picha

michezo

michezo ni katika mambo ambayo mtu anatakiwa asiyakose.

michezo

michezo ni katika mambo ambayo mtu anatakiwa asiyakose. Na michezo ni muhimu si kimwili tu bali pia kiakili. Pia itambulike kuwa kwa mujibu wa Umoja wa mataifa michezo ni haki ya mtoto. Yaani ni kosa kumzuilia mtoto kucheza. Michezo inapewa kipaumbele sana kwa watu wa rika zote na jinsia zote.

michezo inatakiwa pia ifanywe kwa kulingana na mwili, afya, jinsia pamoja na umri. Kuna michezo ambayo watoto hawaruhusiwi kuicheza, pia ipo ambayo inazuia jinsia yaani jinsia fulani haichezi michezo fulani. Halikadhalika afya ya mtu itamzuilia asiweze kucheza baadhi ya michezo.

hakikisha unacheza kiasi cha kukutoa jasho. Na pia ni vyema ukakaa track suti, vazi hili linapendekezwa liwe na mikono mirefu pamoja na miguu mirefu. Jambo la kizingatia hapa uhakikishe jasho linamwagikia na kukaukia mwilini. Hii husaidia katika kuunguza mafuta mwilini.

Michezo ipo ya aina nyingi sana, unaweza ukawa unaruka kamba. Na hili ni katika mazoezi mazuri kwa anayetaka kutafuta pumzi na kuwa mwepesi kama kukimbia. Jogging, pushap mpira na baadhi ya mazoezi mengine mengi ya viungo. Pia kumbuka yapo mazoezi ya akili kama vitendawili, nahau na methali ama kucheza gemu za kompyuta ama simu.Kama nilivyotangulia kusema michezo ina faida za kimwili na kiakili. Ukuaji ulio bora wa akili kwa watoto unachangiwa zaidi na vyakula, kurithi na pamoja na michezo. Watu wa rika zote wanahitaji kucheza ili waweze kuchangamka kimwili na kiakili. Michezo huweza kumuepusha mchezaji na athari ya maradhi kama kisukari, saratani na baadhi ya maradhi mengine.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Zaidi Main: Post File: Download PDF Views 2122

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 web hosting     πŸ‘‰2 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰3 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰5 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

uwanja wa burudani

Jifunze mengi kuhusu Afya, kuwa nasi kwenye makala hii hadi mwisho.

Soma Zaidi...
uwanja wa burudani

Jifunze mengi kuhusu Afya, kuwa nasi kwenye makala hii hadi mwisho.

Soma Zaidi...
VITABU VYA BURUDANI: CHEMSHABONGO, HADITHI, SIMULIZI, NA VICHEKESHO

Soma hadithi za burudani na mashairi, cheka na furahia zaidi katika hadithi zetu

Soma Zaidi...
MASHAIRI

UWANJA WA MASHAIRI Β  Β  Β  Β  Β  Β  Β UWANJA WA ELIMU YA MASHAIRI Bofya link hapo chini kuanza kusoma 1.

Soma Zaidi...