Twahara

FIQH 1.

Twahara

FIQH
1.TWAHARA
Twahara ni neno la kiarabu lenye maana ya usafi au unadhifu. Na neno hili kisheria ni kuondoa yale yanayomzuilia mtu kuswali ambayo ni katika hdathi na najisi, kwa kutumia maji au vinavyosimama badala ya kukosekana kwa maji kama udongo.

Kuondoa najisi ni jambo la wajibu pindi mtu anapokumbuka na akiwa na uwezo wa kufanya hivyo. Kama aliposema Allah kumwambia Mtume (s.a.s): 'na nguozako uzitwaharishe' (surat muzammil: 4). Na Mtume ' ' ' amesema 'haikubaliwi swala (iliyoswaliwa ) bila ya udhu'.

Kuwa twahara tofauti na kuwa ni jambo lililohimizwa sana kwenye uislamu hata Mtume ' ' ' akasema: 'uislamu ni usafi' ila pia kuna faida nyingi sana tunazipata kwa kutekeleza jambo hili:

1.Twahara ni sharti katika kuswihi kwa sala. Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Mtume ' ' ' amesema:'haikubaliwi swala ya mtu aliyehuduthi (aliyejamba) mpaka atawadhe' (Bukhari na Muslim)

2.Allah amewasifia sana watu ambao wanakuwa twahara. Amesema Allah 'hakika Allah anawapenda wenye kutubia na anawapenda wenye kuwa twahara' (Surat baqara aya 222).

3.Kuwa twahara ni sababu ya kutokuadhibiwa kaburini. Ni kuwa watu ambao hawajikingi na najisi kama mkojo na hawajitwaharishi wataadhibiwa makaburini. Imesimuliwa hadithi na Ibn Abas kuwa Mtume ' ' ' alipita kwenye makaburi mawili kisha akasema : 'hakika watu hawa (waliozikwa hapa ) wanadhibiwa, na si kwa makosa makubwa bali kwa hakika huyu mmoja alikuwa hajisafishi anapokojoa.'.' (Ibn Majah N Abu daud na isnad ya hadithi ni sahihi)

Aina za twahara.
Basi tambua kuwa twahara ip katika makundi makuu mawili ambayo ni:

1.twahara haqiqiya: nayo ni ni kujitwaharisha na khabathi yaani najisi na inaweza kuwa kwenye mavazi au mwili.

2.Twahara hukmiyah: nayo ni kujitwaharisha na hadathi na hii inahusiana na mwili tu na aina hii imegawanyika katika makundi matatu ambayo ni:-
A)Twahara kubwa; ambayo ni kuonga (josho la kisheria)
B)Twahara ndogo; nayo ni kutawadha yaani udhu
C)Twahara iliyo badala ya aina mbili zilizotangulia nayo ni kutayamam, yaani kujitwaharisha kwa kutumia udongo.


                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 544


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

KUTOKA KWENYE KISIMA MPAKA KUWA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa KUTOKA KWENYE KISIMA MPAKA KUWA MFALME. Soma Zaidi...

NURDINI ANARUDI KWAO NA BARUA YA MFALME WA BAGHADAD
Hadithi za Alif lela u lela kitabu cha tatu sehemu ya nane Soma Zaidi...

NDOA YA SINBAD NA BINTI WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa NDOA YA SINBAD NA BINT MFALME. Soma Zaidi...

MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME KWA MARA YA PILI
Soma Zaidi...

UPENDO ULIOTAFASIRIWA KWA MICHORO
Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 23
18. Soma Zaidi...

game
Karibu kwenye uwanja wa Game. Soma Zaidi...

SAFARI YA NNE YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA NNE YA SINBAD Basi ikafikia siku ya kuanza safari yangu ya nne ya kibiashara. Soma Zaidi...

SAFARI YA SABA YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA SABA YA SINBAD Walipokusanyika siku ilofata Sinbad akawaambia kuwa kilichofanya nikavunja ahadi yangu ya kutosafiri tena ni kauli ya Sultani Nilipopunzika kwa muda wa miezi miwili nilipata habari kuwa Sultani Soma Zaidi...

HADITHI YA TABIBU NA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA TABIBU WA MFALME Katika nchi ya Zouman iliyopo maeneo ya uajemi alikuwepo mfalme mkubwa sana. Soma Zaidi...

ndege wafikishe
NDEGE WAFIKISHE Hebu paa ndege paa, ufise habari hizi, Ufike wanako kaa, imi kufika siwezi, Paa bila kuzubaa, upae anga iwazi Naujumbe huu twaa, tekeleza hiikazi, Kawa pe utawafaa, wata po fa nyia kazi Kwa watakaokataa, usifanye lazimizi, Wambie lama Soma Zaidi...

Siri ya wageni wale
SIRI YA WAGENI WALE INAFICHUKA Tambua ewe kijana changu, mimi na baba yako tulikutana zamani sana. Soma Zaidi...