Ndoa ya siri

NDOA YA SIRI YAFANYIKA Hatimaye siku ya ijumaa ikafika na mimi nikaoga nyema na kuchukuwa kanzu iliyo nadhifu zaidi.

Ndoa ya siri

NDOA YA SIRI YAFANYIKA
Hatimaye siku ya ijumaa ikafika na mimi nikaoga nyema na kuchukuwa kanzu iliyo nadhifu zaidi. Nikaifaa na kujipaka manukato maridadi na kuwa mtanashati ka kuelekea kwenda sala ya ijumaa. Mapema nilifika msikitini na kuanza kumuomba Mungu. Kwa furaha nia shauku nilioa nayo hata sikuweza kulala msikitini. Baada ya sala kuisha nilitoka masikitini na tayari kuelekea kwa kipenzi changu mtarajiwa.



Nilichukuw amashahidi wawili kwa siri, na hawa walikuwa ni wafanyabiashra wenzangu wa kutokea Baghadad. Tulipanda magari ya kuburuzwa na farasi. Tukafika katika nyumba niliyoelekezwa na tayari kugonga mlango. Mabinti wawili wengine walio wazuri sana wakafungua malango na sisi watu watatu tukaingia. Tulikutanan na ukumbi mzuri wenye malumalu za almasi. Ukuta uluojengwa vyema na kutiwa mapambo ya madini ya fedha a almasi.



Nikaangalia vyema nikaona mapambo yenye kuchorwa kwa lugha ya kiarabu kilicho pendeza. Tuliweza kusogea kila chumba kikiwa kina mapazia marefu yenye rangi za kupeneza sana. Mapazia yalikuwa na michirizi ya madini ya silva pamoja na mapambo ya nayoning'inia mithili ya lulu zilizohifadhiwa vyema. Niliweza kustaajabishwa na manukato ya vyumba hivi ni mazuri sana sijapatapo kuyaona. Tuliendelea hata yukafika kwenye kumbi moja kubwa sana. Hapo tukakuta kuna watu kadha aa wanaume.



Niliweza kuchunguza vyema ukumbi huu nikagundua umepambwa mapambo mazuri sana. Umechorwa michoro ya vippeo michoro iliweza kutiwa rangi za kijani, manjano na bluu. Hakiak niliweza kumpa sifa sana mchoraji. Katikati ya chumba kulukuwa na kiti kikubwa sana cha miguu sita. Miguu iliyopamba kwa vishikizo vya madini ya shaba, magodoro ya hariri yalikaa byema kwenye kiti hiko kikubwa.



Juu ya kiti mzee mkubwa alikuwa amekaa hapo. Nilimtambuwa umri wake ni kati ya 60 mpaka 70. alikuwa na ndevu nyingi na nyeupe zilizomkaa vyema. Alikuwa na sharubu nyupi na mashrafa yaliyo lala vyema. Ndevu zenye afya njema zilizotiwa hina na kufanana vyema. Mzee alivaa kanzi nadhifu yenye manukato zaidi ya watu wote tulio hudhuria. Basi tukakaribishwa vyema nikaka mimi na wenzangu. Jumla tulikuwa wtatu 9.
Bila ya kupoteza muda yule mzee akanitaja kwajina 'Je wewe kijana ndiye Ibrahimu Khalidi wa Baghadad?' nilisita kidogo kujibu huku nikiwaza amelijuaje jina langu, na amejuaje kama natokea Baghadad. 'ndiye mimi mzee' basi akaniambia nisogee karibu na ndipo akaniuliza maswali kadhaa na nikamjibu vyema. Basi akaniuliza ' Kijana Ibrahimu khalid umekubali kumuoa mwanangu Nurat khan'? ' hapo ndipo nilipopata kujuwa jina halisi la binti yule na kumjuwa Baba yake. 'Ndio nimekubali kumuoa Nurat Khan'



Baada ya hapo mbele ya mashahidi ndoa ikafungwa. Mashahidi waliweza kupatiwa dhahabu pishi tano kila mmoja na wakaruhudiwa kuondoka. Mimi nikapelekwa kwa mke wangu. Kwa hakika nilipatapo kuona mambo mengi na mazuri na ya kustaajabisha. Naomba nisielezee hasa kipengelehiki. Basi tukaelekea nyumba nyingine ambapo ndipo binti anaishi. Huko ni mbali na alipo baba yake. Na tukaendelea kumaliza taratibu za usikuwa harusi mimi na mkewangu ('taa ikazimwa'.).

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 211

Post zifazofanana:-

Sababu za kushuka surat al-Falaq na surat an-Nas na fadhila za kusoma sura hizi
SURAT AL-MUAWIDHATAYN (SURAT AL-FALAQ NA SURATUN-NAS) Inaelezwa kuwa sura mbili hizi zilishuka pamoja, na maulamaa wanaelezea kuwa Mtume (s. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Kisamvu
Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa mahakama na mahakama ya Kadhi wakati wa makhalifa
Soma Zaidi...

kujiepusha na uongo na sifa za uongo
Uwongo ni kinyume cha ukweli. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 26
19. Soma Zaidi...

HADITHI 40 ZA IMAM NAWAW AROBAIN AN-NAWAWIY
Soma Zaidi...

NAMNA AMBAZO MWILI HUPAMBANA NA MARADHI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Viazi mbatata
Soma Zaidi...

UGONJWA WA HOMA YA VIRUSI VYA ZIKA (ZIKV) VINAVYO SABABISHWA NA KUNG'ATWA NA MBU
Mnamo mwaka 2016 World Health Organization (WHO) iliitisha kikao cha dharura mnamo mwezi tarehe 1 mwezi wa pili mpaka tarehe 13 mwezi wa nne. Soma Zaidi...

Mkataba wa 'Aqabah na vipiengele vyake na mafunzo tunayoyapata katika mkataba wa aqaba
Mtume (s. Soma Zaidi...

Faida za kula Embe
Embe ni katika matunda atamu na yenye faida kubwa kiafya, soma makala hii hadi mwisho Soma Zaidi...

Amri ya Kuchinja Ng'ombe
Kutokana na kuishi kwao Misr kwa muda mrefu, Mayahudi waliathiriwa na ibada za kishirikina za Wamisr. Soma Zaidi...