HADITHI YA KINYOZI YEYE MWENYEWE
Mimi si mtu wa maneno mengi kama kijana anavyonidhania. Hata hivyo nipo tofauti sana na kaka zangu kwani mimi ndiye mtoto wa mwisho.. nitakusimulieni kisa kimoja hapa ndipo mtagundua kuwa mimi si mtu wa maneno mengi. Siku moja nilipokuwa sina kitu cha kukila na kwa kuwa mimi si mtu wa maneno mengi sikuweza kwenda kukopa. Niliweza kusikia wepesi wa tumbo langu kwa njaa, hata nikathubutu kufunga kipande cha kanga tumboni. Sikujuwa ni kwa nini siku ile nilikuwa na njaa sana. Niliamini huenda ikawa ni majaribu yamenifikia. Mingurumo ya tumbo ilizidi kusumbua.
Basi katika pirika zangu nikakutana na vijana 10 wapo kwenye dau. Kwa mawazo yangu nikadhani wanakwenda kusherehekea. Na hii ilikuwa ni kawaida kwa vijana wakikusanyika eneo hili wanakwenda upande wa pili wa mto kufurahia na kula na kunywa. Mawazo ya njaa yalikuja karibu zaidi hata ikawa chakula kama kipo mbele yangu. Nikaanza kupata harufu ya paja la kuku lililokaangwa na kukaushwa vyema. Chapati za mayai zilizofunika samaki vyema. Harufu ya juisi nikaanza kuipata kwa mbaali wakati nakodolea macho paja la kuku.
Kwa njaa zangu na pupa ndipo nikakimbilia bilauri ya juisi na kuanguka. Loo! Nimevunja bilauri ya watu. Ghafla nikashituka kutoka kwenye dimbwi la mawazo. Nikawahi kwenye dau na mimi kuingia. Bila hata ya kuuliza zaidi kilichowakuta na wapi wanakwenda. Kwa kuwa mimi si mtu wa maneno mengi sikuweza kuuliza sana. Nahodha akang’oa dau na kuanza kutokomea mtoni. Nilianza kushangaa kumbe vijana wote 10 waliomo mule wamefungwa minyororo, na walikuwa chini ya uangalizi wa askari. Kwa kuwa mimi si mtu wa maneno mengi niliendelea kuwa kimya.
Tulipofika ng’ambu ya pili ya mto tulipokelewa na kundi kubwa la askari na kupelekwa kwa kadhi. Sikuzungumza kitu na wala sikujitetea kwa lolote. Ni kwa sababu mimi si mtu wa maneno mengi. Tulipofika kwa kadhi wale mabwana kumbe walikuwa na kosa na mauwaji na hivyo kadhi akaamuriu vijana wote 10 wakatwe vichwa vyao mara moja. Kwa kuwa mimi si mtu wa maneno mengi niliendelea kukaa kimya none hatma ya uwepo wangu pale. Basi askari akawachukuwa wote vijana 10 na kwenda kukata vichwa vyao.
Baada ya muda kidogo askari akaja mbele ya kadhi na kutamka kuwa kazi imekwisha, yaani ameshakata vichwa vyao. Kadhi akamuuliza mbona umechukuwa 9 na huyu wa 10 umemuacha hapa. Askari akajibu hapana mkuu nimechukuwa wote 10. kadhi hakuamini hata akaenda kuhesabu vichwa. Loo! Ni kweli vichwa vilikamilika 10. hapa kadhi akawa na furushi la maswali kichwani mwake. Furushi lote akataka kunitundika mimi. Kwa kuwa mimi si mtu wa maneno mengi niliendelea kunyamaza. Kadhi akaja akiwa amefura kw ahasira na mawazo.
Alipokaa vyema akaagiza aletewe maji kwenye chombo. Kadha alipoletewa maji alikuywa na kutawadha. Alifanya hivi ili kupunguza hasira, ili asijefanya maamuzi yasiyo ya haki. Kisha kadhi akaniuliza haya wewe ni nanai na imekuwaje akuajumlishwa kwenye kundi hili la watu wabaya? Basi sasa sina budi nikaanza kumueleza Kadhi namna nilivyofika pale. Kadhi alishangaa sana kuona vile hivyo akanieleza kuwa ni kwa nini hukuzungumza toka mwanzo. Nikamueleza kuwa mimi si mtu wa maneno mengi. Nikaendelea “usidhani kuwa mimi ni mtu wa maneno mengi, mimi ni tofauti sana na kaka zangu.
Kwani kaka yangu wa kwanza ni kichaa na ameupata ukichaa kutokana na yaliyomkuta na maneno mengi yake. Ili uamini kuwa mimi si mtu wa maneno mengi, nitakuhadithia yaliyowapata kaka zangu wote kutokana na maneno yao mengi. Baada ya kuzungumza hivi kinyozi akaanza kuhadithia yaliyotokea kwa kaka wake wa kwanza:
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela2 Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 581
Sponsored links
👉1
Kitabu cha Afya
👉2
Kitau cha Fiqh
👉3
Madrasa kiganjani
👉4
Simulizi za Hadithi Audio
👉5
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6
kitabu cha Simulizi
Hadithi ya kinyozi kaa wa tatu
Soma Zaidi...
Hadithi ya aliyekatwa vidole gumba
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...
Utajiri wa baba na kifo chake
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...
Ujumbe wa Siri kwenye kitabu cha ajabu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...
MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME KWA MARA YA PILI
Soma Zaidi...
Mrembo mtoto wa tajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...
Viatu vya ajabu vyaondoka na mkono wangu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...
Hadithi ya Mshona nguo
Soma Zaidi...
Nani muuaji?
Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu muuaji wa mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...
HISTORIA YA PANGO, ALADINI NA KITABU
Soma Zaidi...