Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu string indexing. Kama tulivyojifunza kuhusu namba katika somo lililopita, basi hapa tutakwenda kucheza na string.
Indexing:
Unapopewa string yeyote, katika python unaweza ku access yaani kufanyia kazi sehemu tu ya string hiyo na kuacha sehemu nyingine. Huko nyuma tulijifunza kuhusu habari hii ya indexing na nikakueleza kuwa string index inaanzia na 0. Sasa katika somo hili tutainga ndani zaidi katika kuijuwa indexing.
Katika somo letu hili tutakwenda kuifanyia kazi string hii ‘Jifunze python na Bongoclass”
Mfano 1:
Katika mfano huu tutaona jinsi ya kufanya index kwa character ya mwanzo tu. yaani tunataka ku dislay haerufi ya mwanzo tu ambayo ni j. Kama nilivyokueleza kuwa indexing inaanzia na 0. Kwa hiyo character ya mwanzo itakuwa na index ya 0.
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[0])
Hii itatupa jibu j
Mfano 2:
Kwa kupitia mfano huo unaweza ku display character yeyote unayotaka kwenye string yetu. Sasa kwa mfano tunataka ku display character ya 12 kwenye string.
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[12])
Hii itakupa jibu o
Mfano 3:
Saa kwa mfano tunataka kudisplay character ya mwisho to, hapa unaweza kuhesabu ilikujuwa ipo index ya ngapi kisha utatumia mfano uliotangulia. Njia nyingine ni kutumia negative number yaani namba hasi.
Index inapokuwa na namba hasi maana yake imeanza kuhesabiwa kutoka mwisho. Sasa ukihesabu kutoka mwisho index haianzi na -0 ila inaanza na -1 kwa kuwa -0 itakuwa ni ile character ya kwanza kwenye index. Hivyo basi kupata character ya mwisho tutaandika hivi
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[-1])
Hii itatupa jibu s
Mfano 4:
Kwa mfano kama huo ukitaka ku display character ya 4 kutoka mwisho tutatumai -4
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[-4])
Hii itakupa jibu l
Mfano 5:
Pia unaweza ku display character zilizobaki kuanzia index ulioitaka. Mfano ninataka ku display kutoka character ya 8 hadi mwisho. Kufanya hivi utaandika index ya 8 ikifuatiwa na nukta pacha.
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[8:])
Hii itatupa jibu python na Bongoclass
Mfano 6:
Kwa kutumia negative index unaweza pia kufanya hivyo. Ila utambuwe kuwa negative index itahesabu kuanzia -1 kutoka mwisho, kisha ikishapata idadi ya character ita display hizo character kutokea hapo kwenda mwisho yaani kule ilipoa anzia.
Katika string yetu ukitaka ku display neno bongoclass kwa kutumia negative indexing hapo kama utahesabu vyema herufi B ipo character ya 8 kutoka mwish yaani -8. Sasa kama utataka ku dsplay neno bongoclass kwa kutumia negative index itaanza hapo kwenye index ya -8 na kurudi tena kwenye index ya -1 ndipo itapata neno bongoclass
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[-10:])
Hii itatupa Bongoclass
Mfano 7:
Pia unaweza ku display string yote kwa kutumia negative indexing. Ukiweza index ya negative -0 utaanzia mwanzo hadi mwisho
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[-0:])
Jifunze python na Bongoclass
Mfano 8:
Pia unaweza kudisplay character kutoka mbele kwenda nyumba zote. Mfano ninataka ku display kutoka ccharacter ya 4 kurudi mwanzo. Hapo tutaanza na hizo nukta pacha ikifuatiwa na hiyo index
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[:4])
Hi itatupa jibu jifu
Mfano 9:
Kwa mfano kama huo ukitumia negative index nayo itahesabu character 4 kutoka mwisho kisha itadisplay zote zilizobaki.
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[:-4])
Hii itatupa jibu Jifunze python na Bongoc
Sasa tunataka ku display kifungu maalumu tu cha hiyo string yetu, kwa mfano ninataka ku display neno python kutoka kwenye string yetu. Kwa mifano iliyotangulia hicho kitu hakiwezekani. Ili kiwezekane kwanza ujuwe je hilo neno liaanzia index ya ngapi na kuishia ya ngapi.
Mfano 10:
Kwa mujibu wa string yetu neno python linaanzia index ya 8 na kuishia index ya 15. Hivyo nikitaka ku display neno pythone nitaweka 8 ikifuatiwa na nukata pacha kisha zitafuatiwa na 15
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[8:15])
Hii itatupa jibu python
Mfano 11
Pia unaweza kufanya hivyo kwa kutumia negative indexing.
string = 'Jifunze python na Bongoclass'
print(string[-20:-14])
Hii itatupa jibu python
Mwisho
Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunza zaidi kuhusu string method nyinginezeo
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-21 Download PDF Share on facebook WhatsApp