NINI VIDONDA VYA TUMBO?
Ni vidonda vinavyotokea katika ukuta wa tumbo. Vidonda hivi tumezoea kuviita vidonda vya tumbo ila hapa nitataja kitaalamu kuwa vidonda hivi hufahamika kama peptic ulcers.

Vidonda hivi hutokea kutokana na mashambulizi ya bakteria wanaoitwa Helicobacter pylori (H.pylori) au kulika kwa ukuta wa tumbo kutokanana na athari za tindikali zilizopo tumboni (stomach acids) kama vile tindikali ya hydrocloric yaani hydrocloric acid. Kwa wakati tulio nao hili ni tatizo la kawaida maana limewapata watu wengi na halisabababishi vifo vya watu wengi kama maaradhi ya saratani na kisukari.

AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda hivi vimegawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni:-
1.Gastric ulcers hivi hutokea ndani ya tumbo la chakula
2.Esophageal ulcers hivi hutokea ndani ya esophagus. Hii ni sehemu inayounganisha kati ya koo la chakula na tumbo la chakula.
3.Duodenal ulcers hivi hutokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayoitwa duodenum
Vidonda vya tumbo ni pamoja na: