Mafunzo ya kutengeneza Desktop App

Utajifunza kutengeneza app za desktop kwa kutumia WPF framework

12 Lessons
4 Topics
Author: Rajabu
4.8 (120 Reviews)
Unlock Full Course Access

Please login or register to access all lessons, track your progress, and earn certificates.

Course Curriculum

1
Utangulizi wa WPF na tofauti yake na Windows Forms

Katika somo hili tutajifunza: WPF ni nini na historia yake Sababu ya Microsoft kuanzisha WPF Vipengele muhimu vya WPF Tofauti kati ya WPF na Windows Forms Faida na changamoto za kutumia WPF

15 min Video
2
Muundo wa project ya WPF (katika JetBrains Rider)

Katika somo hili tutajifunza: Vipengele vya msingi vinavyounda WPF project Faili muhimu zinazoonekana mara tu baada ya kuunda project mpya Majukumu ya kila faili Mlolongo wa jinsi WPF application inavyotekelezwa (execution flow) Uhusiano kati ya XAML na C# code-behind

15 min Video
3
Utangulizi wa XAML na sheria za uandishi wake

Katika somo hili tutajifunza: XAML ni nini na inafanya kazi gani katika WPF Sheria kuu za uandishi wa XAML Tofauti kati ya XAML na HTML Mfumo wa tag (elements na attributes) Orodha ya tags muhimu 20 katika WPF

15 min Video
4
Kushughulika na maandishi (Text) katika WPF – TextBlock, Run, Paragraph na Styles

Katika somo hili tutajifunza: Jinsi ya kuonyesha maandishi kwa kutumia TextBlock. Kutumia Run, Bold, Italic, na Underline ndani ya XAML. Tofauti kati ya inline style na paragraph style. Namna ya kutumia rangi, font, na alignment kwenye maandishi. Kutengeneza paragraph yenye maandishi yenye mitindo mbalimbali.

15 min Video
5
Kuweka link kwenye text

Katika somo hili tutajifunza: Kutumia RichTextBox kuonyesha au kuhariri maandishi marefu yanayoweza kuscroll. Kupanga stori ndefu kwa kutumia FlowDocument, Paragraph, na Run. Kutumia inline styling kuboresha muonekano wa stori. Kuweka clickable text na linki kwenye maandishi kwa kutumia Hyperlink.

15 min Video
6
Hierarchy ya Controls za Maandishi (Text Hierarchy na Nesting katika WPF)

Katika somo hili tutajifunza: Uhusiano (hierarchy) kati ya controls zinazohusika na maandishi kwenye WPF. Ni controls zipi zinaweza kuwa containers (zina children) na zipi ni leaf controls (hazina children). Jinsi ya kutumia nesting — yaani kuweka control moja ndani ya nyingine ili kujenga maandishi yaliyopangwa vizuri. Mifano halisi ya muundo wa maandishi unaotumia TextBlock, Run, Span, Paragraph, na FlowDocument.

15 min Video
7
Layouts na UI Components katika WPF

Katika somo hili tutajifunza: Dhana ya layout system katika WPF. Jinsi containers zinavyotumika kupanga controls katika interface. Aina kuu za layout panels: Grid, StackPanel, DockPanel, Canvas, na WrapPanel. Mifano ya jinsi ya kutumia kila layout. Mbinu bora za kuchanganya layouts kujenga UI safi na inayobadilika.

15 min Video
8
Hierarchy ya nesting kati ya layouts katika WPF

Katika somo hili tutajifunza: Maana ya nesting katika layouts Ni layouts zipi zinaweza kuwa ndani ya nyingine Jinsi ya kupanga layouts kwa kutumia mfano wa Grid ndani ya StackPanel Mpangilio bora wa kutumia layouts kwa ufanisi Vidokezo vya kitaalamu katika kupanga hierarchy ya layouts

15 min Video
9
Kutengeneza layout ya ukurasa kamili (header, sidebar, content na footer)

Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kupanga vipengele vikuu vya ukurasa wa WPF kwa kutumia layouts. Tutaunda header, sidebar, content area, na footer. Hii ndiyo sura ya msingi ya programu nyingi za desktop zinazotumia WPF. Tutatumia Grid, StackPanel, na DockPanel kupanga sehemu hizi.

15 min Video
10
kutumia Button katika WPF

Tutajifunza mambo yafuatayo: Maana ya button na kazi yake katika WPF Namna ya kuongeza button kwenye XAML Jinsi ya kuunda event method kwa C# Maelezo ya ndani ya Button_Click(object sender, RoutedEventArgs e) Mifano mingine mitatu ya matukio tofauti ya button Kubadilisha style ya button kwa XAML

15 min Video
11
Matendo mbalimbali yanayoweza kufanywa na batani (Button actions)

Leo tutajifunza baadhi ya vitendo (actions) ambavyo batani inaweza kufanya inapobonyezwa katika programu ya WPF. Tutatazama mifano kama kufungua link kwenye browser, kufuta maandishi, kubadilisha rangi ya kipengele, kubadilisha maandishi ya batani, kuonyesha ujumbe, na mambo mengine ya msingi.

15 min Video
12
kutengeneza windows nyinine na kufanya navigation kwa kutumia button

Leo tutajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kuunda windows mbili ndani ya project ya WPF kwa kutumia JetBrains Rider, na jinsi ya kuhamia kutoka dirisha moja kwenda jingine kwa kubonyeza button. Tutalinganisha dhana hii na kurasa za tovuti, ili uone mfanano wa kiufahamu kati ya desktop UI na web UI.

15 min Video

Ready to start learning?

Join thousands of students who are advancing their careers with BongoClass

Enroll Now