PROJECT 4 MAFUNZO YA PHP LEVEL 1 UKUSANYAJI WA DODOSO LA TAARIFA ZA SENSA

Project hii itakupa mwanga jinsi ya kukusanja maswali na madodoso mengine kwa kutumia HTML form na PHP. Katika masomo yanayokuja utajifunza namna ya kuzikusanya dodoso hizi na kuziwka kwenye database.

DODOSO LA USAJILI

Katika program hii mtumiaji ataweza taarifa zake kisha zitakuja kama alivyoziweka. Program hii itakusaidia utakapokuja kujifunza namna ya kudisplay taarifa kutoka kwenye database. Kwa sasa hatutatumia database ila somo litakalofata taarifa hizi moja kwa moja zitatola kwenye database baada ya mtu kujiajili.

 

Program hii itatumia mafaili mawili. Moja ni la HTML kwa ajili ya kukusanya madodoso. Kisha faili lingine litakuwa ni kwa ajili ya kudisplay taarifa zilizojazwa. Katika faili la HTML kwenye action utakuta kuna link ya faili linalofata ambalo ndilo litakalopelekewa taarifa zilizojazwa kwa ajili ya kuchakatwa.

 

Ijapokuwa unaweza kuchanganya mafaili haya sehemu moja ;akini nimependelea kuyatengenisha kwa ajili ya kujifunza zaidi. Hivyo kama ndio na wewe unaanza weka mafaili mawili. Kisha faili m,oja ni la htm;l code na la pili ni kwa ajili ya php code.

 

Katika program hii faili la kwanza nimeliita index.html ambalo litabeba php code na la pili script.php ambalo litabeba html code. Bofya hapa kuangalia project hii live. Ama fuata link hii https://www.bongoclass.com/mafunzo/php/p.php

Kimeandikwa na Rajabu Terehe 2023-02-28