KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU

1.1.Kumuamini Mwenyezi Mungu (S.W).
'Madai ya Makafiri dhidi ya kuwepo kwa Allah (s.w) na Udhaifu wa Madai hayo.
Makafiri wa zamani na wa zama hizi wakiwemo Charles Darwin, Friedrich Engles, n.k wanadai kuwa imani ya uwepo wa Mungu Muumba dhana tu haina dalili yeyote. Miongoni mwa hoja (madai) zao wanazotoa ni hizi zifuatazo;

(a)Mwenyezi Mungu hayupo kwa sababu haonekani na wala hadirikiki kwenye milango ya fahamu. Rejea Qur'an (17:90-92).
Milango ya fahamu kama vile macho katika kumuona, pua katika kumnusa, masikio katika kumsikia, ngozi katika kumhisi au kumgusa pia, n.k.

Udhaifu wa hoja hii,
Milango ya fahamu ina udhaifu mwingi sana na kikomo pia, kama vile macho au pua huweza kuona au kunusa vitu vilivyo karibu tu na visivyokuwa na kizuizi, kuna vitu vingi vinavyotuzunguka lakini hatuvioni kama upepo, sauti, n.k.

(b)Mwenyezi Mungu amefanywa kuwepo na wanadamu kutokana fikra na mawazo duni na uduni wa maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Hii ni baada ya mwanaadamu kushindwa kutatua matatizo katika mazingira yake na hivyo kuibukia kujiundia muingu.

Udhaifu wa hoja hii,
Historia inaonyesha kuwa hakuna zama mwanaadamu aliishi bila ya ujuzi wa kukabiliana na mazingira yake, Mwanaadamu wa kwanza kuumbwa alipewa ujuzi (elimu) ya kukabilana na mazingira yake na hatimaye kushushiwa muongozo kamili wa maisha kutoka kwa Muumba wake.
Rejea Qur'an (2:31,38).

(c)Hapana Mungu Muumba bali vitu vyote vimetokana na mabadiliko ya kimaada.
Wanadai kuwa maumbile na viumbe vyote vinatokana na mabadiliko kidogo kidogo ya kimaada (evolution) baada ya muda mrefu kupita kutoka hali moja kwenda nyingine. Mfano binaadamu kutoka pweza, mjusi, sokwe na hatimaye mtu kamili.

Udhaifu wa hoja hii,
Nadharia hii haina ushahidi wowote wa kisayansi, kiuchunguzi na utafti bali ni dhana tu aliyoibuni Darwin ili kupotosha uhalisia na ukweli juu ya chanzo cha maumbile. Hadi leo hii hakuna mwanasayansi yeyote anayeweza kuthibitisha nadharia hii.

(d)Kama Mungu Muumba yupo, ni ipi nasaba (ukoo) yake au ametokana na nini?
Makafiri wa zamani na sasa wanasingizia kutoamini kuwepo Mungu kwa kuwa hawajui nasaba, ukoo au asili yake anatokana na nani au na nini.

Udhaifu wa hoja hii,
Kwa kutumia mantiki, Muumba wa vitu vyote ndiye chanzo na asili ya vitu vyote. Hivyo ni lazima asiwe na nasaba, mwanzo au mwisho pia. Na asitokane na vitu au maumbile yale.
Rejea Qur'an (112:1-4).

(e)Vitu havikuumbwa bali vimetokea kwa bahati nasibu (by chance) na vitatoweka kwa bahati nasibu pia muda wake ukifika.
Makafiri wa zamani na sasa wanadai kuwa asili ya maumbile yote yametokana na bahati nasibu (by chance), hivyo vitatoweka kama vilivyoibuka.

Udhaifu wa dai hili,
Hakuna uwezekano wa kuwepo maumbile bila ya Muumbaji na msimamizi mwenye ujuzi na uwezo wa hali ya juu na mtegemewa wa kila kitu, kwani kila kitu kinachoonekana kimeumbwa na kimewekwa kwa lengo maalum.

'Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo.
Makafiri wanadai kuwa kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) ni ububusa na kufuata mkumbo bila ya udadisi na kutumia akili. Dai hili sio la kweli kwa sababu zifuatazo;
Kwanza, Mwenyezi Mungu (s.w) ametuma Mitume mbali mbali kwa wanadamu ili kuwafundisha na kutoa dalili za kuwepo kwake bila ya shaka yeyote kwa dalili za wazi ili kumfahamu na kuweza kumuabudu ipasavyo.
Rejea Qur'an (4:165).

Pili, Vipawa, ufahamu na akili alivyopewa mwanaadamu ni kumuwezesha kumtambua Muumba wake na kuweza kumuabudu inavyostahiki. Hivyo kutotumia akili katika kumtambua Mwenyezi Mungu kupitia ishara mbali mbali ni kustahiki adhabu.
Rejea Qur'an (3:190), (30:21), (7:179), (8:22) na (12:105).

Tatu, Mitume wa Mwenyezi Mungu pamoja na kuwafundisha wafuasi wao juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu, hawakuwataka kuamini na kufuata bila ya hoja na dalili za wazi bali walionyesha ishara na miujiza kuthibitisha ujumbe wao.

Nne, Msisitizo wa Elimu katika Qur'an kuwa faradhi ya kwanza kama nyenzo pekee ya kumuwezesha mwanaadamu kumjua na kumuabudu Mola wake na kuweza kuyamudu mazingira yanayomzunguka na kuweza kusimamisha Ukhalifa ardhini.

Tano, Maana ya neno 'imani' ambalo lina maana ya 'kuwa na yakini moyoni pasina shaka' yeyote juu ya jambo fulani kwa kuwa na ujuzi nalo na pia kupitia dalili na ishara za kutosha za kuonyesha kuwepo kwake.


                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 451


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Haki ya Serikali kuzuia Dhulma
Soma Zaidi...

Quran haikunukuliwa kutoka kwa mayahisdi na wakristo
(vi)Madai Kuwa Mtume (s. Soma Zaidi...

Tamko la suluhu baada ya vita vya Siffin
Soma Zaidi...

Zijuwe Faida za Kuwa na Istiqama (Msimamo Thabiti)
38. Soma Zaidi...

DUA BAADA YA TAHIYATU, NA KUTOA SALAMU KWENYE SWALA
13. Soma Zaidi...

UGONJWA WA MALARIA NA TAKWIMU ZA ATHARI YAKE KIDUNIA
Malaria ni katika maradhi ambayo husambazwa na na mbu jike aina ya anopheles. Soma Zaidi...

Mitihani aliyopewa Nabii Ibrahimu kutoka kwa Allah
Tumeona katika historia yake kuwa Nabii Ibrahiim(a. Soma Zaidi...

Kuamini mitume wa mwenyezi Mungu, sifazao na lengo la kuletwa kwao
1. Soma Zaidi...

Kumuandaa maiti kabla ya kufa na baada ya kufa, mambo muhimu anayopasa kufanyiwa maiti wa kiislamu
3. Soma Zaidi...

Swala ya Idi al-fitir na namna ya kuiendea
Soma Zaidi...

Mazao ambayo inapasa kutolewa zaka
Soma Zaidi...

Ni zipi sifa za imamu wa swala?
Soma Zaidi...