Sifa za Kuwa Mpole na Mnyenyekevu

22.

Sifa za Kuwa Mpole na Mnyenyekevu

22. Kuwa Mpole na Mnyenyekevu



Mtu mpole ni yule aliyetulia, asiyelipuka kwa hamaki. Huzungumza na watu kwa sauti ya chini. Akiudhiwa halipuki kwa hasira na kupaza sauti bali husubiri kwa utulivu. Huwa ni mwepesi wa kuwasamehe waliomkosea. Muumini hana budi kujipamba na sifa hii ya upole kwani ni miongoni mwa sifa za waja wema wa Allah (s.w)


'Na waja wa Rahman ni wale wanokwenda (na kurejea) katika ardhi kwa unyenyekevu; na wajinga wakisema nao (maneno mabaya) huwajibu (maneno ya) salama'. (25:63)


Pamoja na kujipamba na tabia ya upole, Waislamu hawaruhusiwi kuyaachia maovu yakafanyika katika jamii bila ya kuyakemea. Ni juu ya Waumini kuamrisha mema na kukataza maovu na kuwa wagumu kwa maadui wa Uislamu na wenye kuhurumiana wao kwa wao. Hii ndiyo tabia ya Mtume na Maswahaba wake kama tunavyojifunza katika Qur'an:


'Muhammad ni Mtume wa Allah na walio pamoja naye ni wenye nyoyo thabiti (ngumu) dhidi ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao...' (48:29).
Pindi maadui wakiacha uadui wao dhidi ya Uislamu, waislamu watawaelekea kwa upole:


'Na kama (hao maadui) wakielekea katika amani, wewe pia ielekee (amani) na mtegemee Allah. Hakika yeye ndiye asikiaye na ajuaye.Na kama wakitaka kukuhadaa basi Allah atakutosheleza. Yeye ndiye aliyekusaidia kwa nusura yake na kwa walioamini'. (8:61-62).




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 231


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-