Katika somo hili tutajifunza kuhusu: Historia ya C# na nafasi yake kwenye ulimwengu wa programu. Maana ya .NET, pamoja na dhana za solution, project na application. Rider IDE na hatua za kuanza kazi. File extensions zinazotumika kwenye C# na .NET. Namna ya kutamka jina la lugha ya C#.
Katika somo hili tutajifunza kuhusu syntax rules za C#, ambazo ndizo misingi ya kuandika code sahihi. Tutaona namna ya kutumia statements, semicolons, curly braces, indentation, na naming rules. Pia tutajifunza dhana ya case sensitivity na jinsi inavyoathiri uandishi wa code.
Katika somo hili tutajifunza: Maana ya data types na kwa nini ni muhimu. Aina kuu za data kwenye C#. Namna ya kutangaza na kutumia variables. Uhusiano kati ya value types na reference types. Type conversion (casting) – implicit na explicit.
Katika somo hili tutajifunza: Maana ya operator katika C#. Makundi ya operators na matumizi yake. Arithmetic operators, comparison operators, logical operators, na assignment operators. Special operators (null-coalescing, ternary, na new pattern matching operators). Mfano wa matumizi ya operators kwenye C# (toleo jipya).
Katika somo hili tutajifunza: Maana ya control flow kwenye C#. Kutumia if, else if, na else kuunda maamuzi. Kutumia switch na switch expression (C# mpya). Mfano wa vitendo jinsi control flow inavyotumika.
Katika somo hili tutajifunza: Maana ya loop kwenye C#. Aina za loops: for, while, do...while, na foreach. Jinsi ya kuvunja au kuruka loop kwa break na continue. Mifano ya vitendo kutumia loops.
Katika somo hili tutajifunza: Maana ya function (method) kwenye C#. Sababu za kutumia functions. Aina za functions (static, instance, void, zinazorejesha thamani, n.k.). Parameta na argument (tofauti na matumizi). Mfano wa kisasa wa functions kwenye C#.
Somo hili litafafanua maana ya string katika C#, jinsi zinavyohifadhiwa, na jinsi ya kufanya kazi nazo. Pia tutajifunza method 20+ muhimu zinazotumika sana ku-manipulate strings.
Somo hili linazungumzia array katika C#, namna zinavyoundwa, jinsi ya kufikia data zilizomo ndani yake, na method muhimu zinazotumika ku-manipulate array.
Katika C#, namba kama int (nambari nzima) na float/double/decimal (nambari zenye desimali) ni value types zinazotoka kwenye System.Int32, System.Single, System.Double, na System.Decimal. Somo hili litajadili method na properties muhimu zinazotumika na aina hizi za data ili kufanya mahesabu, ukaguzi, na mabadiliko ya thamani.
Somo hili litaeleza jinsi ya kupokea data kutoka kwa mtumiaji (user input) kwenye programu za C#. Tutajifunza namna ya kutumia Console.ReadLine(), jinsi ya kugeuza (convert) input kuwa aina tofauti za data, na tahadhari zinazohitajika ili kuepuka makosa.
Somo hili litazungumzia jinsi ya kushughulika na makosa (errors) katika C#. Tutajifunza kuhusu: try, catch, finally Exception classes Custom exceptions Error handling ni muhimu sana kwa sababu hufanya programu kuwa imara na isiyovunjika kirahisi wakati wa makosa.
Somo hili linafundisha dhana ya msingi ya Object-Oriented Programming (OOP) katika C#. Tutajifunza: OOP ni nini na kwa nini inatumika. Vipengele vikuu vya OOP. Dhana ya Class na Object. Maelezo ya Properties na Methods. Kwa nini tunahitaji class kuu na entry point ya programu. Mfano wa kimsingi wa OOP kwa maelezo ya kina.
Katika somo hili tutajifunza kuhusu Encapsulation, moja ya nguzo kuu za OOP. Tutaona: Encapsulation ni nini. Aina za access modifiers (public, private, protected, internal). Mifano midogo kwa kila modifier. Mfano mkubwa unaojumuisha yote.
Katika somo hili tutajifunza kuhusu Inheritance (urithishaji) kwenye OOP. Tutajua maana yake, kwa nini inahitajika, jinsi ya kutumia :, na tutatoa mifano midogo midogo kwa kila kipengele. Mwisho tutajumuisha mfano mmoja mkubwa unaokutanisha vyote.
atika somo hili tutajifunza Polymorphism kwenye OOP. Tutaona maana yake, aina zake kuu (overloading na overriding), masharti yake, jinsi inavyofanya kazi, na tutapata mifano midogo midogo ya kila kipengele. Mwishoni tutaandika mfano mmoja mkubwa unaokutanisha vyote.
Katika somo hili tutajifunza maana ya abstraction, kwa nini tunaitumia, jinsi ya kutekeleza kwa kutumia abstract classes na interfaces, na tofauti kati ya hivi viwili. Tutatoa mifano midogo midogo kwa kila kipengele, kisha mfano mkubwa unaokutanisha vyote.
Somo hili litafundisha kuhusu data classes na records katika C#. Tutaelewa tofauti ya value types na reference types, jinsi records zilivyoongezwa kuanzia C# 9+, na kwa nini ni muhimu unapofanya kazi na data zinazohitaji usalama na urahisi wa kusimamia.
Somo hili linazungumzia kwa undani kuhusu objects na dhana zinazohusiana nazo kwenye C#. Tutaona tofauti kati ya instance members na static members, tutajifunza kuhusu static classes & methods, na pia tutaelewa singleton pattern, mojawapo ya design patterns maarufu sana kwenye OOP.
Somo hili litazungumzia collections na generics katika C#. Tutaelewa matumizi ya arrays, lists, na dictionaries, kisha tutaona dhana ya generics na kwa nini ni muhimu. Mwisho, tutaanza kuonja LINQ (Language Integrated Query) kama njia ya kufanya query kwenye collections.
Somo hili litaeleza method muhimu zinazotumika mara kwa mara kwenye List<T>, Dictionary<TKey, TValue> na dhana ya generics kwa ujumla. Tutajifunza jinsi ya kuongeza data, kuondoa data, kutafuta data, na kufanya manipulations mbalimbali kwenye collections.
Somo hili litaeleza kuhusu LINQ (Language Integrated Query) katika C#. Tutajifunza maana ya LINQ, faida zake, jinsi inavyofanya kazi na collections, pamoja na aina kuu za query syntax. Tutaona mifano ya msingi ya Where, Select, OrderBy, GroupBy, Join, na nyingine.
Katika somo hili tutajifunza LINQ advanced methods ambazo hutumika kwa uchambuzi wa data na kupata matokeo ya haraka: Aggregate Any All First Single Count Sum Average Max Min Tutaziona kwa mifano midogo midogo na mwisho tutaunganisha kwenye mfano mkubwa.
Katika somo hili tutajifunza: Maana ya synchronous na asynchronous programming. Nini maana ya Thread. Nini maana ya Task. Nini maana ya Task.Run().
Katika somo hili tutajifunza: Namna ya kusubiri Task (Task.Wait). Namna ya kupata matokeo kutoka Task (Task.Result). Kufanya kazi nyingi sambamba (Task.WhenAll). Kusubiri kazi yoyote ikamilike (Task.WhenAny).
Katika somo hili tutajifunza: Tatizo la kutumia Task.Wait() na Task.Result. Nini maana ya async. Nini maana ya await. Jinsi ya kuandika method asynchronous.
Katika somo hili tutajifunza: Kuunganisha async/await na Task.WhenAll. Kutumia Task.WhenAny. Kufanya kazi nyingi zinazotoa matokeo. Kutumia Task.Delay kama mfano wa kazi ndefu. Faida za kutumia mbinu hizi.
Katika somo hili tutajifunza: Tofauti kati ya multithreading, tasks, na parallel programming. Kutumia Parallel.For na Parallel.ForEach. Faida na changamoto za parallel programming.
Katika somo hili tutajifunza: Delegate ni nini na matumizi yake. Jinsi ya kufafanua na kutumia delegates. Multicast delegates. Events na event handling. Mifano midogo midogo ya kueleza kila kipengele.
Katika somo hili tutajifunza: Keywords muhimu kwenye event handling. Jinsi ya kufafanua event na subscriber. Aina kuu za events. Jinsi ya kuandika custom event. Orodha ya built-in events katika .NET. Angalizo kwa console vs applications halisi.
Katika somo hili, tutajifunza: Wapi events zinahitajika katika program. Faida za kutumia events. Aina za situations ambapo event inakuwa muhimu. Mifano rahisi ya vitendo. Angalizo la console vs UI apps
Katika somo hili tutajifunza: Nini maana ya file handling. Class muhimu za C# kwa file I/O. Ku-create, read, write, append files. Mifano midogo midogo ya vitendo.
Katika somo hili tutajifunza: Jinsi ya kusoma text files kwa njia tofauti. Jinsi ya kuandika text files kwa njia tofauti. Methods muhimu za StreamReader na StreamWriter. Mifano midogo midogo kwa vitendo.
Katika somo hili tutajifunza: Nini maana ya binary files. Class muhimu za binary file handling: FileStream, BinaryReader, BinaryWriter. Jinsi ya kusoma na kuandika data binary. Mifano midogo midogo ya vitendo.
Katika somo hili tutajifunza: Class muhimu za kusimamia files na directories. Kuangalia existence ya files/directories. Ku-create, delete, copy, move files na directories. Methods muhimu za Path class. Mifano midogo midogo ya vitendo.
Katika somo hili tutajifunza: Kwa nini file operations zinahitaji exception handling. Exceptions za kawaida kwenye file operations. Kutumia try-catch-finally na using. Best practices kwa file handling. Mifano midogo midogo ya vitendo.
Katika somo hili tutajifunza: Nini maana ya library na package. Kwa nini tunatumia libraries na packages. Aina za libraries. Mifano midogo midogo ya kutumia libraries.
Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutumia maktaba (libraries) zilizopo tayari kwenye C# tukitumia Rider IDE. Tutazungumzia maana ya library, aina zake, jinsi ya kuzitumia kwa using, na jinsi ya kuinstall maktaba mpya kupitia NuGet (ambayo Rider nayo inaiunga mkono moja kwa moja).
Katika somo hili tutajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza library (DLL) yetu wenyewe, kisha kuitumia kwenye project nyingine. Library yetu itakuwa na class rahisi yenye method chache.
Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kugeuza library tuliyotengeneza kuwa NuGet package (.nupkg), kisha kuisambaza na kuitumia kwenye project nyingine.
Katika somo hili tutajifunza aina kuu za libraries na packages kwenye .NET, jinsi zinavyotofautiana, na wakati gani tutazitumia.
Katika somo hili tutajifunza: Database programming ni nini kwenye C#. Utangulizi wa ADO.NET (mfumo wa .NET wa kuwasiliana na database). Vipengele muhimu: Connection, Command, DataReader, DataAdapter, DataSet. Tofauti kati ya MySQL na SQLite. Jinsi ya kuandaa Rider IDE ili tuweze kutumia MySQL na SQLite kwenye miradi yetu ya C#.
Katika somo hili tutajifunza: Connection string ni nini na vipengele vyake. Jinsi ya kufungua na kufunga connection kwa MySQL na SQLite. Hatua za msingi: Open(), Close(), na Dispose(). Kutumia using statement ili kuepuka memory leak. Mifano ya connection kwa MySQL na SQLite.
Katika somo hili tutajifunza: Kutumia MySqlCommand na SQLiteCommand. Jinsi ya kuandika na kutekeleza queries. Kufanya INSERT, UPDATE, DELETE. Kusoma data kutoka kwenye database kwa kutumia SELECT. Umuhimu wa kutumia using na parameterized queries (kuepuka SQL Injection).
Katika somo hili tutajifunza: Kutumia prepared statements kwa queries zenye parameters. Kuandika parameterized queries ili kuzuia SQL injection. Tofauti ndogo za syntax kati ya MySQL na SQLite. Mifano ya INSERT, SELECT, UPDATE, DELETE kwa prepared statements.
Katika somo hili tutajifunza: JSON ni nini na kwa nini inatumika. Libraries zinazotumika kusoma na kuandika JSON kwenye C#. Kufanya serialization (object → JSON). Kufanya deserialization (JSON → object). Kusoma na kuandika JSON moja kwa moja kutoka/kwa files. Dynamic JSON na LINQ to JSON. Kutumia System.Text.Json (modern library ya Microsoft). Kutumia Newtonsoft.Json (popular library). Best practices na error handling.
Join thousands of students who are advancing their careers with BongoClass
Enroll Now