Somo hili linazungumzia dua muhimu zilizotajwa katika Qur’an zilizosomwa na Hawariyuna – wafuasi wa kweli wa Nabii Isa (a.s.). Tutaziona kama kielelezo cha imani, utiifu na unyenyekevu mbele ya Allah.
Hawariyuna walikuwa wafuasi wa karibu wa Nabii Isa (a.s.) waliomsadia kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu. Walijulikana kwa kusalimisha nafsi zao kwa Allah na kwa kumtii Mtume wake. Katika Qur’an, dua zao zimetajwa ili kutufundisha mafunzo ya subira, imani ya dhati na kujisalimisha kwa Allah.
dua ya kuomba kujumuishwa na mashahidi
رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنْزَلْتَ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ
(Āl-ʿImrān 3:53)
Tafsiri ya Kiswahili:
“Mola wetu Mlezi! Tumeyaamini uliyo yateremsha, na tumemfuata huyu Mtume, basi tuandike pamoja na wanao shuhudia”
Hii inaonyesha imani ya Hawariyuna kwa wahyi wa Allah na ufuasi wao wa dhati kwa Nabii Isa (a.s.). Waliomba wasiwe tu waumini wa kawaida, bali waandikwe miongoni mwa mashahidi wa ukweli wa dini.
dua ya kuomba meza kutoka mbinguni (Dua hii aliomba Nabii Isa pindi wanafunzi wake walipohitaji miuziza)
اللَّهُمَّ رَبَّنَا أَنزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِّأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِّنكَ ۖ وَارْزُقْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ
(Al-Mā’idah 5:114)
Tafsiri ya Kiswahili:
“...Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku..”
Dua hii inaonyesha uhitaji wa Hawariyuna wa dalili ya dhahiri kutoka kwa Allah, na pia shukrani yao kwa neema ya chakula na riziki.
Imani thabiti: Dua ya kwanza inatufundisha kuomba uthabiti katika imani na kuhesabiwa miongoni mwa mashahidi wa haki. Katika maisha yetu ya kila siku, tunaweza kuiomba Allah atufanye mashahidi wa haki kazini, majumbani na katika jamii.
Shukrani na riziki: Dua ya pili inatufundisha kumshukuru Allah kwa riziki na kuomba kila tunachopata kiwe ni baraka. Katika maisha ya kila siku, tunaweza kuitumia tunapopokea neema, au tunapotaka riziki yenye baraka.
Dua za Hawariyuna zinatufundisha misingi miwili mikuu: kuamini kwa dhati na kushukuru neema za Allah. Waliomba kwa unyenyekevu, wakitambua udhaifu wao na kuonyesha utiifu wao kwa Nabii Isa (a.s.). Hii ni funzo kwetu kwamba dua ni chombo cha kuimarisha uhusiano wetu na Allah katika kila hali.
Umeionaje Makala hii.. ?
Nabii Ibrāhīm (a.s.) ni mmoja wa Mitume wakuu na alipewa cheo cha Khalīlullāh (rafiki wa karibu wa Allah). Alijulikana kwa jihadi yake ya kuhubiri Tawḥīd katika jamii iliyozama kwenye ibada ya sanamu. Alipitia mitihani mikubwa kama kuchomwa moto, kuamrishwa kumchinja mwanawe, na kuhamishwa kutoka kwa watu wake. Dua zake zimehifadhiwa kwa wingi ndani ya Qur’an, zikionesha upendo, unyenyekevu, na kujisalimisha kwa Allah.
Soma Zaidi...Nabii Idrīs (a.s.) alikuwa miongoni mwa Mitume wa mwanzo baada ya Adam na Sheth. Alijulikana kwa elimu, uvumilivu na ibada. Qur’an imemsifu kwa ukweli na hadhi ya juu, japokuwa dua zake hazikuelezwa kwa wazi. Riwaya za kale zinahusisha dua zake na maombi ya hekima na uongofu.
Soma Zaidi...Somo hili linazungumzia dua ya Mariam binti Imran, mama yake Nabii Isa (a.s.), aliyekuwa mwanamke mtukufu na msafi. Dua zake zilizotajwa katika Qur’an zinatufundisha unyenyekevu, utiifu na kujisalimisha kwa Allah katika nyakati muhimu za maisha.
Soma Zaidi...Nabii Adam (a.s.) ndiye baba wa wanadamu na Nabii wa kwanza. Alikosea kwa kula mti uliokatazwa, kisha akatubia kwa dua yenye unyenyekevu na Allah akamsamehe. Dua hii inatufundisha namna ya kurejea kwa Allah tunapokosea.
Soma Zaidi...Katika somo hili tunajifunza kuhusu Nabii Ya‘qūb (a.s.), maisha yake, changamoto kubwa alizokutana nazo katika malezi ya wanawe na mitihani ya kifamilia, dua zake alizomuelekea Allah, na jinsi alivyokuwa mfano wa subira. Pia tutaona namna dua zake zilivyokuwa kwa muundo wa moja kwa moja na pia wa kuashiria.
Soma Zaidi...Mfululizo huu utachambua dua za Mitume na Manabii waliotajwa katika Qur’an na Sunnah, tukielewa muktadha wake wa kihistoria, majibu ya Allah, na mafunzo yake. Lengo ni kutupa mwongozo wa namna ya kutumia dua hizo katika maisha yetu ya kila siku.
Soma Zaidi...Somo hili linamzungumzia Nabii Sulayman (a.s.), mwana wa Dawud (a.s.), ambaye Allah alimpa ufalme mkubwa, elimu ya ajabu, na uwezo wa kuongoza hata viumbe wasioonekana kama majini na wanyama. Qur’an inarekodi dua zake muhimu, zikihusu msamaha, ufalme, na shukrani kwa neema alizopewa.
Soma Zaidi...Somo hili linazungumzia Nabii Ayyub (a.s.), miongoni mwa Mitume waliokabiliwa na mitihani mikubwa ya afya na mali. Tutazungumzia changamoto alizokabiliana nazo, dua aliyoiomba kwa Allah, majibu aliyoyapata, mafunzo, na jinsi tunavyoweza kutumia somo hili katika maisha yetu ya kila siku.
Soma Zaidi...Nabii Hūd (a.s.) alitumwa kwa kaumu ya ʿĀd waliokuwa na nguvu kubwa, lakini wakawa na kiburi na ukaidi dhidi ya amri ya Allah. Walimkataa Hūd na kuendelea na shirki na dhulma. Katika Qur’an, tunapata dua na maneno yake ya kumtegemea Allah mbele ya upinzani. Dua yake ni mfano wa ujasiri na imani ya dhati kwa Allah.
Soma Zaidi...Somo hili linamzungumzia Nabii Shu‘ayb (a.s.), aliyejulikana kwa ujumbe wa haki na busara kwa watu wa Madyan. Tutazungumzia changamoto alizokabiliana nazo, dua aliyoomba kwa Allah, muktadha wa dua hiyo, majibu, mafunzo, na matumizi yake katika maisha ya kila siku. utangulizi
Soma Zaidi...