PYTHON - somo la 7: Jinsi ya kubadili aina ya data


imageKatika soo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubaduli aina moja ya data kwena aina nyingine. Kwa mfano unaweza kubadili namba kuwa string ama kubadili string kuwa nanda ama kubadili float kuwa int.Kwa nini somo hili ni muhimu?

Ili uweze kujuwa umuhimu wa somo hili nitakuletea case hapo chini ambazo zitaonesha umuhimu wa somo hili:-

1. Katika programming language kama python unapotumia user input prompt data zinakuja katuka hali ya string. Mfano program yako inahitaji mtu aweke umri wake. Sasa huo umri ataandika 24 kwa mfano. Lakini hiyo 24 itahesabika kuwa ni string, hivyo huwezi kuifanyia mahesabu. Hivyo basi utahitajika kuibadili kuwa aina ya data unayotaka kama integer ama float.

 

2. Katika python unapogawanya namba mbili jibi linakuja katika mtindo wa floaf yaani namba zeye desimali. Hivyo wakati mwingine itahitajika uzibadili kuwa integer ili uweze kuifanyia mahesabu.

 

Jinsi ya kubadili ainaza data

1. Kubadili data kuwa namba yaani integer

Ili uweze kubadili data kuwa int utatumia function ya int(), itabeba argument moja ndani yake ambayo ni hiyo data.

 

Mfano:

print('5' +5); Hii itakuletea error kwa sababu 5 ya kwanza ni string na hiyo ya pili ni int. Hivyo basi tutibadilisha hiyo ya kwanza kuwa int

print(int('5') +5) hii hapa itakupa jibu 10  kwa kuwa data zetu zote zipo katika format moja ya int

 

2. Kubadili data kuwa string:

Ili kubadili data kuwa str tutatumia function hii str() na itabeba argument moja ambayo ni hiyo data yako. Kwa mfano print(type(5)) hii itatupa jibu int kumaanisha kuwa hiyo 5 ni integer. Sasa tunataka iwe string.

 

Kwanza tutatengeneza variable kuwakilisha namba 5, kisha tutaibadili hiyo namba kwa kutumia variable tuliotengeneza. Kisha tuta angalia aina ya data ya hiyo variable baada ya kuibadili

a = 5

a= str(a)

print(type(a))

 

Hii itatupa jibu string. Pia unaweza kuiandika kama hivi print(type(str(5)))

 

3. Kubadili data kuwa float

Function inayotumika kubadili data kuwa float ni float(). Kwa mfano unataka kuandika namba 5 kwa mtindo wa 5.0 hapa tutafanya print(float(5))Hii itatupa jibu 5.0.

Pia unaweza kuangalia ina yetu mpya ya data kwa print(type(float(5)))Hii itakupa jibu float.

 

4. Kubadili data kuwa boolean

Hizi ni data za True na False, ili uweze kubadili data kwenye mtindo huu utatumia function ya bool(). Mfano neno “True” na True sio sawa unaweza kucheki kwa code hizi print("True" == True)hii itatupa jibu la False. Lakini kama tutaibadili true ya kwanz akuwa bool itakuwa ni sawa print(bool("True") == True)

Hii itatupa jibu la True. Pia unaeza kuicheki aina ya data 

print(type('True'))Hii itatupa jibu kuwa ni string lakini hii print(type(bool('True')))Itatupa jibu la bool

 

Mwisho:

Katika somo linalofuata tutajifunza kufanya mahesabu mbalimbali kwa kutumia pythonJe! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-21 Download PDF Share on facebook WhatsApp

RELATED POSTS

picha

Katika somo hili utajifunza kuhusu maana ya python na kazi
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza syntaxy za python yaani sheria
picha

Katika somo hili utajifunza jisni ya kujuwa aina ya data
picha

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu string indexing. Kama tulivyojifunza
picha

Katika somo hili utajifunza maana ya variable, na sheria za
picha

Katika somo hili tunakwenda kujifunza aina nyingine za data ambazo
picha

Katika somo hili utakwenda kujfnza kuhusu string method nyinginezo. Katika
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data ambazo hutumika
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu operator. Hasa hapa tutakwend
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu number method yaani function