BLOGGER somo la 2: Jinsi ya kuandika post na kuiboresha pamoja na kuidhibiti
Katika post hii utakwend akujifunza jinsi ya kuandika post, kuisimamia na kuoboresha.
Kama unatumia simu upande wa kushoto kuna menu hapo bofya utaletewa list ya menu. Bofya palipoandikwa NEW POST. na kama unatumia kompyuta bofya palipoandikwa NEW POST upande wa kushoto kwa juu.
Kama unatumia simu ukurasa utakaofunguka utakuwa tofauti na wanaotumia kompyuta. Hata hivyo nitafafanua kwa manufaa ya wote wanaotumia simu na kompyuta. Hapo chini naleta picha mbili moja kwa wanotumia simu na ingine ni kwa wanaotumia kompyuta.
Kwa watumiaji simu
Kwa watumiaji kompyuta
Hapo kwenye namba 1 ndipo utakwenda kuandika kichwa cha habari cha hiyo post yako.
Kwenye namba 2 ni kwa ajili ya ku preview yaa ni kuangalia jinsi ambavyo post yako itaonekana na wasomaji wako kabla hujaipost
Kwenye namba 3 hapo ndipo utakapobofya pindi unapomaliza. Ukibofya hapo post yako inakuwa live. Hivyo watu wote wataweza kuiona.
Hiyo ni menu ambapo kila unachokiona hapo kitakusaidia katika kuboresha muonekano wa post. Kwa wanaotumia siku buruza huo mstari utakuonyesha menu zaidi.
Kwenye nmaba 4 hapo hutumika ku edit html code za hiyo post yako. Kama unataka kuongeza maboresho kwa kuweka code za html, css na javascript kwenye post yako, basi hapo ndio sehemu inayotumika.
Menu ya vifaa vya uandishi
Sasa ngoja tuone baadhi ya sehemu muhimu katika uandishi wa post yako kwenye blog.
Ni kwa ajii ya kufanya herufi kuwa bold
Ni kwa ajili ya kufanya maandishi kuwa italics
Ni kwa ajili ya kupigia mstari maandishi
Kwa ajili ya kukata maadhishi
Kwa ajili ya kuweka rangi kwenye maandishi
Kwa ajili ya kuweka rangi ya background
Kwa ajili ya kuweka link
Kwa jili ya kuweka picha
Kwa ajili ya kuweka video na audio
Kwa ajili ya kuweka emoj
Kwa ajili ya kupangilia muonekano wa paragraph
Kwa ajili ya kupangilia mtiririko wa namba
Kwa ajili ya kunukuu
...
Download App Yetu
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.