swala ya witri na namna ya kuiswali

3.

swala ya witri na namna ya kuiswali

3. Swala ya Witri
Witri maana yake ni namba isiyogawanyika kwa mbili kama vile 1, 3, 5, 7, 9, 11 n.k. Sunnah ya witri huswaliwa katika kipindi cha usiku baada ya swala ya Al-Isha na kabla ya kuingia swala ya Al-Fajiri. Lakini ni bora kuichelewesha Witri na kuiswali katika theluthi ya mwisho ya usiku, baada ya swala ya kisimamo (tahajjud).



Mtume (s.a.w) alikuwa akiswali Witri pamoja na swala ya Tahajjud (Swala ya Usiku) na wakati mwingine alikuwa akiswali Witri mara tu baada ya Al-Ishaai. Ni vema kuswali witri baada ya al-Isha kama hakuna uhakika wa kuamka Usiku. Mtume (s.a.w) ameikokoteza sana swala ya Witri kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo:



Buraydah (r.a) amesimulia, Nimemsikia Mtume (s.a.w) akisema; Witri ni haq (wajibu). Asiyeswali si miongoni mwetu. Witri ni wajibu'. (Abu Da udi)



Witri ina swaliwa kwa rakaa tatu. Huswaliwa kwa rakaa mbili na kutoa Salaam, kisha hukamilishwa na rakaa moja.



Namna ya Kuswali Swala ya Witri
1. Katika rakaa ya kwanza utasoma Sura ya Al-A'alaa (Sabbihisma) baada ya Suratul-Faatiha.


Katika rakaa ya pill utasoma Suratul-Kaafiruuna baada ya suratul-faatiha..



Katika rakaa moja ya mwisho. baada ya kusoma Suratul-Faatiha, utasoma Suratul- lkhlas, AI-Falaq na An-naas. Kuleta Qunut (dua) katika rakaa ya mwisho katika ltidali.


Dua tunayoileta katika Qunut ni hii ifuatayo:


Allahumma ihdidaa fii man hadaita "Ewe Mola n[ongoze kama wale uliouxiongoza"



Wa `aafinaa fiiman `aafaita "Na unininusuru kama hao uliowarursuru"



Watawallanii fiiman tawaffaita "Na unitawalishe pamoja na wale ulio watawalisha



wabaarik lii fii maa a'atwaitanii "Na unitilie pataka katika vile ulivyonipa



Waqinii sharra maa gadhwaita "Unikinge na shari ulizonikadiria"


Tabaarakta rabbanaa wata'aalaita "Ni nyingi kabisa juu yetu baraka zako na umetukuka kweli kweli"


Ni muafaka kuleta dua nyinginezo vile vile kulingana na haja ya mwenye kuswali.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 974

Post zifazofanana:-

Chemsha bongo namba 14
12. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Ayyuub(a.s)
Kutokana na kisha hiki cha Nabii Ayyuub(a. Soma Zaidi...

Funga za suna na funga za kafara na nadhiri: Masharti yake, nguzo zake na wakati wa kutekeleza
Funga za Sunnah. Soma Zaidi...

jamii
Soma Zaidi...

nmna ya kufanya istikhara na kuswali swala ya Istikhara
Soma Zaidi...

STANDARD FOUR ENGLISH TEST 14
Soma Zaidi...

HIKUMU YA BASMALLAH YAANI KUSOMA BISMILLAH
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Sababu za Kushuka Surat Al-Masad (tabat yadaa) na fadhila zake
4. Soma Zaidi...

NJIA AMBAZO MARADHI HUAMBUKIZWA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

mafunzo ya TAJWID na imani ya dini ya kiislamu
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEUNGUA
Kuungua kupo kwa aina nyingi. Soma Zaidi...

FORM ONE GEOGRAPHY
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...