Naulizia nyenzo alizotumia nabii Ada (A.S) kusimamisha ukhalifa
Baada ya Nuhu(a.s) Mtume aliyemfuatia ni Nabii Hud(a.s). Hud(a.s) alitumwa na Mola wake kuwalingania kabila (taifa) la ‘Ad. Kabila la ‘Ad lilikuwa likijulikana kama ‘Ad-al-ram au ‘Ad-Ula. ‘Ad walikuwa wakiishi kusini ya Bara
Swali:
Naulizia nyenzo alizotumia nabii Ada (A.S) kusimamisha ukhalifa
Jibu
Mbinu za Hud(a.s) Katika Kufikisha Ujumbe
Katika kulingania Uislamu kwa watu wake, Hud(a.s) alitumia mbinu zifuatazo:
Kwanza alijieleza kwa uwazi na kuwanasihi watu wake:
“Akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi sio mpumbavu. Lakini mimi ni Mtume niliyetoka kwa Mola wa walimwengu. Nakufikishieni ujumbe wa Mola wangu. Na mimi kwenu ni (mtu) nasihi muaminifu.(7:67-68)
Mnaona ajabu kukufikieni mawaidha yanayotoka kwa Mola wenu kwa (ulimi wa) mtu aliye mmoja katika nyinyi ili akuonyeni? (Muabuduni Mwenyezi Mungu) na mkumbuke alivyokufanyeni Khalifa baada ya watu wa Nuhu.Na akakuzidisheni sana katika umbo. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu.” (7:69)
Pili aliwapa hoja kwanini wanalazimika kumuamini Allah na kumuabudu ipasavyo.
Mcheni yule ambaye amekupeni haya mnayoyajua.” “Amekupeni (chungu ya) wanyama na watoto wanaume.” “Na mabustani na chemchem, (mito).” (26:132-134)
Tatu, aliwabashiria kupata malipo mema hapa hapa ulimwe nguni endapo watamcha Allah(s.w) ipasavyo:
“Enyi watu wangu! Ombeni msamaha kwa Mola wenu (kwa mabaya yenu yaliyopita) kisha mtubie kwake, atakuleteeni mawingu yateremshayo mvua tele, na atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu (mlizonazo). Wala msikengeuke kuwa waovu.” (11:52)
Nne, aliwahofisha watu wake na adhabu kali ya Allah(s.w)
iwapo watamuasi.
“Na kama mtarudi nyuma (hainidhurishi kitu); nimekwisha kukufikishieni niliyotumwa nayo kwenu; na Mola wangu atawafanya makhalifa (wakazi wa mahali hapa) watu wengine wasiokuwa nyinyi; wala nyinyi hamtaweza kumdhuru hata kidogo. Hakika Mola wangu ni Mwenye kuhifadhi kila kitu.” (11:57)
“(Wakumbushe) alipowaambia ndugu yao Hud.‘Je, hamtamu ogopa (Mwenyezi Mungu hata nikikutajieni adhabu yot itakayokufikieni kwa mabaya yenu mnayoyafanya)? Bila shaka mimi kwenu ni Mtume muaminifu.” (26:124-125).
Tano,aliwafahamisha kwa uwazi watu wake kuwa hakutarajia kupata malipo ya Utume wake kutoa kwao.
“Enyi watu wangu! Sikuombeni ujira juu ya haya. Haukuwa ujira wangu ila kwa yule aliyeniumba. Basi hamyatii akilini (haya ninayokuambieni)?” (11:51).
“Wala sikutakieni juu yake ujira, ujira wangu haupo ila kwa
Mola wa walimwengu wote.” (26:127)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 ai web app 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Mafunzo ya Computer kwa Kiswahili
Utajifunza na kuelewa hata kama hauna computer kwa muda huo
Soma Zaidi...Faida za mbegu za maboga
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za mbegu za maboga
Soma Zaidi...Tabia za watu wenye damu ya group A au kundi A.
Posti hii inahusu zaidi tabia za watu wenye damu la kundi A na vyakula ambavyo wanapaswa kuvitumia, na pengine tutaona baadhi ya vyakula ambavyo havipaswi kutumiwa na watu wenye damu ya kundi A au group A
Soma Zaidi...