1. Bezoa goat (mbuzi pori)

beroar
Huyu ni mnyama aliyefanana sana na mbuzi isipokuwa huyu ana mapembe makubwa. Mnyama huyu ni katika wanyama wenye maajabu katika dunia hii. Wataalamu wa sayansi na viumbe hasa wale waliobobea kwenye maisha ya wanyama mwitu, wannashangazwa sana na fahamu alizonazo mnyama huyu.

Wataalamu wanaeleza kuwa mnyama huyu amepewa anaitwa Bezoar goat kwa lugha ya kiingereza na jina hili asili yake ni kutoka katika lugha za kifurs kwa maana ya medicine yaani dawa. Na hii ni kutokana na uwezo wake wa kujitibu pindi anapong’atwa na nyoka.

Mnyama huyu anaishi eneo ambalo mimea aina ya Euphorbia inapatikana. Mnyama huyu pindi anapong’atwa na nyoka haraka sana anawahi kula majani ya mimea hii na hatimaye sumu ya nyoka inakosa nguvu na mnyama huyu haendeleu kudhurika.

beroar Kwa ufupi mnyama huyu ni katika wanyama wachache ambao wanaweza kujitibu dhidi ya sumu ya nyoka. Mwenyezi Mungu aliyetukuka ndie aliyempa elimu hii ya kujuwa tiba hii, kwani wapo wanyama wengi msituni waking’atwa na nyoka hawawezi kujitibu.

Mwenyezi Mungu mtukufu anatupa sisi masingatio kupitia maisha ya viumbe. Tukumbuke kuwa Mwenyezi Mungu ndiye ana uwezo wa kila kitu. Anampa elimu amtakaye katika viumbe vyake na anamnyima amtakaye. Atakayepewa amshukuru Allah na atakaye nyimwa pia amshukuru.