SWALI

Umuhimu wa kuamini mitume wa Allah katika maisha yetu ya kila siku

Swali No. 226
JIBU

Umuhimu wa Kuamini Mitume wa Allah (s.w)

(i) Kuamini Mitume wa Allah (s.w) ni amri ya Allah (s.w)

Rejea Qur’an (4:150-152)


 

(ii) Kuamini Mitume wa Allah (s.w) ni nguzo ya nne ya imani ya Kiislamu.


 

(iii) Kuamini Mitume wa Allah (s.w) ni miongoni mwa sababu za kunusurika muumini na adhabu ya Allah hapa duniani na Akhera pia.


(iv) Kutoamini Mitume wa Allah (s.w) au Kuamini baadhi na kukufuru baadhi yao ni sababu ya kuangamia mtu Duniani na Akhera.
Rejea Qur’an (4:150-152).Kumbukumbu
Swali hili limeulizwa na Muulizaji Kutoka WhatsApp Chat yetu tarehe 07-02-2023-18:01:33 . Jina la muulizaji limehifadhiwa.

Nicheki Nicheki WhatsApp


MASWALI YANAYOFANANA