SWALI

Je nitapataje backlink ylkwenye website yangu? 

Swali No. 523
JIBU

Ni backlink sio black link. 
Hizi ni link ambazo zinatoka kwenye website kujakwako. 

Kwa mfano kwenye website yangu nikaweka link ambayo inakwenda kwenye website yako,  hiyo link ya post iliyo connect na website yako ni backlink. 

Tuseme hivi: 
Mimi nazungumzia wasanii wakubwa Tanzania sasa nikaona wewe una post imezungumzia kitu kama hiki. Basi mimi nikimaliza kuandika post ninaweka soma zaidi hapa. Kisha naweka link ya post yako. Sasa backlink ni hii link ya post yangu iliyokuja kwako. 

Utapataje backlink
1. Share post zako. 
2. Omba watu wa cpnnect na blog yako. 
3. Andika makala kwenye blog za watu kisha na wewe link na kwako. 
4. Kupiga promotion ya SEO hii njia sikushauri sana maana ina risk sana unaweza pigwa 

Pia fanya hivi: 
1. Nenda jamiiforum andika post kisha link na kwenye blog yako. 

2. Njoo Bongoclass nitakupa access ya kuandika makala uweze ku link na kwako.Kumbukumbu
Swali hili limeulizwa na Muulizaji Kutoka WhatsApp Chat yetu tarehe 26-02-2023-08:50:59 . Jina la muulizaji limehifadhiwa.

Nicheki Nicheki WhatsApp


MASWALI YANAYOFANANA