Maumivu ya tumbo la chango wakati wa hedhi

Sababu za maumivu ya tumbo la chango wakati wa hedhi, nini ufanye na dalili za maumivu ya tumbo la chango

Maumivu ya tumbo la chango wakati wa hedhi


MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA HEDHI


Maumivu wakati wa hedhi kama tulivo zoea kuyafahamu kama tumbo la chango, ama chango la wananwake. Kitaalamu maumivu haya yanatambulika kama dysmenorrhea. Ni maumivu ambayo wanayapata wanawake walio katika umri wa kupata hedhi, na mara nyingi yanakuwa ni chini ya tumbo. Kikawaida maumivu haya ni ya kawaida kiasi hayamfanyi mwanamke kushindwakufanya kazi zake. Lakini wakati meingine yanaweza kuwa makali kiasi cha mwanamke kushindwa kufanya kazi. Kuna sababu nyingi za maumvu haya na dalili zake. Makala hii itakwenda kuangalia sababu za tumbola hedhi ama maumivu ya tumbo la chango, dalili zake na nini afanye.


DALILI ZA MAUMIVU YA UMBO LA HEDHI AU CHANGO
1.maumivu ya chini ya tumbo. Maumivu haya ynaanz kidogo kidogo na kuongezeka.
2.Maumivu ya tumbo yanayoanza siku moja ama tatu kabla ya kuingia hedhi na huweza kuendeea kwa siku 2 ama tatu baada ya hedhi
3.Maumivu ya tumbo ya kawaida
4.Maumivu kwenye mgongo na mapaja.


Baadhi ya wanawake pia wanaweza kupata dalili zifuatazo:-
1.Kichefuchefu
2.Kupata kinyesi laini
3.Maumivu ya kichwa
4.Kizunguzungu


SABABU ZA MAUMIVY YA TUMBO LA CHANGO AU TUMBO LA HEDHI
Wakati wa hedhi inapokaribia tumbo la mimba linajikunja na kukaza ili kuondoa tishu (nyamanyama) zilizoota ndani ya tumbo. Wakati huu mwili huzalisha homoni ijilikanayo kama prostagladins ambayo ndio husaidia kuondoa tishu za ziada zilizoota wakati tumbo lilipokuwa tayari kupokea ujauzito. Katika kuodolewa tishu (yamanyama) kizi ndipo mwanamke hupata maumivu ya tumbo la hedho au maumivu ya tumbo la chango.


Walio hatarini zaidi maumivu haya kuwa makali sana
Katika hali ya kawaida maumivu ya tumbo la chango ama maumivu wakati wa hedhi sio makali kiasi hiko cha kuharibu shughuli za kawaida. Ila huweza kutokea wakati mwingine yakaongezeka zaidi ya kawaida. Hii ni kutokana na uzalishwaji wa hmoni kwa wingi. Lakini pia wapo watu wapo hatarini katika hili, yaani maumivu ya tumbo la chango yanaweza kuzidi:-



1.walio katika umri chini ya miaka 30
2.Waliovunja ungo wakiwa na umri wa mika 11 ama chhini ya hapo
3.Kama unapata damu nyingi wakati wa hedhi
4.Kama hedhi yako inarukaruka
5.Unawza pia kurithi hali hii kama ipo kwenye ukoo wenu
6.Kama unavuta sigara




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 176


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-