Katika somo hili utakwenda kujifunza Asili ya waarabu na kusambaa kwao katika bara arab
HISTORIA YA WATU WA MAKA KUTOKA KWA NABII IBRAHIM (A.S)
Nabii Ibrahim (AS), pia anajulikana kama Khalilu-Llah" (خليل الله) yaani rafiki wa Allah, anachukuliwa kuwa babu mkubwa wa Nabii Muhammad ﷺ, ambaye alifuata ari ya babu yake katika kuamini na kuhubiri aina safi zaidi ya upwekeshaji wa Mwenyezi Mungu. Tarehe ya kuzaliwa kwake haijulikani ingawa kuna maoni mengi yanayotofautiana kwa kiasi kikubwa.
Nabii Ibrahim aliamrishwa na Allah kumleta Mke wake Hajar na mtoto wake Ismail na kumucha jangwani. Alimuacia kisi kidogo cha chakula na maji. Kiasi kile hakikudumu kwa muda mrefu kikaisa. Jangwani hapo hakukuwa na mti, wala maji. Baada ya maji kuisha Ismail akapata kiu kikali na akaanza kulia kwa kiu, ili aweze kupata maji. Mama yake akawa anakimbia kati ya vilima wiviwli akipanda juu kuangalia kama ataona bonde lenye maji karibu. Vilima hivyo vilijulikana kama Swafa na Marwa ambapo Mpka leo vinaonekana na mahujaji wanatekeleza Ibada ya hija kwa kutembea kwenye vilima hivi.
Wakati huo yeye alizunguruka kati ya vilima hivyo viwili huku Ismail alinendelea kuhangaika na kiu. Basi akawa anapiga chini miguu yake. Ndipo Allah akaamrisha patoke maji chini ya miguu. Inasemekana ni Malaika Jibril alipiga pale chini kwa mbawa zake. Basi mama Ismail akarejea na kukuta kuna maji. Ndipo akaanza kuzungusia kisima hiko. Kwa kuwa kisima hiko kilikuwa na sehemu pekee inayotoa maji jangwani hapo basi kuna baadhi ya wasafiri waliokuwa wakipita hapo kibiashara wakitokea Yemen walipita na kuomba maji. Kisima hiki kimejulikana kama zamzam na sababu ya jina hili ni kuwa pale alipokuwa anajuia maji yasisambae akama anasema zam zam kwa lugha yake alimaanisha tulia tulia. Lugha hii ina asili na Africa ambapo Hajra alitokea.
Mama Ismail akawa anatoa huduma ya maji kwa wasafiri. Wasafiri wale wakaanza kuweka makazi na hatimaye mji mdogo ukajengeka. Sehemu hiyo ndio Mkkah ya leo, na kisima hiko ndio kisima cha Zamzam ambacho mpaka leo kipo. Basi Ismail na Mama yake waliishi hapo, huku Nabii Ibrahim akama anakuja kuwatembelea mara kwa mara.
Kisima cha Zamzam kiliendelea kuwepo kwa mamia ya miaka. Ila baadaye kilitoweka. Kutoweka kwa kisima hili kunazungumziwa nikwa sababu ya Mdhambi waliokuwa wakiyafanya watu wa kabila la Jurhum. Pia historia inaelezwa kuwa watu hawa walifukuzwa Maka hivyo wakakifukia kisima hiki pamoja na mali zao na baadhi ya vitu vingine. Hvyo kwa miaka mingi Makkah ilikuwa haina kisima hiko. Ilifikia wakati hata watu wakasahau kabisa sehemu ambapo kisima hiko kilikuwepo. Pia kulikuwa na habari za kuzusha kuhusu yeyeto ambaye atakifukuwa kuwa anaweza kupatwa na jambo baya.
Mwanawe, Ismail na mama yake Haajar, walikaa katika bonde la Makkah pamoja na kabila la Yemeni, Jurhum. Ilikuwa Makkah ambapo baba na mwana walijenga Ka'bah, wakinyanyua nguzo zake kwa mujibu wa amri ya Allah na kisha wakiita watu kufanya hija. Ismail mwenyewe alikuwa na wana kumi na wawili kutoka kwa binti wa Mudad (mkuu wa kabila la Jurhum), ambao majina yao ni Nabet, Qidar, Edbael, Mebsham, Mishma', Duma, Micha, Hudud, Yetma, Yetour, Nafis na Qidman, ambao mwishowe waliunda makabila kumi na mawili yaliyokaa Makkah na kufanya biashara kati ya Yemen, Shaam, na Misri.
Baadaye, makabila haya yalienea kote kwenye peninsula, wakati mwingine hata nje ya mipaka yake. Kati ya makabila kumi na mawili, yote yalitoweka isipokuwa uzao wa wawili: Nabet na Qidar. Wanabatei (au wana wa Nabet) walijenga ustaarabu uliofanikiwa kaskazini mwa Hijaz, wakifanya Petra (katika siku hizi Jordan) kuwa mji mkuu wao hadi Warumi walipokuja na kushinda ufalme wao. Uzao wa Qidar, waliishi kwa muda mrefu Makkah wakiongezeka kwa idadi, hasa kupitia 'Adnan na mwanawe Ma'ad ambao Waarabu wa 'Adnani walijinasibisha kwao. 'Adnan alikuwa babu wa ishirini na moja katika mfululizo wa ukoo wa Nabii. Nizar, mwana pekee wa Ma'ad, alikuwa na wana wanne ambao walijitenga katika makabila manne makubwa; Eyad, Anmar, Rabi'a na Mudar. Makabila ya Mudar yalijitenga katika matawi mawili makubwa: Qais 'Ailan bin Mudar na tawi la Elias bin Mudar. Kati ya Elias bin Mudar walikuwa Tamim bin Murra, Hudhail bin Mudrika, Banu Asad bin Khuzaimah na tawi la Kinana bin Khuzaimah, ambao kutoka kwao walikuja Quraysh, uzao wa Fahr bin Malik bin An-Nadr bin Kinana.
Quraysh walijitenga katika makabila mbalimbali, maarufu zaidi walikuwa Jumah, Sahm, 'Adi, Makhzum, Tayim, Zahra na matawi matatu ya Qusai ibn Kilab: 'Abd Al Dar bin Qusai, Asad bin 'Abdul 'Uzza bin Qusai na 'Abd Manaf bin Qusai. 'Abd Manaf alijitenga katika makabila manne: 'Abd Shams, Nawfal, Muttalib na Hashim. Ni kutoka familia ya Hashim ambapo Allah alimchagua Nabii wa mwisho na Mtume, Muhammad ﷺ mwana wa 'Abdullah mwana wa 'Abdul Muttalib mwana wa Hashim, rehema na amani za Allah ziwe juu yake.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-07-27 18:14:32 Topic: Historia ya Mtume Muhammad (s.a.w) Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 596
Sponsored links
👉1
kitabu cha Simulizi
👉2
Kitabu cha Afya
👉3
Madrasa kiganjani
👉4
Kitau cha Fiqh
👉5
Simulizi za Hadithi Audio
👉6
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Jaza maswali yote ama baadhi kisha bofya kitufe za kutuma majibu hapo chini.
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 61: Matukie mengineyo kwneye safari ya Taif
Baadhi ya matukio mengine yaliyoteokea kweye safari hii ya Tfai Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 59: Mwaka wa huzuni
Baada ya kupambana kwa Muda Mrefu kumsaidia Mtume Muhammad, na hatimaye Mzee Abu Talib na Khadija Mke wa Mtume wanafariki Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 15: Historia ya Abdallah baba wa Mtuume Muhammad
Katika somo hili utakwenda kujifunza historia fupi ya Abadallah baba wa Mtume Muhammad ﷺ Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 32: Mwanzoni mwa ibada ya Swala
Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu mwanzoni mwa kuamrishwa ibada ya swala na vipi iliswaliwa. Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 8: Kulelewa kwa Mtume Muhammad ﷺ na Halima
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuusu malezi na makuzi ya Mtume Muhammad ﷺ akiwa kwa bibi Halima Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 27: Kushuka tena kwa Wahyi
Baada ya kukatika kwa Wahyi kwa muda wa masiku kadhaa hatimaye Jibril akaleta tena wahyi kwa mara nyingine. Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 38: Taharuki yaingia Mjini Mkkah
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu yaliyotokea baada ya watu wa Mkkah kulinganiwa kwenye dini kwa mara ya kwanza Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 24: Katika pango la Hira
Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu yaliyojiri katka pango la Hira kabla ya kupokea utume Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 41: Mbinu za kukomesha kuenea kwa uislamu
Katika somo hili utakwenda kujifunza mambo yaliyofanyika katika harakati za kukomesha kuenea kwa uislamu. Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 53: Kuslimu kwa Hamza bin Abdul-Muttalib
Hapa utajifunza historia ya kuslimu kwa Hamzah bin Abdul-Muttalib. Soma Zaidi...