ALADINI NA BINTI WA MFALME.

ALADINI NA BINTI WA MFALME.

ALADINI NA BINTI WA MFALME.


ALADINI NA BINTI WA MFALME.



Baada ya pango kuziba Aladini alianza kupata taabu sana. Wale nyuki walikuwa wakimuuma, kale kamwanga kadogo ka pete hakakuonekana tena. Ukweli ni kuwa yule mzee alikuwa ni mchawi aliyesoma kuhusu uajiri wa eneo hili, alitambuwa kuwa ukipata mshumaa tu utakuwa na nguvu ya ajabu sana. Hakuna mchawi wala mganga atakayekutia mkono. Kulingana na maelezo ya hiko kitabu huwezi kuuchukuwa huo mshumaa mwenyewe, lazima upokee kutoka kwa mtu mwingine vinginevyo ni kifo. Pia atakayeuchukuwa hatakiwi kutoka humo ni lazima afie humo, vinginevyo ni kifo. Hatahivyo atakayeuchukuwa anatakiwa awe ni kijana wa kiume asiyemjuwa mwanamko hata (yaani hajawahi ku ') hivyo ndio maana Aladini alikuwa ni chaguo pekee.


Sasa mzee mchawi alivyoona Aladini hataki kumpa mshumaa alijuwa kuwa vinginevyo ni kifo chake. Alichofanya ni kuziba shimo ili Aladini afe kabisa iiwe ni kafara yeke. Ila jambo la hatari ni kuwa mchawi alisahau kuchukuwa pete yake kwa Aladini. Na hiki ndio kitu pekee sasa kinachoweza kumtoa Aladini. Ndani ya pango Aladini aliendelea kulia sana. Aladini alijuta na akatamani kula lakini hakuna cha kukila. Nyuki kadhaa waliweza kumuuma na kumuongezea maumivu badala ya njaa aliyo nayo. Siku ya kwanza ilipita ola bila Aladini kuliona jua wa la kula kitu, siku ya pili nayo ikabita. Aladini sasa amechoka sana, kiu na njaa vinamsumbuwa, kiza na joto yote yanampa taabu.


Aladini aliendelea kuomba dua kwa Mungu mlezi na aliendelea kutubu. Aladini alitambuwa madhambi yake yote na kuahidi kutokurudia endapo Mungu atamtoa salama kwenye pango lile la kifo. Machozi ya aladini yaliweza kutotesha mavazi yake kwa siku ya kwanza, lakini sas aAladini hakuweza tena kulia kwa machozi. Maana hana maji ya kutosha kuzalisha machozi mwilini. Hakika Aladini yupo katika hali ngumu sana. Kwa upande mwingine mama aliamini kuwa Aladni yupo hatiani, na hii ni baada ya kukumbuka kuwa shemeji yake aliambiwa kuwa na kovu kubwa la jeraha kwenye paji la uso wake. Lakini shemeji huyu hana hilo kovu.


Mama aligundua kuwa mwanae yupo hatariri. Mama aliendelea kuomba dua na kumtafuta mwanaye kila alipojuwa. Kwa upande wa mchawi baada ya kuondoka pale alipotea kabisa, alipokumbuka kuwa pete ya ajabu hana, alishindwa kurudi. Kwa mujibu wa kitabu alichosoma ni kuwa alitakiwa kurudi pale baada ya kiaka 3, kila jaribio likifeli anatakiwa angoje miaka mitatu. Na tayari hili sasa ni jaribio la 5. na kila alipofeli kijana alipoteza maisha, na saa ni zamu ya Aladini. Habari ya Aladini ni tofauti kidogo na wenziwe, maana wenziwewaligoma kutoa mshumaa lakini walirudisha pete baada ya kulaghaiwa. Lakini Aladini alibakiwa na pete ya mchawi.
Katika kiza cha pango Aladini hakutambuwa muda, kuwa ni asubuhi ama jioni. Wakati alipokuwa akiomba dua alikuwa akisuguwasugwa ile pete, ghafla lijini kubwa likatokea. Pango zima likawa na mwangaza. Lijini likasea kuwa 'mimi ndiye mtumwa wa hiyo pete, nambie unataka nini nikusaidie' Aladini kwa ujasiri akatamka kuwa 'nitoe hapa kwenye pango' punde Aladini akajikuta yupo nje. Alikimbia sana na alipofika nyumbani ilikuwa ni majira ya asubuhi. Aladini alipofika mlangoni kwao Aliangka na kupoteza fahamu. Ama yake akampepea na kumpahuduma ya kwanza. Alipozinduka Aladini alihitaji kitu cha kula. Mama akamueleza 'mwanangu hapa sina hata pesa, ila kuna nguo hizi niende sokoni nikauze tupate pes'


Aladini aliposikia kuwa ndani hakuna pesa ya kula alikumbuka kuwa mfukoni anamshumaa ule aliochukuwa kule pangoni. Aladini akamueleza mama yeke kuwa kuna mshumaa amekuja nao atakwenda kuuza wapate pesa. Aladini akauchukuwa ule mshumaa na kuanza kuusafisha na maji maana ni mchafu sana hivyo usingenunuliwa. Wakati anausuguwa ghafla harufu ya manukato ikazagaa ndani kwao Aladini, mwangaza hafifu ukatokea ukutani na binti membo akatokea kisha ananena 'mimi ndiye mtumwa wa huo mshumaa, nitume chochote nitakutekelezea' Aladini bila woga akamueleza niletee chakula cha kula mimi na mama'


Punde masinia mawili ya dhahabu yaliyofunikwa wa makawa yenye rangi nzuri. Vishikizo vya juu vya makwa vilikuwa ni sanamu la huyu jini wa kike. Aladini alipofunua kila sinia lilikuwa na sahani moja, bilauri za dhahabu, birika moja na vikombe viwili. Kikombe kimoja kilikuwa na asali ya dhahabu, kikombe kingine kilkuwa na juisi ya matunda. Aladini hakujuwa ni matunda gani maana ilikuwa na mchanganyiko wa rangi utadhani mikia ya tausi wa uhabeshini.bilauri ya maji ilikuwa ni ya madini ya fedha. Visahani vidogo vya kuwekea vikombe vilikuwa ni vipande vya lulu vyenye rangi nzuuri. Haya yote yaliendelea kumsataajabisha Aladini. Aladini alistaajabu zaidi alipoona kijiko, kwani kilikuwa ni cheusi, jambo ambalo hakulitarajia.


Aladini aliposhika kijiko, kilianza kuangaza chumba kizima mwangaza huu ulimkumbusha ule wa kwenye lile pango. Aladini akaanza kukumbuka kila alichokiona kwenye lile pango. Na kila alipokumbuka vilikuwa vikionakena ukutani. Punde alipokichia kile kijiko mambo yalitulia. 'mmmh' aliguna Aladini, mguno ambao ulimshitua mama aliyekuwa anajiandaa kwenda sokoni kuuza vingui alivyoshona wapate cha kukila. 'una nini Aladini' ni swali la mama kwa mwanaye kipenzi. Mama alipotoka alikuta mambo yamebadilika, harufunzuri ya vyakula. Kufunua alikuta chakula kizuri, chakula ambacho huwa kinaliwa na wafalme na mawaziri.


Aladini aakamkaribisha mama na kumwambia asiulize zaidi ya kula maswali baadaye. Aladini alizungumza maneno hayu huku paja la kuku wa kuoka likiwa mdomoni. Kwa njaa alifundia na kunywa juisi na kulamilizia na asali. Alipomaliza alimsimulia mama kila kitu. Kisha aladini akachukuwa vitu vyote vile na kwenda kuviuza ila kijiko hakukiuza, alitaka ipakie kumbukumbu. Pesa laiyoipata aliweza kuitumia kwa muda wa miezi kadhaa.


Maisha ya Aladini yakarudi kawaida, na Aladini hakutaka kutumia nguvu zile kwa muda mrefu. Na aliamuwa kuishi kama alivyoishi zamani. Hakukuwa na mabadilio yeyote zaidi ya kuwa alikuwa ni mtiifu na mwenye kusaidia kazi mzazi wake. Aladini aliweza sasa kushona nguo kwa umaridadi mkubwa kama baba yake. Siku moja mfalme wa nchi alitangaza kuwa watu wote wasitoe ndani maana binti mfalme atapita mtaani kwenda bwawani kuoga. Ilikuwa ni kawaida yake kila miezi sita anakwenda kuoga bwawani. Hivyo siku hiyo hakuna anayeruhusiwa kutoka.


Aladini alitaka kujuwa sura ya binti mfalme. Alichofanya ni kwenda bwawani na kujificha juu ya mti. Baada ya muda binti mfalme akaja bwawani. Aladini alitaka kuziba sura akiamini kuwa binti mfalme amekuja kuoga hivyo atavua nguo. Ukweli ni kuwa binti mfalme hakuwa akioga ila ni kuchezea maji na wadogo zake na kuchezea mchanga mweupe wa bwawani. Aladini alishuhudia kila alichokiona, aladini alipendezwa ghafla na sura ya binti. Katika kucheza alikuja ndege mzuuri na kumtua binti kwenye kichwa chake. Binti alitabasamu na kufurahia, ndege yule alipuruka na kuelekea juu ya mtu ambapo Aaladini amejifucha. Macho ya Aladini yakakutana na binti, 'mmmmh huyu kaka nzuri sana' ni maneno yaliyotoka moyoni mwa binti..


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 108

Post zifazofanana:-

jamii muongozo
Haja ya Mwongozo kutoka kwa Allah (s. Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

Kitabu cha Afya 02
Kama tulivyosema hapo juu kuwa afya ni kuwa mzima kimwili na kiakili. Soma Zaidi...

JIFUNZE DINI YA KIISLAMU, quran, hadithi, tawhid, tajwid, sira na fiqh
Jifunze mengi kuhusu dini hapa Soma Zaidi...

Siku za kupata mimba
Nitakujulisha siku ya kupata mimba na sifa zake, na namna ya kuweza kuitafuta Soma Zaidi...

JARIBIO LA TATU LA A LADINI
Soma Zaidi...

Kuenea kwa dhana ya udhibiti uzazi na uzazi wa mpango
Kustawi kwa Kampeni ya Kudhibiti UzaziMiongoni mwa sababu zilizosaidia kustawi kwa kampeni hii ni matokeo ya mapinduzi ya viwanda (Industrial revolution) ya huko Ulaya. Soma Zaidi...

VYAKULA VYA FATI, PROTINO NA WANGA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

HADITHI YA BINT WA PILI MWIMBA MASHAIRI MWENYE MAKOVU
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI WA PILI MWIMBA MASHAIRI MWENYE MAKOVU. Soma Zaidi...

kitabu cha matunda
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

Tafsir ya suratul quraysh na mafuzoyake
Soma Zaidi...

Swala ya Kuomba Toba (tawbah) na namna ya kuiswali
Soma Zaidi...