4. The fastest (anaekwenda mbio zaidi)

Wanyama ni viumbe wanaoishi baharini, mchikavu na wengine wanaishi majini. Wanyama wameggawanyika katika kakundi mengi kuna wanyama ambao ni samaki, kuna wanyama ambao ni mamalia, na kuna wanyama ambao ni ndege. Katika nchi kavu tembo ndiye mnyama mkubwa kuliko wote. Kwa upande wa majini nyangumi ndiye mnyama mkubwa kuliko wote. Halikadhalika wanyama wamekuwa wanasifika kwa sifa mbalimbali. Katika makala hii tutaangalia mnyama anayekwenda kwa kasi zaidi kuliko wote.

pic
Cheetah ni katika wanyama wenye maajabu sana. Katika makala ijayo tutakuja kumuona huyu mnyama kwa undani zaidi. Inasemekana mnyama huyu anaweza kukimbia kwa mwendo wa kasi sana, na pengine ndiye mnyama anayekwenda kwa kasi zaidi kuliko wanyama wote. Mnyama huyu anaweza kutembea kwa mwendo kasi wa kilomita 93 kwa saa (93km/h). Tafiti zinaonesha kuwa mnyama huyu hukata tamaa pindi anapomkumbiza mnyama kwa umbaliwa mita 300 bila ya kumpata, zipo sababu juu ya jambo hili tutaona kwenye makala ijayo. Hivyo huyu ndiye mnyama mwenye mwendo kasi zaidi nchikavu.

pic Sailfish ni katika samaki wanaopatikana karibia bahari zote. Samaki hawa wanasifa ya kutembea kwenye makundi. Na wanajipatia chakula chao kwenye kina kirefu na kina cha kati. Samaki hawa inasemekana ndiye katika samaki wanaokwenda kwa mwendokasi zaidi majini. Sail fish anaweza kuntembea kwa mwendo kasi wa kilomita 105 kwa lisaa (105km/h). Kama unavyomuona kwenye picha hapo juu Sail fish wanakuwa na ncha mbeleni na hii inawasaidia zaidi katika kuyakata maji kisawasawa.

pic
Swift ni ndege anayechukuwa rikodi ya kwenda mwendo kasi zaidi kuliko ndege wote na kuliko wanyama wote pamoja na samaki. Anaweza kwenda kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa lisaa (160km/h).