RAJABU ATHUMAN MAHEDE

Rajabu Athumani Mahede Amesoma shule ya msingi Pangani ambapo amemalizia darasa la saba mwaka 2007 na kujiunga na shule ya kata itambulikayo kama Funguni secondary school ambapo alimaliza kidato cha nne mwaka 2011. Rajabu Athumani alijiunga na elimu ya A-level kidato cha tano mwaka 2012 katika shule ya secondary ijulikanayo kama Iwalanje secondary school iliyopo Mkoani Mbeya. Rajabu Athumani alimaliza kitado chasita mwaka 2014 na kujiunga na elimu ya chuo kikii.

Rajabu Athumani alijiunga na elimu ya Chuo kikuu (University Educaton) katika chuo kikuu kiitwacho University of Dar Es-Salaam (UDSM) ambach ni moja kati ya vyuo vikuu vinavyofanya vyema barani Afrika. Huko Rajabu Athumani alisomea fani ya ualimi kwa muda wa miaka mitatu. Rajabu Athumani alimaliza elimu ya chuo kikuu kama mwalimu wa somo ya Jiografia na Kiingereza na kutunukiwa Shahada (degree).

Rajabu Athumni akiwa chuoni pia alijifunza taaluma za program za kompyuta, na hivyo kuwa na uelewa kuhusu misamiati mingi inayotumuka kwenye fani za kompyuta. Hali hiyo ilimtia hamasa zaidi na kuamua kutafuta kozi mbalimbali za kompyuta na kuanza kusoma. Yote haya utaweza kuyathibitisha kwa kile unachokiona kwenye tovuti hii.

Rajabu Athuman amekuwa ni msaada mkubwa kwa vijana wanaoanza kutengeneza blog ama tovuti ama wanaotaka kujuwa namna ya biashara za kimitandao zinaanzaje. Lakini faida zaidi inapatikana kupitia Blog, tovuti hii pamoja na Channel ya yoytube. Ambapo huko watu wanajifunza mengi hususan kuhusu Afya, Dini, Burudani, biashara na msaada kwa wanafunzi.