(a)Il-hamu.Ni mtiririko wa habari au ujumbe unaomjia mwanaadamu bila ya kufundishwa na mtu yeyote au kuona mfano wake katika mazingira yoyote. Mambo mengi mwanaadamu huyafahamu kwa Il-hamu. Wagunduzi wa fani mbali mbali za elimu kama vile Hisabati, Fizikia, Jiografia, n.k. na Wavumbuzi wa vitu mbali mbali katika taaluma mbali mbali za kisayansi wameweza kufanya hivyo kwa kupata Il-hamu kutoka kwa Allah. Hivyo hakuna fani yoyote ya elimu isiyotoka kwa Allah (s.w).


“Amemfundisha mwaanadamu mambo yote aliyokuwa hayajui” (96:5).