Nimeandika Makala hii kutkana na uzoefu wangu. Hivyo haya ni mawazo binafsi TU.
Kuhusu Google AdSense Approval – Usidanganyike!
Kwa uzoefu wangu kuhusu mchakato wa kuidhinishwa kwa akaunti ya Google AdSense, kuna taarifa nyingi zinazopotosha ambazo zimekuwa zikienea kuhusu nini hasa kinazingatiwa ili akaunti ikubalike. Mara nyingi tumekuwa tukiamini mambo yasiyo sahihi kama haya:
Mambo tuliyoaminishwa kimakosa:
1. Lazima tovuti au blog iwe na watembeleaji wengi.
2. Iwe na umri wa angalau miezi mitatu.
3. Iwe na idadi kubwa ya machapisho (posts).
Hali halisi kwa mujibu wa uzoefu wangu:
1. Tovuti iwe "live" muda wote
Tovuti yako inapaswa kupatikana bila kukatika, hasa wakati unapotuma maombi ya AdSense. Google ina uwezo wa kugundua hata kama tovuti yako ilikuwa haipatikani kwa muda mfupi. Hakikisha unatumia huduma ya uhakika ya hosting.
2. Iwe rahisi kutumia (simple navigation)
Epuka kuweka navigation ngumu kufikia maudhui. Mfano wa kosa ni kuweka menu > category > tag > post ndipo maudhui yaonekane. Google hutumia bots kusoma tovuti, na bots hawawezi kufuata muundo tata. Hivyo, weka maudhui yako yapatikane kwa hatua chache tu.
3. Angalau domain iwe inatambulika na Google
Ni vyema kuiunganisha tovuti yako na Google Search Console ili kusaidia kuitambua kwa urahisi. Angalia kama domain yako inaonekana unapoitafuta Google.
4. Maudhui ya kipekee (unique content)
Ikiwa unatumia blog au tovuti ya makala, hakikisha kila chapisho ni cha kipekee na chenye ubunifu. Google hukagua kwa makini sana maudhui ya blog, na ni vigumu kukubaliwa kama unakopi au kutumia maudhui yasiyo na ubora.
5. Kurasa muhimu zisikosekane
Hakikisha una kurasa muhimu kama About, Privacy Policy, na Contact Us. Kurasa hizi ziwe wazi, rahisi kufikiwa, na ziwe na maudhui ya kueleweka.
Mbinu ya Haraka ya Kukubalika na AdSense
Njia rahisi ya kuanza ni kuunda web app badala ya blog ya kawaida. Web app ni kama tovuti yenye huduma au kazi maalum, siyo tu machapisho ya habari au makala. Ukishakubaliwa, unaweza kuanza kuongeza vipengele vingine taratibu. Mfano wa web app ni kama:
https://bongolite.com/
Kwa ushauri zaidi na mafunzo kuhusu tovuti, blog, na Google AdSense, tembelea:
https://bongoclass.com
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya hapa chini kuipakua sasa!
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika post hii utajifunza historia ya internet maka kufikia Leo.
Soma Zaidi...