picha

SHAIRI KUTOA NI USHUJAA

KUTOA NI USHUJAA KUTOA NI USHUJAASalamu kwanza awali, wasikizi tikieni, Mwambaje nazenu hali, kheri nawatakieni, Mungu awape sahali, muifuzu mitihani, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa,Kila alie akili, hutunza yake thamani, Hilo sote twakubali

SHAIRI KUTOA NI USHUJAA

KUTOA NI USHUJAA
KUTOA NI USHUJAA
Salamu kwanza awali, wasikizi tikieni, Mwambaje nazenu hali, kheri nawatakieni, Mungu awape sahali, muifuzu mitihani, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Kila alie akili, hutunza yake thamani, Hilo sote twakubali, sitaraji upinzani, Zingata yangu kauli, ikufae maishani, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Mja ulie na mali, mtazame masikini, Kwani wake udhalili, niqadari ya manani, Kumtenga niajali, tena mbaya hukumuni, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Natena usikubali, aingie dhilalani, Maliyo siibakhili, nikuipa kisirani, Mungu kwayake ajili, mlinde huyojirani, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Kumwacha niukatili, tena usio kifani, Fikiria mara mbili, mali kwakomtihani, Hakutatosha kuswali, namisaada toweni, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Ukitaka afadhali, nauishi kwa amani, Mafunzo haya nakili, uyatie matendoni, Kiombwa siwe mkali, toa kwadhati moyoni, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Maisha nipande mbili, kuna nyuma na usoni, Ukatae ukubali, lambeleni hulioni, Kesho hashindwi jalali, nawe kukushusha chini, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Mtu nzi:H D.Hassa n @SUKARI YA MASHAIRI@ Pangani Tanaga 0655832944


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: General Main: Post File: Download PDF Views 1094

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 ai web app     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

HADITHI YA SIRI YA UTAJIRI WA AJABU : sehemu ya 01

huu ni ufupisho wa kisa cha utajiri wa ajabu katika kijiji fulani huko zamani za kale.

Soma Zaidi...