Pata jibu kamili kuhusu swali lako
Kwanza utambue kuwa kutopata siku zako sio pekee dalili ya ujauzito. Inaweza kuwa ni side effect ya hiyo sindano.
Pili, mabadiliko tu ya homoni yanaweza kusababisha maumivu na kukosa hedhi.
Tatu dawa za uzazi nasra nyingi husababisha mabadiliko kama hayo.
Jambo la msingi ni kuonana na daktari wako akufanyie uchunguzi juu ya sindano hiyo. Kama inakudhuru akubadilishie.
Hata hivyo yeye inawezekana kupata ujauzito hata kama umetumia sindano endapo kuna shida imetokea lamda dawa imeshindwa kufanya kazi vyema.