Menu



Dalili za Ukimwi

Makala hii itaeleza dalili za ukimwi, dalili za VVU, magonjwa nyemelezi na matumizi ya ARV

Dalili za Ukimwi

ELIMU YA KUHUSU HIV NA UKIMWI


Ni nini maana ya Ukimwi?
UKIMWI ni ufupisho wa maneno “upungufu wa kinga mwilini” ni hali sugu, inayoweza kutishia maisha inayosababishwa na virusi vya Ukimwi (VVU). Kwa kuharibu mfumo wako wa kinga, VVU huingilia uwezo wa mwili wako kupambana na viumbe vinavyosababisha magonjwa. Viumbe hivyo ni kama bakteria, virusi, protozoa, fangasi na vinginevyo.




Nini maana ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)?
VVU ni ufupisho wa maneno Virusi Vya Ukimwi, ni virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini. Hudhoofisha mwili uwezo wake kujilinda dhidi ya vijidudu vya maradhi. Neon hili kwa lugha ya kiingereza hufupishwa kama HIV.




VVU ni maambukizo ya zinaa. Yanayoweza pia kuenezwa kwa kuongezewa damu iliyoambukizwa au kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au kunyonyesha. Inaweza kuchukua miaka mimngi huwenda 5 mpaka 10 kabla ya VVU kudhoofisha kinga yako ya mwili hadi kufikia ukimwi.



Je ipo tiba ya VVU na UKIMWI?
Hakuna tiba ya VVU / UKIMWI, lakini kuna dawa ambazo zinaweza kupunguza kasi ya ukuaji wa magonjwa na uharibifu wa kinga ya mwili. Dawa hizi zimepunguza vifo vya UKIMWI katika mataifa mengi yaliyoendelea. Lakini VVU inaendelea kupunguza idadi ya watu barani Afrika, Haiti na sehemu za Asia. Dawa hizi mimkusanyiko wa dawa nyingi kwa pamoja hufahamika kama ARV yaani Ant-Retrovirus na matibabu yake hufahamika kama ART yaani Ant-Retroval Therapy. Dawa hizi piazimegawanyika katika makundi mengi kama NRTIs, NNRTs, Protease inhibitors na nyinginezo kibao.




DALILI ZA VVU NA UKIMWI NI ZIPI?
Dalili za VVU na UKIMWI hutofautiana, kulingana na awamu ya maambukizo, muda kutoka maambukizo yalipotokea pia afya ya mtu kabla ya maambukizo.
Hatua ya kwanza ya maambukizi (Primary infection)

Watu wengi walioambukizwa na VVU hupata ugonjwa unaofanana na Homa ndani ya mwezi mmoja au miwili baada ya virusi kuingia mwilini. Hivyo kutengeneza dalili za awali za VVU na UKIMWI. Dalili hizi si lazima zimpate kila mtu, wapp wengine hawazipati kabisa. Sana dalili hizi hutokea wiki mbili toka kupata maambukizi mpaka wiki nne kisha hupotea. Kwa baadhi ya watu zinaweza kuanzia wiki ya kwanza, na wengine kuishia wiki ya sita. Dalili hizo ni:-




1.Kupatwa na homa.
2.Maumivu ya kichwa yasiyo na sababu
3.Maumivu ya misuli
4.Kuota upele
5.Kupatwa na baridi ama kuhisi baridi.
6.Kukauka na koo ama kupatwa na vidonda kooni.
7.Kupatwa na Vidonda vya kinywa au sehemu za siri
8.Kuvimba kwa Tezi za limfu kwenye mapaja, makwapa na haswa kwenye shingo
9.Mwili kuwa na Maumivu bila ya sababu maalumu.
10.Kutokwa na Jasho la usiku
11.Kuharisha



Ingawa katika kipindi hiki kiwango cha virusi sio rahisi kuviona kwa vipimo vya kawaida vinavyotumika kupima, lakini ni kuwa katika kipindi hiki kiwango cha virusi ni kingi sana kwenye damu, na muathirika anaweza kumuambukiza mwengine kwa urahisi sana. Baada ya wiki sita dalili hizi hupotea na hazitajirudia tena. Hapa virusi vitatulia ndani ya mwili kwa miaka mingi bila ya kuonyesha dalili yeyote ile, huku vukiendelea kuharibu kinga ya mwili kidogokidogo.




Hatuwa ya pili Toka kuambukizwa.
Kama tulivyoona dalili za VVU katika hatuwa ya kwanza. Sasa hutokea kwa baadhi ya watu kuwa tezi za limfu zisivimbe wakati wa hatuwa ya kwanza, ila zikavimba katika hatuwa hii ya pili. Tofauti na hili hakuna dalili nyingine maalumu ya VVU katika hatuwa hii ya pili. Hatuwa hii inaweza kuchukuwa mpaka miaka 10. Kwa watu wengi ni kati ya miaka 4 mpaka 10 ila wengine mara chache hutokea ikawa chini ya hapo.




Baada ya maambukizi ya Awali
Hiki ni kipindi cha miaka kadhaa baada ya kuambukizwa. Katika wakati huu hakuna dalili ya VVU inayoonekana. Hata hivyo kadri iaka inavyosonga mbele ndivyo seli zinavyozidi kudhoofu. Wakati virusi vinaendelea kuongezeka na kuharibu seli za kinga, unaweza kupata maambukizo kidogo au ishara sugu na dalili kama vile:




1.Homa
2.Uchovu
3.Node za mtoki, kwapa, na shingo kuvimba – na hii ndio mara nyingi moja ya ishara za kwanza za maambukizo ya VVU
4.Kuhara
5.Kupungua uzito
6.Kikohozi
7.Kupumua kwa pumzi




Kuendelea kwa UKIMWI
Ikiwa hautapata matibabu maalumu ya ART na kutumia ARV mapema iwezekanavyo kwa ajili ya kuthibiti maambukizo yako ya VVU, ugonjwa huendelea hadi kufikia kuwa UKIMWI kwa takriban miaka 10. Wakati huu ukiwa na UKIMWI unakua, mfumo wako wa kinga umeharibiwa sana, na hivyo kukufanya uweze kuambukizwa na magonjwa nyemelezi – Mgonjwa nyemelezi ni magonjwa ambayo hayangemsumbua mtu aliye na kinga nzuri.



DALILI ZA UKIMWI.
Mpaka kufikia hapa ndipo mgonjwa huambiwa ana UKIMWI. Kumbuka mpaka kufikia hapa tayari miaka Zaidi ya mine hadi 10 itakuwa imepita. Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa endapo mgonjwa hatatumia matibabu maalubu ya ARV hatoweza kuzidi miaka 3. Sasa hebu tuzione dalili na Ishara za UKIMWI katika hatua hii:-




1.Kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku
2.Kutetemeka kwa homa au Homa juu inayofikia nyuzi 100 F (38 C) na kudumu kwa wiki kadhaa
3.Kikohozi
4.Kupumua kwa pumzi za taabu
5.Kuhara kusiko kata
6.Utando mweupe wa kudumu au vidonda visivyo vya kawaida kwenye ulimi wako au kinywani mwako
7.Maumivu ya kichwa mara kwa mara
8.Uchovu wa kudumu, usioelezewa
9.kuona maluweluwe
10.Kupungua uzito bila ya sababu maalumu
11.Vipele kwenye ngozi au majipu




NJIA AMBAZO VVU HUAMBUKIZWA;
Kuna nadharia nyingi zinaelezea ni namna gani ambazo VVU huambukizwa. Katika hizo kuna mbazo ni Imani potofu kabisa na hazifai kukubaliwa. Hapa nitakuletea njia ambazo zinaambukiza VVU. Njia hizo ni:-
1.Kwa kufanya mapenzi (ngono). Unaweza kuambukizwa ikiwa unafanya ngono ya uke, ya mkundu au ya mdomo na mwenzi aliyeambukizwa VVU ambaye damu yake au shahawa zake au majimaji ya ukeni huingia mwilini mwako kwa kupitia michubuko midogo, ama vidonda ama mikato ama sehemu iliyowazi inayoruhusi kufikiwa damu kwa urahisi. Na hii ndiyo njiainayoongoza katika kuambukiza VVU



2. Kwa kuongezewa damu kutoka kwa aliye athirka. Katika namn nyingine, virusi vinaweza kuambukizwa kupitia kuongezewa damu. Kwa sasa si sana njia hii maana damu anayopatiwa mgonjwa itapitia uchunguzi wa kina kabla ya kuongezewa ijapokuwa madhaifu ya kibinadamu yanaweza kufanyika.



3. Kwa kushirikiana matumizi ya sindano na vitu vyenye ncha kali kama visu na viwembe. VVU vinaweza kuambukizwa kupitia sindano, inaweza kutokea wakatiwa matibabu yatakayofayika chini ya utaratibu. Inaweza pia kuwa watumiaji a madawa ya kulevya hushirikiana sana matumizi ya sindano. Endapo mtumiaji wa kwana ana VVU na akajidunga ama kujikata, kisha akachukuwa mtumiaji mwinine na kujidunga ama kujikata muda mfupi toka mtumiaji wenye VVU kutumia.



4. Wakati wa ujauzito au kujifungua au kupitia kunyonyesha. Mama walioambukizwa VVU wanaweza kuambukiza watoto wao endapo hwatakuwa makini. Mama mjamzito mwenye VVU anatakiwa atumie dozi haraka iwezekanavyo ili kuepushamaambukizi kwa mtoto. Hata hivypo inampasa azalie hospitali ili uangalifu zaidi ufanyike wakati a kujifunguwa.



HAYA HAYAWEZI KUAMBUKIZA VVU
1.Mate
2.Mkojo
3.Kugusana mikono ama kukumbatia
4.Kula pamoja
5.Kucheza pamoja.
6.Kung’atwa na mbu



SASA UKIMWI UNATOKEAJE?
Seli ndio matofali yaliyojengea miili yetu. Ndani ya miili yetu kuna aina nyingi za seli, na seli za damu. Ndani ya damu pekee kuna aina zisizopunguwa tatu za seli. Kuna seli hai nyekundu, nyeupe na seli sahani. Kila seli kati ya hizi ina kazi zake. Sasa hii seli hai nyeupe yenyewe ndio inakazi ya kupigana na vijidudu vya maradhi vinapoingia katika miili yetu. Vijidudu hivyo vinaweza kuwa bakteria, virusi ama fangasi. Seli hizi ndizo ambazo ambazo huitwa CD4.



Sasa virusi vya VVU vinapoingia mwilini vinaanza kuharibi hizi seli ambazo zinalinda mwili. Kawaida mtu anaweza kuwa na seli hizi 500 mapa 1500 katika kipimo kimoja. Sasa VVU vinaanza kuziharibu hizi na kupunguza idadi yake. Na kila seli hizi zikipunguwa ndipo mfumo wa kinga unavyoendelea kuharibika na ndivyo maradhi yanapozidi kupata nafasi ya kuingia mwilini.



Sasa endapo zimeharibiwa na kufika idadi ya 200 katika kipimo kimoja hapa mtu huyu ataambiwa ana Upungufu wa Kinga Mwilini yaani UKIMWI. Katika hatuwa hii mtu atakuwa akinyemelewa na maradhi nyemelezi kama fangasi, kifuwa kikuu, na mengineyo.



Endapo mgonjwa atatumia ARV mapema anaweza kukaa miaka mimngi sana bila ya kufikia hatuwa hii. Kuna umuhimu wa kutumia ARV mapema, sababu hizo ni kama:-
1.Kupungua maambukizi ya VVU
2.Kulinda afya ya mtu
3.Kupunguza uharibifu wa seli
4.Kulinda mwili dhidi ya maradhi nyemelezi.







                   



Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views 1262

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Daliliza shinikizo la Chini la damu.

Shinikizo la chini la damu (hypotension) litaonekana kuwa jambo la kujitahidi. Hata hivyo, kwa watu wengi, shinikizo la chini la damu linaweza kusababisha dalili za Kizunguzungu na kuzirai. Katika hali mbaya, shinikizo la chini la damu linawez

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea

Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Soma Zaidi...
Njia za kuzuia Ugonjwa wa tauni.

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepuka Ugonjwa wa raundi.

Soma Zaidi...
Saratani ya Matiti ya wanaume.

Posti hii inazungumzia kuhusiana na Saratani ya matiti ya Mwanaume ni Saratani nadra ambayo hutokea katika tishu za matiti za wanaume. Ingawa saratani ya matiti hufikiriwa zaidi kuwa ugonjwa wa wanawake, saratani ya matiti ya mwanaume hutokea. Saratani y

Soma Zaidi...
Tatizo la kujaa mate mdomoni nimeambiwa nina minyoo

Mie ni kijana wa kiume umri 33, nna tatizo la kujaa mate mdomoni nimeambiwa nna minyoo lakini hata nikinywa dawa sioni afadhali, niliona labda ni pombe nikapumzika kunywa tatizo lipo pale pale japo nisipokunywa haliwi kwa ukubwa ule ila lipo.

Soma Zaidi...
Sababu za Kuvimba kwa kope.

Post hii inazungumzia kuhusiana na Sababu zinazopelekea kuvimba kwa kope, kawaida huhusisha sehemu ya kope ambapo kope hukua na kuathiri kope zote mbili. Pia hutokea wakati tezi ndogo za mafuta ziko karibu na msingi wa kope huziba. Hii inasababisha kuw

Soma Zaidi...
Jinsi ya kujilinda na maradhi ya ini

Hapa nitakueleza namna ambavyounaweza kupunguza hatari ya kupata maradhi ya ini. Kwa njia hizi unaweza kujikina wewe na wengineo na maradhi haya hatari ya ini.

Soma Zaidi...
Fahamu sababu za ugonjwa unanipeleka Kuvimba kwa mishipa ya Damu

posti hii inazungumzia kuhusiana na ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu katika mwili wako wote. Kuvimba kwa Mishipa ya Damu hujulikana Kama Behcet amboyo husababisha dalili nyingi ambazo hapo awali zinaweza kuonekana kuwa hazihusiani. Dalili na ish

Soma Zaidi...
Dalili za minyoo mviringo (ascariasis)

Ascariasis ni aina ya maambukizi ya minyoo mviringo. Minyoo hii ni vimelea wanaotumia mwili wako kama mwenyeji kukomaa kutoka kwa mabuu au mayai hadi minyoo wakubwa. Minyoo ya watu wazima, ambayo huzaa, inaweza kuwa zaidi ya futi (sentimita 30) kwa

Soma Zaidi...
Madhara ya kutotibu ugonjwa wa makende kushindwa kushuka

Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu magonjwa ya makende kushindwa t, hiki ni tatizo na huleta madhara

Soma Zaidi...