picha

Kujiepusha na kukaribia zinaa

Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.

Kujiepusha na kukaribia zinaa

(e)Kujiepusha na kukaribia zinaa



Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa. Yanayochochea zinaa ni pamoja na mavazi yasiyozingatia sheria ya Kiislamu; michanganyiko ya wanaume na wanawake isiyozingatia sheria ya Kiislamu; michezo, miziki, ngoma, nyimbo na mengineyo yanayochochea zinaa.



"… Hakika hiyo zinaa ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa)" (17:32)



Uchafu na ubaya wa zinaa unadhihirika wazi kwa wahusika binafsi na kwa jamii kwa ujumla katika maeneo yafuatayo:



(i)Magonjwa ya zinaa ukiwemo UKIMWI, ambayo hudhoofisha afya na kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
(ii)Kuporomosha maadili ya jamii. Watu wazinifu hawana haya, ni watovu wa nidhamu, walaghai, waongo, wabinafsi na wapupia machafu ya kila namna.
(iii)Zinaa huondosha umuhimu na heshima ya ndoa.
(iv)Kuvunja ndoa na kusababisha matatizo ya kifamilia.
(v)Husababisha watoto wa mitaani na kuingiza jamii katika janga la wahuni, wala unga, matapeli, majambazi pamoja na kusababisha kundi kubwa la vijana wasio na uwezo wa kufanya lolote.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views 2964

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Athari za kumuamini mwenyezi Mungu katika maisha ya kila siku

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mtazamo wa kikafiri juu ya maana ya dini.

Maana ya dini kwa mujibu wa makafiri ina utofauti mkubwa na vile ambavyo uislamu unaamini kuhusu dini.

Soma Zaidi...