Navigation Menu



image

KUAMINI MALAIKA

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

KUAMINI MALAIKA

2.2.Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu (s.w).
Maana: Malaika ni viumbe walioumbwa kutokana na nuru.

Sifa za Malaika:
- Ni viumbe wa kiroho wenye mabawa.
- Ni viumbe wasio na matashi ya kimwili (kula, kunywa, kulala, n.k.)
- Hawana hiari katika kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w).
- Ni vimbe wasio na jinsia.
- Ni viumbe walioumbwa kutokana na Nuru.

Kazi za Malaika.
Zifuatazo ni baadhi tu ya kazi za baadhi ya Malaika.
(a)Kuleta Wahyi (ujumbe) kwa wanaadamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Malaika Jibril ndiye mhusika mkuu wa kupeleka wahyi kwa mitume na manabii.
Rejea Qur’an (81:19-20), (16:2) na (11:69-73).

(b)Kumchunga na Kumlinda kila mtu na kuandika amali zake nzuri na mbaya.
Kila mtu anakundi la malaika nyuma na mbele yake kumlinda na mambo yaliyo nje na uwezo wake. Pia kuna malaika wa kulia anayeandika mema na wa kushoto anayeandika maovu ya mtu.
Rejea Qur’an (82:1-12), (50:17-18) na (13:11).

(c)Kuwaombea Waumini maghufira kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Hawa ni malaika ambao huzunguka katika makundi ya waumini anapotajwa ndani yake Mwenyezi Mungu (s.w) au kusomwa Qur’an Tukufu.
Rejea Qur’an (40:7), (42:5) na (17:78).

(d)Kuwasaidia waumini katika vita vya kupambana na maadui wa Allah (s.w).
Pindi waumini wanapopigana katika kusimamisha haki, Mwenyezi Mungu (s.w) huteremsha malaika kuwasaidia.
Rejea Qur’an (3:123-126) na (8:12).

(e)Kuwaangamiza watu waovu waliopindukia mipaka.
Watu waovu waliopindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu (s.w) wakaonywa muda mrefu na wasionyeke huangamizwa na malaika maalum.
Rejea Qur’an (11:81-83).

(f)Kutoa roho za viumbe.
Malakul-Maut ndiye mhusika mkuu na wengineo katika kutoa roho za viumbe.
Rejea Qur’an (32:11).

(g)Kuzihoji, kuzistarehesha au kuziadhibu roho za wafu kaburini.
Malaika wanaohusika na kazi hii ni Munkar na Nakir.

(h)Kupuliza Parapanda siku ya Qiyama.
Mipulizo ya Parapanda katika kufisha na kufufua viumbe siku ya Qiyama itafanywa na malaika Israfil.
Rejea Qur’an (39:68).

(i)Kuwaliwaza na kuwakaribisha watu wema peponi.
Hili kundi jingine la malaika watakaofanya kazi hiyo siku ya Qiyama.
Rejea Qur’an (41:30-32) na (39:73).

(j)Kuwasimanga na kuwaadhibu watu waovu motoni.
Kuna kundi la malaika watakaokuwa wanaadhibu watu waovu motoni. Mlinzi mkuu wa milango ya moto ni Malaika Maalik.
Rejea Qur’an (25:22), (74:26-30) na (43:77).

(k)Kumtukuza na kumsifu Mwenyezi Mungu (s.w).
Kuna kundi la malaika maalum kwa kazi hii tu.
Rejea Qur’an (40:7).

Maana ya Kuamini Malaika katika maisha ya kila siku.
Zifuatazo ni athari za muumini wa kweli juu ya imani ya malaika katika kila kipengele cha maisha ya kila siku;

Kwanza, imani ya kweli juu ya Malaika humuepusha na kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w) na viumbe wake hasa wale wasioonekana kama Malaika, majini, n.k.
Rejea Qur’an (37:149-154), (43:16-19) na (21:26-27).

Pili, imani juu ya malaika huchochea mja kufanya ibada kwa bidii na kujiepusha na maovu na machafu ili kupata cheo kama malaika au zaidi.

Tatu, imani juu ya malaika pia humfanya mtu kuepuka kufanya maovu popote alipo na muda wowote kwa kujua kuwa yupo pamoja na malaika.

Nne, Mja anapoamini kuwa malaika huandika na kuhudhurisha vitendo vyake kwa Mwenyezi Mungu (s.w), hufanya bidii katika kufanya mema zaidi na kuepuka maovu kadri ya uwezo wake.

Tano, Muumini anapoamini kuwa malaika humuombea maghufira kwa Mwenyezi Mungu (s.w), hufanya bidii katika kuzidisha mema na kuepuka maovu kadri awezavyo ili kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu (s.w) zaidi.
Rejea Qur’an (17:13-14) na (18:49).


                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 830


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula Mbegu za maboga
Soma Zaidi...

quran na sayansi
Soma Zaidi...

AMRI YA KUMFUATA MTUME (s.a.w9)
Amri ya Kumfuata Mtume (s. Soma Zaidi...

fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...

Kitabu Cha Dua 120
Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe vyote. Soma Zaidi...

2.3.Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w Quran, tawrat, Zabur na injili
2. Soma Zaidi...

Kafara ya mwenye kuvunja masharti ya ihram
Soma Zaidi...

Maandalizi ya kujiandaa mwenyewe kabla ya kufa ama kufikwa na mauti (kifo)
Kwakuwa kila mtu anatambua kuwa ipo siku atakufa hivyo ni vyema kuanza kujiandaa mapema. Soma Zaidi...

Nguzo 6 za iman ya dini ya kiislamu kwa mafundisho ya quran na sunnah
Nguzo za Imani. Soma Zaidi...

NASAHA ZANGU NNE KWAKO KUHUSU QURAN, MAUTI, DUA NA MENGINE
Soma Zaidi...

Taratibu za mahari katika uislamu
Soma Zaidi...

Hukumu ya zakat Al-Fitir na namna ya kuitoa zaka ya fitir
Soma Zaidi...