Naomba mnielekeze jinsi ya matayarisho ya Mbegu za papai mpaka nianze kuzitumia kama tiba


image


Mbegu za papai ni katika baadhi ya mbegu ambazo hutumika kama dawa, na tunda lake ni katika matunda yenyevirutubisho vingi sana. Mbegu za papai zinatumka kwa matumizi mengi sana kiafya. Je ungependa kujuwa faida za papai na jinsi ya kuandaa mbegu zake kama tiba? endelea na makala hii


SWALI:

Naomba mnielekeze jinsi ya matayarisho ya Mbegu za papai mpaka nianze kuzitumia.

Papai ni katika matunda yenye vitamini C kwa wingi. Ukiachia mbali na utamu wa tunda hili lakini papai mbegu zake zina faida kubwa kiafya mwilini. Makala hii itakueleza faida za mbegu za papai na jinsi ya kuziandaa kama dawa.

 

Faida za mbegu za papai

Mbegu za papai mara nyingi huliwa baada ya kukaushwa na kusagwa unga. Pia unaweza kuzikaanga kidogo ama kuzichemsha.

  1. husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi vyema
  2. Husaidia kuzuia kupata saratani
  3. Hulinda figo kufanya kazi vyema
  4. Husaidia mwili katika kupambana na vijidudu vya maradhi
  5. Husaidia kwa wenye kisukari
  6. Husaidia katika kuondosha sumu za kemikali mwilini
  7. Mbegu za papai zina virutubisho mbalimbali

 

Jinsi ya kuandaa mbegu za papai:-

1. Zitoe vyema kwenye papai

2. Zianike hadi zikauke

3. zisage unga

4. Tumia unga wake kwenye chai ama uji kijiko kimoja kila siku.

 

Faida za kiafya za kula papai

1. Papai ni katika matunda yanayoingiza afya sana kwenye mwili wa binadamu. Papai lina vitamin C na vitamini A kwa wingi pia kuna potassium na folate. Pia tafiti zinaonesha kuwa antioxidant aina ya lycopene iliyomo kwenye papai husaidia katika kuzuia kupata saratani.

2. Pia papai lina vitamin B, vitamin E na vitamin K. Pia lina madini ya calsium (kashiam) potassium, mgnessium na copper. Pia punje za papai ni dawa kwa baadhi ya matatizo ya ini na figo. Pia kwenye papai kuna protelytic enzymes hawa husaidia katika kuuwa bakteria na minyoo pamoja na wadudu wengine hatari ndani ya tumbo (mfumo wa kum eng’enya chakula).

4. Papai linatambulika kwa kuwa na uwezo wa kuulinda mwili na maradhi ya uzee kama macho, misuli na kuzeheka kwa haraka. Ndani ya papai kuna Zeaxanthin hii ni anti oxidant ambayo inakazi ya kuchija miale hatari ya jua. Pa inaaminika kuwa antioxidant hizi husaidia katika afya ya macho na husaidia katika kudhibiti kudhoofu kwa misuli.

45. Papai huaminika kusaidia kupunguza hatari ya kuwa na ugonjwa wa pumu. Hupunguza hatari ya kuuguwa pumu. Ndani ya papai kuna virutubisho vingi, lakini uwepo wa beta-carotene ndani ya papai husaidia kwa wagonjwa wenye pumu.

 

Soma zaidi hapa



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani offline       ðŸ‘‰    2 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    3 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu       ðŸ‘‰    4 Download App zetu hapa ujifunze zaidi    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Faida za kula pilipili
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula pilipili Soma Zaidi...

image Faida za kula asali
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula asali Soma Zaidi...

image Kazi za tunda la papai katika kurekebisha homoni imbalance
Posti hii inahusu zaidi kazi za tunda la mpapai katika kurekebisha homoni.ni tunda ambalo ufanya kazi yake kwa sababu ya kuwepo kwa virutubisho muhimu ndani ya tunda hili. Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kula karanga
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula karanga Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kula kisamvu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kisamvu Soma Zaidi...

image Uyoga (mushrooms)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula uyoga Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kula fyulisi/ peach
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula fyulisi/peach Soma Zaidi...

image Boga (pumpkin)
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula maboga Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kula tunda pera
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tunda pera Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za peaz/ peas
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula peazi Soma Zaidi...