picha

Funga za suna na funga za kafara na nadhiri: Masharti yake, nguzo zake na wakati wa kutekeleza

Funga za Sunnah.

Funga za suna na funga za kafara na nadhiri: Masharti yake, nguzo zake na wakati wa kutekeleza

Funga za suna na funga za kafara na nadhiri: Masharti yake, nguzo zake na wakati wa kutekeleza

Funga za Sunnah.
- Nia ya kufunga Sunnah inaweza kutiwa muda wowote ule kabla ya Adhuhuri
iwapo mfungaji hakuonja chochote tangu Alfajir.
- Kuna hiari ya kuvunja funga ya Sunnah muda wowote ule pindi itakapobidi.



Umuhimu wa funga za sunnah.
1.Ni kumtii na kumuiga Mtume (s.a.w).
2.Ni kujazilizia mapungufu ya funga ya faradhi.
3.Humuwezesha muumini kufikia lengo la funga (kuwa Wacha-Mungu).
oFunga za Sunnah na namna ya kutekeleza.
a)Kufunga siku tatu kila mwezi.
- Ni kufunga siku tatu mfululizo za mbalamwezi, mwezi 13, 14 na 15.



b)Kufunga ya siku ya Jumatatu na Al-khamisi.
- Jumatatu ni siku aliyozaliwa Mtume (s.a.w) na Al-khamisi ni siku kupandishwa amali za mja kwenda kwa Mola wake.



c)Kufunga siku sita za mwezi wa Shawwal.
- Ni kufunga sita mara baada ya mwezi wa Ramadhani kuisha.



d)Funga ya Arafa.
- Ni kufunga siku ya mwezi 9, Dhul-Hijj ambamo mahujaji wako katika kisimamo katika uwanja wa Arafa.

e)Funga ya Ashura.
- Ni kufunga siku ya mwezi 10, Muharram (mfungo nne). Ni siku aliyookolewa Nabii Musa na Bani Israil kutoka kwa utawala wa Firaun.



f) Funga katika mwezi Shaaban.
- Ni kufunga kwa wingi katika mwezi wa Shaaban bila ya kutimiza siku 30.



Funga za Kafara.
- Ni funga anazolazimika muislamu kufunga ili ziwe kitubio au fidia baada ya kutenda kosa fulani.

Aina za funga za kafara.
1. Kufunga miezi miwili mfululizo kwa muislamu aliyemuua mtu kwa bahati mbaya na akakosa mali ya kulipa fidia.
Rejea Qur’an (4:92).


2. Kufunga miezi miwili mfululizo kwa muislamu aliyemsusa mkewe kwa kumfananisha na mama mzazi wake.
Rejea Qur’an (58:1-4).



3. Kufunga siku tatu mfululizo kama kafara kwa muislamu aliyevunja kiapo.
Rejea Qur’an (5:89).



4. Kufunga miezi miwili mfululizo kwa mume na mke waliofanya jimai (tendo la ndoa) mchana wa mwezi wa Ramadhani.



5. Kufunga kama kitubio cha muislamu aliyewinda na hali yuko katika Ihram.
- Idadi ya siku inategemea na thamani ya kile alichokiua (alichokiwinda).
- Kama hana uwezo wa kufunga, atatoa fidia ya mbuzi au kondoo.
Rejea Qur’an (5:95).



6. Kufunga siku 10, tatu akiwa Makkah na 7 baada ya kurejea nyumbani kwa muislamu aliyevunja miiko ya Ihram.
- Kama hana uwezo wa kufunga, atafidia kwa kuchinja mbuzi au kondoo.
Rejea Qur’an (2:196).



Siku zilizoharamishwa kufunga Sunnah.
i. Siku ya Sikukuu ya Iddil-Fitri na Iddil-Hajj.
- Ni haramu kufunga siku za Idd mbili hizi kwa namna yeyote ile.
ii. Siku za Tashriiq.
- Siku za tashriiq ni tarehe 11 – 13, mwezi wa Dhul-Hajj.
iii. Siku ya shaka.
- Ni siku ya tarehe 29 au 30 mwezi Shaaban kabla ya mwezi wa Ramadhan.
iv. Siku ya Ijumaa.
- Haifai kufunga siku ya Ijumaa tu, isipokuwa kwa aliyekuwa na tabia ya kufunga Sunnah na ikatokea funga ya sunnah ni siku ya Ijumaa.



                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 4793

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 web hosting     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zinazofanana:

Namna ya kutawadha yaani kuchukuwa udhu

Kuchukuwavudhu ni ibada, lakini pia ni matendo ya kuufanya mwilivuwe safi. Katika post nitakwenda kukifundisha namna ya kutia udhu katika uislamu.

Soma Zaidi...
Mifano na namna ya kurithisha

Ugawaji wa mirathi-Mume ana nusu (1/2) = 1/2 -Mama ana sudusi.

Soma Zaidi...