yao ambayo huwa msingi imara wa kuunda jamii yenye kuishi kwa furaha na amani.



Je, kukutana mwanamke na mwanamume kwa lengo tu Ia kufurahia ngono, kunapelekea kufikiwa kwa moja ya malengo haya? Kama sivyo huku ni kutumia vipawa vya kimaumbile nje ya lengo lililokusudiwa na ni kuingilia mfumo wa maumbile aliouweka Allah (s.w). Qur-an imekuwa bayana mno kuwa kuingilia au kubatilisha mfumo wa maumbile aliouweka Allah ni kitendo kiovu mno na cha kitwaghuuti.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 182


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Sulaiman(a.s)
Kutokana na histoira ya Nabii Sulaiman (a. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa surat Al-Humazah
Zijuwe sababu kuu za kushuka surat Al-Humazah katika quran Soma Zaidi...

Hadithi Ya 26: Kila Kiungo Cha Mtu Lazima Kitolewe Sadaka
Soma Zaidi...

MASWALI MUHIMU KUHUSU HISTORIA NA MAISHA YA MTUME (S.A.W)
1. Soma Zaidi...

Vipengele vya Mikataba ya 'Aqabah na faida zake katika kuimarisha uislamu Maka na Madina
Katika Hija iliyofuatia katika mwaka wa 621 A. Soma Zaidi...

mtazamo wa uislamu juu ya dini
Soma Zaidi...

DARSA ZA TAWHID
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Mipaka katika kumtii mzazi, na mambo yasiyopasa kumtii mzazi
Soma Zaidi...

2.3.Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w Quran, tawrat, Zabur na injili
2. Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na Historia ya Nabii Yunus(a.s)
(i) Allah(s. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 21: Sema Namuamini Allah Kisha Kuwa Mwenye Msimamo
Soma Zaidi...

ihram na nia ya Hija na Umra
1. Soma Zaidi...