image

MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME KWA MARA YA PILI

MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME KWA MARA YA PILI


MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME KWA MARA YA PILIAladini alimlaumu sana Sultani kwa kushindwa kuonyesha uadilifu kwenye ahadi yao. Aladini alimueleza mama kila kilichotokea. Aladini alikaa kwa muda kufikiri nini afanye. Mama hakuonekana kuwa na lolote la kusema. Kwa uande mwingine binti sultani sikuzote alikuwa upande wa baba yake. Asingeweza kumpinga baba yake kwani angeweza kumtia hatiani Aladini. Aladini akawaza itu kisha akaenda kunywa maji kutuliza mwili. Aldini alisubiri siku ya tatu ambapo ndio harudi itafanyika. Usiku wa harusi Aladii alisugua mshumaa wake na punde jini la mshumaa likatokea na kumueleza anataka shida gani.


Aladini kwa ujasiri akatamka “nataka usiku uniletee kitanda alicholala Binti sultani na moto wa waziri” nimesikia na nimetii. Yalikuwa ni maneno machache ya Aladini na Jini. Hali ilikuwa kama hivyo, ilipofika usiku wakati mtoto wa waziri aliotaka kulala na bint Sultani ghafla kitanda kikahamishwa. Loo !!! Aladini yupo mbele yao, Aladini akamwambia jini amtoe mtoto wa waziri amuweke nje kwenye baridi. Aladi ni akamwambia bint, “usihofu hakuna chochote kibaya kitakachotokea, wewe ni mke wangu ila baba yako hakuheshimu ahadi yetu.


Ijapokuwa binti anampenda Aladini lakini sasa alipatwa na woga kwenye nafsi yake. Usiku ukapita Aladini akiwa kwenye usingizi mnono kabisa. Wakati huohuo bint alikuwa yupo katika mawazo mengi hata hakupata usingizi. Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa upande wa mtoto wa waziri ambaye alitupwa nje. Ilipofika karibu na asubuhi aladini alimueleza mtoto wa waziri kila kilichotokea na hivyo yeye hapaswi kuwa na binti Sultani. Jisha Aladini akamuamrisha jini awarudishe, na ikawa hivyo.


Ilipofika asubuhi Mfalme akataka kwenda kumsalimia mkwewe na binti yake. Loo!!! aliwakuta wote wapo kwenye huzuni na majonzi makubwa sana. Alipojaribu kuzungumza nao hakuambulia majibu yeyote. Mtoto wa waziri aliogopa kusema maana atamkosa binti Sultani. Na binti sulani alitaka kuzungumza ila alimuogopa baba yake kuwa anaweza kumfanyia kitu kibaya Aladini. Basi hali ilikuwa hivi ndani ya siku tatu, Aladi I akawa anawachukuwa na ikikaribia alfajiri huwarudisha. Siku ya nnze Mfalme alitaka aambiwe ukweli vinginevyo wote atawatandika bakora vilivyo.


Mtoto wa Waziri akaanza kueleza kila kilichotokea na ni nani aliyekuwa akiwafanyia mambo yote kuwa ni aladini. Binti naye akaeleza vivyo hivyo. Mfalme alichoka sana, kwani hakuamin kama anaweza kufanyiwa jambo kama hili. Alipata kulisikia jambo hili zamani sana lakini ilikuwa ni ngano tu na halikuwa na ukweli. Sasa macho ya mfalme yamebadilika na kuwa mekundu, kwa hasira, huzuni na taharuki. Kwa hakika kutimiza Ahadi ni jambo la kiungwana. Mfalme alikumbuka kuwa alimueleza mama wa Aladini kuwa ndani ya miezi mitatu atampatia jibu. Kaka kabla ya miezi mitatu hakutoa jibu la kukubali ama kukataa na vinginevyo amemuozesha binti yake.


Leo mfalme amepata funzo kuwa kutimiza ahadi ni jukumu la kila mtu na ni kwa yeyote awe mdogo kiumri ama kicheo. Na unaweza kupata madhara kwa kutotimiza ahadi. Mfalme alitumia siku nzima kukaa peke yake, kutafakari na kutafuta utatuzi. Mwishowe alimuita binti yake na kumtaka ushauri. Kwa kuwa ndoa ya binti haikukamilika kwa mujibu wa sheria maana kijana wa sultani haja hata mgusa binti Mfalme. Binti akaanza kufunguka “baba kama utaniruhusu kuzungumza yaliyo moyoni, na kama utaniahidi kuwa hutamfanyia Aladini chochote kibaya, nitakueleza kila kitu” nakuahidi binti yangu kipenzi, tafadhani nieleze yale nisiyo yajuwa kuhusu huyu Aladini” ni maneno machache kati ya Mfalme na binti yake.


Basi binti mfalme akaanza kueleza kila kilichotokea mpaka kufikia siku ile. Mfalme alizidi kuchoka baada ya kugundua kuwa kumbe Aladini aliwahi kukiuka amri ya kubakia ndani na kwenda bwawani kumchungulia binti yake. Binti akaendelea kueleza kuwa “kunanzia siku ile baba niltokea kumpeda aladini, na hata siku ile ulipomkatalia posa mama aladini nilianguka kwa maumivu nilioyapaa. Kwa siku kadhaa nilishinwa kuona tamu ya chakula”. maneno haya yalizidi kumuumiza mfalme. Yaani ulinzi wote aliouweka kwa binti yake lakini bado kulitokea mianya ya miyo wa binti yake pekee kutekwa na kijana masikini wa mtaani. “Kweli mapenzi hayajui hadhi, cheo wala kabila” alijisemea mfalme huku akipiga funda la maji.


“baba tafadhali mkubalie Aladini, kwani ndio furaha ninayoisubiri” binti mfalme alizidi kukandika maneno makali juu ya masikio ya mfalme. Mfalme alichukuwa muda wa siku tatu kutafuta ufumbuzi mwishowe akamuita waziri wake na kumueleza kuwa ndoa ya binti yake na mtoto wake ameivunja rasmi mpaka Aladini atakaposhindwa mwenyewe. Ila walipanga sasa mikakati ya kuhakikisha kuwa Aladini anashindwa kulipa mahari. Waziri na mfalme kwa pamoja waliamini kama watawakatisha wawili hawa mapenzi yao kwa amri wataweza kupata madhara huenda wakamkoseshea amani binti yake. Hivyo wakatafuta binu mbadala ya kumfanya Aladini ashindwe yeye mwenyewe.


Baada ya kukubaliana mahari kabambe, mahari ambayo hata mtoto wa waziri mwenyewe asingeweza kuilipa. Hata mtoto wa mfalme mwengine angeweza kuilipa ila kwa taabu. Mipango yao yoote hii binti mfalme aliweza kuipata kwa kupitia mashushushu wake wa kike aliowaweka kwenye chemba ya baba yake. Ijapikuwa alijuwa fika mipamngo hii lakini hakuwa na chochote cha kufanya zaidi ya kuomba dua. Mfalme baada ya kumaliza kikao chake akaagiza mama Aladini aletwe ili apatiwe majibu ya posa ya mwanae. Kwa haraka sana taarifa zikamfikia mama aladini, na bila kuchelewa akafika mbele ya mfalme.


Mfalme akamuangalia mama aladini na kumwambia asogee karibu yake huku moyoni mama aladini akawa anajisemea “nikutwishe mzigo wa mahari na ukishindwa nitakuoa mimi ili mwanao aniite baba. Hataweza tena kumuoan binti yangu” ni maneno aliyojisemea mfalme baada ya kuvutiwa na uzuri wa mama Aladini. Mfalme alitabasamu na kufanya masharubu yake yapepee vyema, mama Aladini alitabasamu alipoona zile sharubu, huku akimkumbuka marehemu mume wake mzee Mustapha. Mfalme akatamka kuwa mwanao amekubaliwa posa yake. Hivyo ajiandae kulipa mahari ili kumuoa binti Mfalme.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 172


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Harusi ya aladini na binti sultani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

ALADINI KATIKA PANGO LA UTAJIRI
Soma Zaidi...

Hadithi iliyosimuliwa na mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hadithi ya Kinyozi kaka wa kwanza
Soma Zaidi...

Ndoa ya Siri yafanyika
Posti hii inakwenda kukuendelezea hadithi kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi kaka wa pili
Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi mwenyewe
Soma Zaidi...

Mshenga wa aladini mbele ya mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

hatima ya kinyozi
Soma Zaidi...

HADITHI YA CHONGO WATATU WATOTO WA WAFALME
Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi
Soma Zaidi...

Sababu ya kukatwa vidole gumba
KWA NINI VIDOLE GUMBA VILIKATWA? Soma Zaidi...