Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu number method yaani function zinazofanya kazi kwenye namba.
Matendo ya hesabu
Katika mahedabu Kuna matendo makuu manne ambayo ni:-
Kujumlisha
Kutoa
Kuzidisha
Kugawanya
Kujumlisha
Kama ilivyo kwa lugha nyinginezo hata katika python unapojumlisha utatumia alama ya +. Unaweza kujumlisha variable kwa variable ambazo zinawakikisha namba
Mfano:
a = 5;
b=6;
print(a+b)
Hii itakupa jibu 11;
Pia unaweza kujumlisha kweli list
a = [2,4,6,7]
print(a[2] + a[1])
Hii itatupa jibu 10 kwa kuwa index ya 2 ni 6 na index ya 1 ni 4. Hivyo ni sawa na kusema 6+4.
Pia unaweza kujumlisha namba hasi na chanya chanya na kupata matokeo yaleyale.
Mfano: print(-6 + 2) hii itatupa jibu 4
Kutoa
Kama tulivyoona hapo juu kuhusu kujumlisha basi na kutoa kunafuata kanuni zilezile tunatumia alama ya - Ili kutoa.
Mfano:
a = [2,4,6,7]
print(a[2] - a[1])
Hii itatupa jibu 2
Mfano
print(9-5)
Hii itatupa jibu 4
Kuzidisha
Katika kuzidisha tutatumia *
print(6*3)
Hii itakupa jibu 18
a = [2,4,6,7]
print(a[2] * a[1])
Hii itatupa jibu 24
Kugawanya
Katika kugawanya tutatumia /
Mfano:
print(10/2)
Hii itatupa jibu 5
a = [2,4,6,7]
print(a[2] / a[0])
Hii itatupa jibu 3.0
Tuingie ndani zaidi
Sasa tunakwenda kuingia ndani zaidi kwenye somo hili. Kuna case nitakuletea hapo chini:-
case 1:
print(10/3)
Hii itatupa jibu 3.3333333333333335
Utaona hapo imegawanya na kutuletea fesimali nyingi sana, baada ya kibaki. Sasa tutakwenda kutatuwa changamoto hii kwa namna mbili.
Kukadiria viwango vya desimali
Sasa tunataka hapo juu tukadirie viwango kadhaa vya desimali. Kufanya hivyo tutatumia round() function.
Function hii itakuwa na argument 2 ambazo ni namba husika na digit ambazo unataka zitokee kwenye viwango vya desimali. Namba na digit vitatenganishwa na alama ya koma (,)
Mfano tunahitaji kupata viwango viwili tu vya desimali.
namba = 10/3
print(round(namba, 2))
Hii itatupa jibu 3.33 utaona hapo tumepata viwango viwili tu vya desimali
Kuandika kiasi kilichobaki
Tofauti na kupata mrundikano wa namba za desimali, unaweza pia kuandika kiasi likichobaki TU. Katika mfano wetu hapo juu namba 10 ukiigawa kwa namba 3 itabaki Moja.
Kufanya hivi tutatumia function ya divmod() function hii itakuwa na argument 2 ambazo ni namba inayogawanywa na namba inayogawanya.
Na katika majibu itakuja hivyo hivyo namba ya kwanza itaonesha jibu na namba ya pili itaonyesha kilichobaki.
print(divmod(10,3))
Hii itatupa jibu (3,1) yaani jibu ni 3 na itabaki 1.
Case 2:
Tunahitaji kuandika zile namba zenye power yaani video na vipeuo. Mfano tunataka kupata majibu ya 2 kipeo Cha 3 yaani 2*2*2. Hii katika Hali ya kawaida huandikwa 23
Hapo 2 ndio huitwa base na hiyo 3 huitwa power. Katika python tunaweza kutekeleza hayo kwa kutumia pow() ambayo itakuwa na argument 2. Ya kwanza ni base na ya pili ni power.
print(pow(2,3))
Hii itakupa jibu 8
case 3:
Wakati mwingine unahitaji watu waingine namba kwa mfano unahitaji mtu ajaze umri wake. Sasa Kuna watu wanawezs kujaza -21 baada ya kuandika 21. Sasa hihesabu hizo ni namba mbili tofauti kabisa.
Kutatuwa tatizo Hilo utahitajikankubapa absolute namba, yaani namba halisi. Katika python function tutakayoitumia ni adb() ambayo itabeba argument Moja nayo ni hiyo namba.
pr
int(abs(-21))
Hii itatupa jibu 21.
Mwisho:
Somo linalofuata tutakwenda kujifunza zaidi kuhusu method nyinginezo.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-21 Download PDF Share on facebook WhatsApp