Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala
.Dhana ya Imani katika Uislamu.
'Maana ya Tawhiid.
- Ni fani inayohusiana na imani ya kuwepo Allah (s.w) na siku ya mwisho pamoja na vipengele vyote vya nguzo za imani.
- Ni kumpwekesha Allah (s.w) katika kila kitu kwa Upweke na Umoja wake na uweza wake juu ya kila kitu.
'Matapo (makundi) ya Tawhiid.
- Tawhiid imegawanyika makundi makuu matatu:
1)Tawhiid ' Rubbuubiyya: Ni Kumpwekesha Allah (s.w) katika Utawala wake.
2)Tawhiid ' Asmaa Wassifaat: Kumpwekesha Allah katika Majina na Sifa zake.
3)Tawhiid ' Ibaadah: Kumpwekesha Allah (s.w) katika Uungu na Kuabudiwa.
'Maana ya imani kwa mujibu wa Qur'an (Uislamu).
- Ni kuwa na yakini moyoni juu ya kuwepo kitu au jambo fulani lisiloonekana kwa macho bali kwa dalili zinazothibitisha kuwepo kwake.
'Imani kwa mtazamo wa Uislamu na ule wa dini zingine:
- Katika Uislamu imani ni ile inayodhihirishwa katika vitendo vya mtu tofauti na dini zingine.
- Katika Uislamu imani juu ya kitu au jambo fulani lisiloonekana hutokana na dalili au ushahidi wa kuonesha uwepo wake tofauti na dini zingine.
Nguzo za Imani.
'Nguzo za imani ya Kiislamu ni Sita:
1.Kumuamini Mwenyezi Mungu (s.w).
2.Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu (s.w).
3.Kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w).
4.Kuamini Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w).
5.Kuamini Siku ya Mwisho.
6.Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu (s.w) kuwa kheri na shari vyote vinatokana kwake.
Rejea Qur'an (2:285), (4:136), (57:22) na (11:6).
'Nguzo ya Ihsani.
- Nayo ni 'kumuabudu Allah (s.w) kana kwamba unamuona na kama humuoni basi yeye anakuona'.
'Nani muumini wa kweli? (Sifa za muumini wa kweli).
- Ni yule ambaye imani yake inathibitishwa katika matendo ya kila kipengele cha maisha yake ya kila siku.
Rejea Qur'an (2:8-9).
- Ni yule anayejipamba na sifa za waumini zilizoainishwa katika Qur'an na Sunnah katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kila siku.
Rejea Qur'an (23:1-11), (25:63-77), (33:35-36), n.k.
- Ni yule anayeendea kila kipengele cha maisha yake kwa mujibu wa vipengele vyote vya nguzo za imani ya Kiislamu.
oHawi muumini wa kweli kwa imani isiyoendana na matendo wala kwa kuamini baadhi ya nguzo za imani.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa
Mwandhishi Tarehe 2018-08-01 Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 457
Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Madrasa kiganjani
Haki ya Serikali kuzuia Dhulma
Soma Zaidi...
Nini maana ya tabii tabiina
Soma Zaidi...
Zijuwe suna (sunnah) za Udhu ama Kutawadha
Soma Zaidi...
Maana ya Kuamini Siku ya Mwisho
Soma Zaidi...
HISTORIA YA NABII IBRAHIM
Soma Zaidi...
Aina za talaka, sharti zake na taratibu za kutaliki katika uislamu
Maana: ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa baina ya mume na mke mbele ya mashahidi wawili kwa kuzingatia sheria ya Kiislamu. Soma Zaidi...
Kitabu Cha Dua 120
Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe vyote. Soma Zaidi...
HISTORIA YA KUUMBWA KWA NABII ADAMU (A.S)NA HADHI YAKE NA HADHI YA WANAADAMU DUNIANI
Adam(a. Soma Zaidi...
HISTORIA YA MAISHA YA MTUME S.A.W KABLA YA UTUME
MAISHA YA MTUME (S. Soma Zaidi...
Kuamini qadar na qudra katika uislamu
Kuamini Qadar ya Allah (s. Soma Zaidi...
Utaratibu wa kuzika, hatua kwa hatua, na namna ya kusindikiza jeneza
4. Soma Zaidi...
MASHARTI YA KUKUBALIWA KWA DUA
MASHART YA KUKUBALIWA KWA DUA. Soma Zaidi...